The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kibamba kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Edward Kinabo, Septemba 8, 2025, ameendelea na kampeni zake za mtaa kwa mtaa katika Kata ya Goba, mtaa wa Matosa, akihamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura.
Kinabo amemuita mgombea Ubunge wa CCM Anjellah Kairuki katika jimbo hilo kushiriki naye katika mdahalo wa wazi mbele ya waandishi wa habari ili kila mgombea aeleze sera zake na wananchi wapime hoja kujua nani anafaa. Amesema wananchi wa Kibamba hawapaswi "kuuziwa mbuzi kwenye gunia" bali wapewe nafasi ya kutathmini wagombea kwa uwazi.
Ameongeza kuwa CCM walidhani watapita bila upinzani baada ya CHADEMA kutojiridhisha kushiriki uchaguzi jambo ambalo limeshindikana kwani baadhi akiwamo yeye mwenyewe Kinabo walijiondoa CHADEMA ili kuhakikisha wanatoa changamoto kwa CCM