Kulikuwa na uvumi kuwa kiungo wa Real Madrid, Eduardo Bamavinga ana umri wa miaka 19 na mwanaye ana miaka 8. Hali inayooonesha kuwa alimpata mtoto huyo akiwa na miaka 11.
Picha1: Camavinga akiwa na mtoto aliyehisiwa ni mwanaye
Picha2: Camavinga akiwa na wazazi wake na ndugu zake
Picha1: Camavinga akiwa na mtoto aliyehisiwa ni mwanaye
Picha2: Camavinga akiwa na wazazi wake na ndugu zake
- Tunachokijua
- Mnamo Mei 28, 2022 baada ya mchezo wa fainali wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Liverpool ya Uingereza dhidi ya Real Madrid ya Uhispania, Wachezaji mbalimbali walipata fursa ya kupiga picha za kumbukumbu na familia zao.
Eduardo Camavinga mchezaji wa Real Madrid aliyekuwa na miaka 19 wakati huo alionekana akipiga picha na mtoto wa miaka 7. Baada ya kusambaa kwa picha hiyo fununu na habari zilienea zikidai mvulana huyo alikuwa ni mtoto wa Camavinga. Mijadala mingi ilihoji inawezekanaje Camavinga mwenye miaka 19 awe na mtoto wa miaka 7, Wanajiuliza je Camavinga alimpata mtoto huyo akiwa na miaka 12?
Ukweli upoje?
Baada ya kufuatiliwa imebainika kuwa mvulana huyo aliyepiga picha na Camavinga si mwanaye bali ni mmoja wadogo zake kutoka kwenye familia yake yenye watoto watano (Tazama picha namba 2). Eduardo yupo na kwenye mahusiano na mwanamitindo wa Ufaransa na bado hawajapata mtoto.
Camavinga alizaliwa katika kambi ya wakimbizi huko Cabinda, Angola mwaka wa 2002, na wazazi wa Kongo. Ni mmoja wapo katika familia yenye watoto watano. Familia yake ilihamia Ufaransa alipokuwa na umri wa miaka 2.
Jarida la Kimtandao la Ghpluzz lilifuatilia pia habari hii na kuthibitisha kuwa anayeonekana kwenye picha ni mdogo wake Camavinga na sio mtoto wake.