Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

TATIZO NI KUWA UVCCM MLITEGEMEA KUONA POST NYINGI TOKA CHADEMA ZA KUMPONDA LOWASA, LAKINI IMEKUWA KINYUME. HIVYO IMNAANZA KUWEWESEKA KWA KUWA MLILOTEGEMEA HALIKUTOKEA
 
lini lowassa alienda ccm?acha kiwewe

Jinga kwa yuko wp nw dr slaa kadi ya chama ccm anayo tena iko active tu na sasa ivi lowassa nae anayo tena mpya tu vp taarifa ya lumumba azijakufikia tu bado badilisha vyanzo vyako vya habari mkuu unapitwa na wakat


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nimependa mchango wako maana una hoja za msingi hata kama sizikubali. Sasa tuje kwenye mtazamo wangu kuhusu huyo Lowassa. Hivi Lowassa anakubalika kwa nyota au uliwahi kumuona akihutubia ukasikia falsafa zake? Lowassa nimjuaye mimi ni mtu ambaye sifa zake zinahubiriwa na wapambe na sio yeye. Hata cdm walimchukua kwa sifa za kusikia sio kwa uwezo halisi waliojiridhisha nao. Kikubwa ambacho sina shaka nacho, uwezo wake wa kipesa ambao vyanzo vyake havifahamiki ndio vilivyompa sifa zinazohubiriwa lakini sio uwezo wa kisiasa wa dhahiri.

Viongozi wa cdm nitaendelea kuwalaumu na hata kuwadharau kwakuwa cdm hizo kura milioni sita wangezipata hata kama wangenisimamisha mimi kwani ilikuwa inakubalika. Baada ya uchaguzi wa 2010-2015, cdm walianzisha operation mbalimbali nchi nzima za kupata wanachama na kupandisha hamasa kwa wananchi, na wao ndio chama kilichofanya mikutano mingi au wajibu wa chama cha siasa kuliko vyama vyote. Hata hamasa ya watu kujiandikisha na kitambulisho cha kura kuitwa kichinjio ni kwakuwa watu walijua Lowassa ndio atakuwa mgombea wa ccm ili wamchinje. Viongozi wa cdm bila kujali ukweli huu wakaingia tamaa ya pesa na kumchukua mtu ambaye hakuwa na uwezo halisi zaidi ya sifa za propaganda pekee. Hata huko ccm ambako Lowassa alikuwa anaonekana tishio ni lini ulimuona akikijenga zaidi ya kugawa pesa chafu chini ya meza na watu kumsifia? Ni lini toka Aachie uwaziri mkuu uliwahi kumuona akiongea hata dakika 10 ukavutiwa na speech yake?

Hata kama ni kutaka kuitoa ccm na kushirikiana na shetani ndio hiyo kumsimamisha mtu anaongea dakika chini ya 3 kwa kusema kipaombele changu ni "Elimu, elimu, elimu, au Lowassa mabadiliko, mabadiliko Lowassa" Mkuu hata uandike kitabu kuhusu Lowassa, nitafurahia uandishi wako lakini sio msaada wa Lowassa ndani ya cdm. Mbowe na genge lake wanapaswa kutuomba radhi watu tuliopigania mageuzi ya kweli na kisha kutuletea mtu aliyetaka urais badala ya mabadiliko.
Hoja zako zimewakilisha wengi nami ni mmoja wao. Kweli tupu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lowasa alikuwa Chadema akaenda CCM watu wakaona ni Jambo la kawaida na wengine wakiwemo Chadema wakafurahia kuondoka kwake huko CCM akapokelewa kama mwanachama asiye na impact kwao huku baadhi wakijutia kumpokea.

Leo hii nassar amevuliwa ubunge watu wanazungumzia suala lake na mijadala imekuwa mipana kuliko hata yeye mwenyewe alivyokuwa anadhani. Wapo wanaomwona ni mzembe kukaa nje ya BUNGE bila ruhusa, wapo wanaoamini alidhamiria, wapo wanaoamini ni mpango wake kuekea CCM na wengine wanakubaliana naye kwamba ameonewa na hivyo aende mahakamani.

Watu Hawa wawili wanatufundisha Nini , Nassary alionekana shujaa zaidi alivyokuwa Chadema na wananchi walimuunga mkono bila kujali umri wake. Lakini pia yeye wenyewe anayo haki ya kurejesha Imani kwa wananchi kwa kuendelea kupigana Vita ya kweli au vinginevyo ahamie upande wa pili apigane Vita ya mabua.

Lakini pia graph yake ikishuka itamchukua MUDA kumpandisha kwani dhambi iliyommaliza Lowasa na Sasa si kitu Tena ni dhambi ya kuwasaliti waliouzunika nawewe.

Wanaoshawishi nao wamewekwa na watu na wanaweza kuondolewa wakaondoka na wewe.....Jenga msingi imara wa maisha take kwa kusimama imara kuliko kuyumbishwa na wanaume wasiokuwa na hati miliki ya chochote Cha kesho yako.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom