Edward Moringe Sokoine tutakukumbuka daima, ulikuwa shujaa wetu watanzania

Edward Moringe Sokoine tutakukumbuka daima, ulikuwa shujaa wetu watanzania

Mmawia

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
122,494
Reaction score
96,074
Leo hii ni kumbukizi ya kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania na kipenzi cha watanzania mh Edward Moringe Sokoine kilichotokea 12.04.1984.

Marehemu alipata ajali ya gari akiwa njiani kutokea Dodoma kuelekea Dar es salaam ambapo alikuwa ameahirisha kikao cha bunge.

Watanzania tunazidi kumuombea pumziko la milele huko aliko.

Screenshot_20210412-145252.jpg
 
Mambo mengi sana kwa muda mfupi huu, yaani twashindwa hata tu stick kwenye lipi kwa sababu tu ya uninga wa baadhi ya wale tuliowapa madaraka ya kutuongoza

Huyu mwamba pia anasehemu na mchango mkubwa katika Taifa na ilitakiwa atengewe muda wa kujadiliwa yale mema yake

Lakini pia pamoja na kwamba kuna utata kwenye umauti wake mfano wa Mbunge wa wakati huo wa Tarime Chacha Zakayo Wangwe namna walivyoaga dunia na ukizingatia safari wote walikuwa wakitoka mkoa huo huo wa umauti

Na hata physical appearance zao kwa sisi wa kitambo unawezema na kuwaza hawa walikuwa ndugu wa tumbo moja au baba mmoja!?

Mkuu tumalizie viporo vyetu ambavyo bwa Mussa Assad katuanzishia kwa waandishi wetu kwwnda kumchokoza ili wapate maoni yake kama Mtaalamu mwenye fani hiyo ya uchumi.

Tutarudi tena wakati mwingine kumgusia kwa undani kidogo huyu The Late Edward Moringe Sokoine.
 
Mtoa hoja bado tunaomboleza msiba huu mpya, huo wa zamani tuuache kwanza - Mwendazake kaenda zake kwa ghafla sana jamani !!
 
Leo hii ni kumbukizi ya kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania na kipenzi cha watanzania mh Edward Moringe Sokoine kilichotokea 12.04.1984...
Wahujumu uchumi wa wakati huo hawamsahau huyu jamaa..japo ile vita ilingia dosari baada ya baadhi ya watu kuitumia kwa maslahi binafsi ya kukomoana na kulipa visasi
 
Wahujumu uchumi wa wakati huo hawamsahau huyu jamaa..japo ile vita ilingia dosari baada ya baadhi ya watu kuitumia kwa maslahi binafsi ya kukomoana na kulipa visasi
Tulishafikishwa hali mbaya sana.
Kula wali ilikuwa hadi utoke jasho kwa kuyakimbiza magari ya ugawaji
 
Mtoa hoja bado tunaomboleza msiba huu mpya, huo wa zamani tuuache kwanza - Mwendazake kaenda zake kwa ghafla sana jamani !!
Mkuu mimi kama mtanzania mzareeendo nina mkumbuka huyu mzee wetu Sokoine alivyokuwa anayashughulikia mateso yetu bila ya kujitangaza kupitia rtd wala uhuru na mzareendo kipindi kile.

Leo hii kiongozi analianzisha tatizo kwa wananchi alafu baadae anabeba TV, radio anakwenda kujifanya analitatua tatizo na kujiita kipenzi cha wananchi.
 
Leo hii ni kumbukizi ya kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania na kipenzi cha watanzania mh Edward Moringe Sokoine kilichotokea 12.04.1984.

Marehemu alipata ajali ya gari akiwa njiani kutokea Dodoma kuelekea Dar Es salaam ambapo alikuwa ameahirisha kikao cha bunge.

Watanzania tunazidi kumuombea pumziko la milele huko aliko.View attachment 1750133

Thu 12 April 1984​
Sokoine's Death
Thu 14 October 1999​
Nyerere's Death
Fri 24 July 2020​
Mkapa's Death
Wed 17 March 2021​
Magufuli's Death
 
Maduka ya RTC
Kipindi kile nilikuwa nakaa Mtoni tulikuwa tunahudumiwa na canter moja imeandikwa TUPA TUPA KUPATA KUNA MUNGU ya ugawaji hiyo.

Ukitaka kula wali kitumbo uwe tayari kulikimbiza gari likisimama dukani usimame foreni ili upate huduma.
 
Jina la Sokoine linanikumbusha jinsi Maisha yalivyokuwa magumu zama zile,tena ilikuwa mara baada ya Vita Vya Uganda, kisha ikaingia hali ngumu ya uchumi Tanzania.

Kila Kitu foleni. Inasemekana Kifo chake kilikuwa na Conspiracy huyu Jamaa.- Mabepari bwana! Ukiwafanyishia wataondoka naMtu.
Sijui Huyu Pombe naye kama si ntindo ule ule wa sokoine, maana naye kawanyoosha maBepari wengi na wafanya biashara.Kumteka mtu kama Mo si jambo la kitoto,The 2nd richest person in Afrika.

We acha tuu, Kuwa kiongozi katikanchi zetu hizi ni changamoto kubwa sna, lazima utazama pande zote ,chunga maisha yako, chunga maslahi ya Taifa na chunga maslahi ya Mabepari, utaishi kwa salama.
 
Kipindi kile nilikuwa nakaa Mtoni tulikuwa tunahudumiwa na canter moja imeandikwa TUPA TUPA KUPATA KUNA MUNGU ya ugawaji hiyo.

Ukitaka kula wali kitumbo uwe tayari kulikimbiza gari likisimama dukani usimame foreni ili upate huduma.
Tulikuwa tunaamka saa 12 kuwahi foleni
 
Jina la Sokoine linanikumbusha jinsi Maisha yalivyokuwa magumu zama zile,tena ilikuwa mara baada ya Vita Vya Uganda, kisha ikaingia hali ngumu ya uchumi Tanzania...
Hapo kwa Mo umechemka maana siyo the 2nd nadhani yupo nafasi ya 13 baada ya mwana south Afrika kushika nafasi ya 12
 
Back
Top Bottom