Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Mkuu hebu kuwa realistic hivi huwa mnamaanishaga nini mnaposema CHADEMA imesalimu amri kwenye hoja ya ufisadi?

Mnaweza mkathibitisha kuwa kuna ufisadi umefanyika halafu CHADEMA wakashindwa kuusemea? Huwa wenzetu mnatumia kipimo gani?.
Ukiipima CHADEMA kupitia CHADEMA utakuwa unakosea sana. CHADEMA ipime dhidi ya mitazamo ya wananchi inayotokana na pia uchochezi toka kwa wapinzani wa CHADEMA.

Ndani ya CHADEMA bado tunaamini kwamba tunapambana na ufisadi, lakini ni kweli kwamb watu wengi sana wanatumia kupokelewa kwa Lowassa kama ni kukengeuka kwa CHADEMA kwenye mapambano dhidi ya Upinzani.
 
å KABLA LOWASSA HAJAIHAMA CCM.

" Atakae muunga Mkono LOWASSA akapimwe akili haraka"
~Peter Msigwa~

å BAADA YA LOWASSA KUJIUNGA CHADEMA( WAKAT WA KAMPENI)

"LOWASSA ndiye suluhisho la dhuluma na Maendeleo hafifu ya taifa hili tangu Uhuru, chagua LOWASSA chagua CHADEMA"
~Peter Msigwa~

å BAADA YA LOWASSA KURUDU NYUMBANI "CCM".

" Kama kunajambo la maana kubwa LOWASSA ameifanyia CHADEMA ni kuondoka CHADEMA kurudi CCM "
~Peter Msigwa~

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Weka na nukuu za wana CCM!!
 
Mzee Mwanakijiji, hapo ndo unapoonesha unafiki. Haijalishi Slaa ana kadi ya CCM au hana. Kwani Chama ni nini? Suala ni kwamba sasahivi Slaa yupo timu moja na Lowassa. Hicho ni chama tayari. Kama hoja ya Slaa kuondoka Chadema ni kutokana na kutoridhishwa kwake na ujio wa Lowassa, kwa mantiki hiyohiyo, ni kwanini Slaa asijitoe CCM (ubalozi aliopewa kutekeleza ilani ya CCM), hata kama asiporudi Chadema? Unasema "Slaa anaweza kujisemea mwenyewe". Mbona wewe unajivika hadhi zaidi ya aliyonayo mke wa Lowassa kwa kwa kujifanya unajua sana dhamira na mawazo ya Lowassa kuanzia alivyokuja Chadema mpaka kuondoka? Yaani umepata taarifa za ndani kiasi hicho kuhusu Lowassa lakini umeshindwa kupata taarifa za ndani za kiasi hichohicho za Lowassa?




 
Swali langu still valid je ni ufisadi gani uliofanyika CHADEMA ikauvalia njuga watu wakawapuuza?

Ni lazima tuwe realistic tuache kuwa idealistic tangu alipoingia CHADEMA Lowassa wachambuzi walikuja na hoja hiyo. Mpaka sasa hakuna ushahidi wa kwamba CHADEMA wanapuuzwa na wananchi wakiongelea ufisadi labda unipe ushahidi hali ipoje na ilikuwaje huko nyuma?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
MWEMBESI ONE mimi ni mwana-CHADEMA na siasa kwangu ni jambo la kila siku. Ninachosema kuipima CHADEMA kutumia sisi wana CHADEMA si sahihi na si sahihi kwamba "wananchi" wanaipuuza CHADEMA lakini ni ukweli pia kwamba wapo waliokatishwa tamaa na kupokelewa kwa Lowassa.

Kila siku sisi wengine tupo "Field" na swali la kwa nini tulimpokea Lowassa linaulizwa. Kwa kiwango fulani lazima tukubali kwamba CCM walifanikiwa sana kwenye propaganda yao hii.
 
Kwa kuwa hana kadi halali inayolipiwa atabaki kuwa siyo mwanaccm tu. Hakunaga "implied membership" swala la uanachama ni lazima ufuate utaratibu.

Hata cheo alichopo hakimfanyi achangamane na CCM sana hebu tumpe benefit of doubt kwa sasa.
Sent using Jamii Forums mobile app
 


What's membership? How does "gang" membership get identified? Cheo alicho nacho Slaa kinamuhusisha kwa karibu zaidi na matendo ya CCM kuliko hata Wanachadema wengine wengi wa kawaida waliojiunga na CCM lakini mpaka sasa hawana cha kufanya huko CCM. Slaa is actually directly implementing the CCM manifesto.
 
Now you are talking. Tupo tulioumizwa sana na uamuzi ule.
 
Waliokatishwa tamaa lazima wawepo hilo sikatai, na watu lazima waulize kwanini mmempokea Lowassa na hata angepokelewa Mwandosya au Membe, au mwasira people must ask why importing a candidate? Lakini huwezi kuniambia eti Lowassa ni big deal kiasi cha chama kushindwa kupambana na ufisadi how that be an obstacle?. Kama mtu kama JPM ana ujasiri wa kutamka neno fisadi anatangaza vita ya ufisadi anaeleweka, mtu ambaye binafsi tu anakashfa za ufisadi za nyumba za serikali, vivuko vibovu nk, leave that along hajawahi kupinga ufisadi wa JK, yupo kwenye cabinet kuanzia ufisadi wa Ben, JK kashfa zote za Richmond, EPA nk hakuongea kitu. Achana hilo yupo chama kimoja na watuhumiwa wote wa ufisadi isipokuwa Lowassa. Mtu huyu anabeba ajenda ya ufisadi na anaaminika.

Then, unasemaje CHADEMA ishindwe kupambana na ufisadi? Au unaungana na JPM kuwa mafisadi wote wamekimbilia CHADEMA? Wako wapi hao mafisadi? Mimi ni mtu ambaye sishabikii kirahisi hawa wanaoitwa wachambuzi huwa wana overrate sana mambo wakiamua kukuza na kukidisqualify kitu.

Hakuna namna Magufuli aweze kutamka sembuse kupinga ufisadi yet ndani ya chama chake ana watuhumiwa wa ufisadi kama wote, in fact chama chake ndiyo kimepelekea huo ufisadi halafu eti akina Mnyika, Lissu, Mbowe, Mdee nk waitupe ajenda ya ufisadi kwa sababu tu Lowassa yupo CHADEMA. Huku ni kukuza mambo ndugu yangu. Ukisema CHADEMA imetupa agenda ya ufisadi lazima useme hiyo agenda ipo kwa nani siku hizi.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimepitia maoni yako hata hivyo hoja zako nyingi ni self centred,ni mawazo yaliyosheheni hisia binafs!!!Kwa maoni yangu umeonesha udhaifu mkubwa kuaanda maada iliyojaa hisia zako binafsi!!!!Sijaona objectivity kwenye hoja zako hata hata hvyo naheshimu maoni yako!!
 
MWEMBESI ONE Hoja yangu ni rahisi sana. Kuna baadhi ya wana-CHADEMA tena wengine ni viongozi wa ngazi ya Kamati Kuu waliwaaminisha watanzania kwamba Lowassa ndiyo alama ya ufisadi na ndiyo ufisadi wenyewe.

Kuna msemo unaosema kuwa "Haki ni lazima itendeke na ionekane inatendeka". Hii ina maana kubwa sana kwenye siasa. Hata kama sisi CHADEMA tunapambana na ufisadi jee wananchi walikuwa wanaona tunapambana na ufisadi wakati Alama ya Ufisadi ilikuwa kwetu?
 
Hivi unafikiri akina mnyika na mbowe kule bungeni wanaimplement manifesto za nani? Vipi akina Meya Jacob pale ubungo na madiwani wa CHADEMA nchi nzima wana implement llani ya CHADEMA?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Slaa hakushiriki kumleta Lowassa CHADEMA hiyo source yako iangalie vizuri sana!.. Maamuzi yalifanywa na Mbowe yakalazimishwa yakubaliwe na Kamati Kuu.
Ukikumbuka hata Slaa mwenyewe alilitolea ufafanuzi na akasema Tundu Lissu alisema "Kama ni kuiondoa CCM madarakani kwa kusaini mkataba na Shetani bora iwe!".
Dr. Slaa alitoa maoni tu EL akaribishwe lakini sio kupewa madaraka makubwa kiasi kile na ndio swali kubwa zaidi aliuliza "Lowassa ni ASSET au LIABILITY!?".
 
Hili swala linakuzwa sana lakini halina uhalisia, Lowassa alitajwa na Dk Slaa kwenye list of shame sambamba na majina mengine, serikali ya JK mpaka 2015 imekuwa na kashfa nyingi za ufisadi na washukiwa wengi Lowassa hakuwa na uziada wowote labda wewe ndiyo uniambie uziada wa kashfa za Lowassa dhidi ya washukiwa wengine.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…