Mmiliki wa kampuni maarufu duniani ya Rich Dad ambayo inajihusisha na utoaji wa elimu ya biashara Robert Kiyosaki katika kitabu chake cha Why I Want You To Be Rich (Kwanini Nataka Uwe Tajiri) alichaoandika kwa kushirikiana na mwekezaji na mfanyabiashara mwenzake bilionea Donald Trump alitoa tafsiri ya kiongozi.
Alizaliwa April 8,1947 Hawaii Marekani, mwandishi wa kitabu maarufu sana duniani cha Rich Dad, Poor Dad kinachohusu elimu ya biashara na matumizi ya fedha. Bilionea mwenzake Donald Trump ni moja ya wanasiasa wanaowania kugombea Urais wa Marekani kupitia chama cha Republican.
Katika kitabu hiki Robert Kiyosaki aliangalia maeneo makuu matatu katika tasfiri ya neno kiongozi, tafsiri ambayo ilihitimishwa na neno Mwalimu. Alitafsiri neno Kiongozi kwa kuangalia maneneo yafuatayo; kiongozi ni mfano wa kuigwa, kiongozi ni mhamasishaji na mwisho kiongozi ni mtu mwenye maono.
Tafsiri ya Robert Kiyosaki imenilazimisha nimuangalie Edward Ngoyai Lowassa, mgombea urais wa CHADEMA anayewakilisha vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) katika jicho la kisiasa na kiuongozi. Nguzo kuu ya tafsiri ya Robert Kiyosaki ni kujitambua; kutambua uwezo binafsi, upungufu, malengo na kuwa tayari kukabiliana na changamoto zinazojitokeza.
Kuna wakati malengo hukumbana na vikwazo hivyo hutoa wajibu kwa mhusika kusimamia maamuzi sahihi. Mtu anayeweza kumiliki mawazo yake hujikuta akitoa njia sahihi ya kukabiliana na changamoto tofauti na hivyo hujikuta anachanganyikiwa na kuwa mtu wa jazba katika maongezi na maamuzi.
Ni wanasiasa wachache sana ambao hukubali kulaumiwa pale ambapo wanafanya makosa, wengi wao kitendo cha kulaumiwa ni kitendo kiovu kisichopaswa kusikilizwa katika masikio yao. Edward Lowassa ni moja ya wanasiasa wachache katika taifa hili ambaye ametumbukia katika dimbwi la vita ya maneno, kukataliwa, kuvunjwa moyo, kusengenywa na kuchekwa.
Pamoja na kwamba Edward Lowassa amepitia katika vita hii ameweza kushinda nguvu za ndani (zake binafsi) na nguvu za nje ambazo zingemkatisha tamaa. Jambo kubwa ambalo tunajifunza kutoka kwa mwanasiasa huyu ni uvumilivu. Moja ya wanafilosofia wa Chuo Kikuu cha Arkansas kilichopo Marekani aliwahi kusema uvumilivu ni moyo wa maadili yanaoishi. Ni ukweli ulio wazi kuwa uvumilivu ni moja ya kazi ngumu zaidi katika jamii, ni jambo ambalo hatujazaliwa nalo lakini lazima tujifunze.
Katika siasa uvumilivu unakuza utamaduni wa utawala bora na ukomavu wa demokrasia; na kwa demokrasia kufanya kazi vizuri, viongozi lazima kuwa tayari kuvumilia yale wasiyopenda kusikia na kuonyesha ukweli na njia pale inapobidi. Edward Lowassa amekuwa mfano wa kuigwa kwa kufundisha falsafa ya uvumilivu kupitia uzoefu makini wa kimantiki.
Ametimiza kauli yake ya kufanya siasa za kistarabu aliyoitoa wakati wa kusaka wadhamini na kujitambulisha kama mgombea wa CHADEMA anayewakilisha UKAWA katika maeneo mbalimbali ya nchi, amekuwa muumini mzuri wa siasa za safi, amekuwa muumini mzuri wa Hayati Julius Kambarage Nyerere katika falsafa yake ya siasa safi na utawala bora na mwisho amekuwa mfano wa kuigwa si kama mwanasiasa tu bali kiongozi na Baba wa Familia.
Eneo la pili ambalo Edward Lowassa ameonyesha kwamba ni zaidi ya Mwanasiasa ni kuvunja minyororo ya kifikra kwa watanzania kufikiria maisha nje ya CCM. Watanzania ambao waligawanywa kwa woga, waliowekewa mipaka ya kushindwa sasa wamejengewa ujasiri wa kusimamia fikra na matamanio yao, wamekataa kuendelea kupigia magoti CCM. Lowassa amekuwa taa katika giza la kisiasa kwenye taifa letu. Ni mjenzi wa fikra mpya nje ya Chama Cha Mapinduzi.
Maelfu ya Watanzania wamejengewa ujasiri, hari na nguvu zaidi ya kudai mabadiliko ya kiuongozi na kisera kazi ambayo iliongozwa na viongozi wa vyama vinavyounda UKAWA kwa zaidi ya miaka ishirini na mbili. Edward Lowassa amekuwa kinara wa kuvunja fikra za woga kwa wanasiasa ambao wameshika nyadhifa za juu za kiserikali kupitia Chama Cha Mapinduzi.
Eneo la mwisho , Edward Lowassa ameweza kuyamiliki maono yake ya muda mrefu ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika historia tunasoma kwamba Kofi Anan baada ya kuingia katika ofisi za Umoja wa Mataifa kama mwajiriwa wa kawaida alimwandikia mama yake ujumbe na kumtaarifu kuwa siku moja lazima atakuwa katibu wa umoja wa mataifa. Maono haya yalimlazimisha kuwa na juhudi kubwa sana na hatimaye akafanikisha ndoto yake.
Edward Lowassa wewe ni zaidi ya Mwanasiasa.
Tutendee haki mioyo yetu bila wivu na husda bali lililojema kwa maendeleo ya taifa letu.
Naona ushindi wa Lowassa jumapili ya tarehe 25.10.2015.
Mungu Atatuvusha Salama.