EE MORA TUNUSURU NA MPIKA BIRIANI

EE MORA TUNUSURU NA MPIKA BIRIANI

Mandesy

Senior Member
Joined
Mar 22, 2018
Posts
115
Reaction score
125
EE MORA TUNUSURU NA MPIKA BIRIANI

Malenga najikongoja, hadi juu ya jukwaa,

Nina ujumbe mmoja, ufike kwenye mitaa,

Ni ujumbe wenye haja, mantiki yameujaa

Ewe mola tunusuru, na mpika biriani,





Umeibuka mtindo, wa wadada wa mjini,

Akili zawekwa kando, zapelekwa matakoni,

Wanapenda lile tendo, la kuingiza uani,

Ewe mola tunusuru, na mpika biriani,



Wamejivika ujinga, kuwanasa wanaume,

Nyumba zao za kupanga, inayolipa midume,

Akili zao ni chenga, hii lazima niseme,

Ewe mola tunusuru, na mpika biriani,



Wanatingisha mitako, na huo ndio mtaji,

Hawaishi kwa vituko, wakitafuta mitaji,

Wanaipenda mitoko, ya unywaji na ulaji

Ewe mola tunusuru, na mpika biriani,



Amesambaza video, kuwatamanisha watu,

Hasa wale wenye vyeo, tena waume za watu,

Anabinua kinyeo, kilichoota mikutu,

Ewe mola tunusuru, na mpika biriani,



Anasema nyumba choo, asiletewe utani,

Kichwa chake kama choo, akili zi matakoni,

Kawateka mabishoo, kwenda kula biriani,

Ewe mola tunusuru, na mpika biriani,



Biriani ni kificho, cha wake uchangudoa,

Na hayo mapochopocho, anayojitangazia,

Anarembua mimacho, kwa vijana na washua,

Ewe mola tunusuru, na mpika biriani,



Mwili kaweka rehani, kila mtu haya twende,

Bora mkono kinywani, kugeuzwa kila pande,

Mwenyeji ama mgeni, akunjwa kama upinde,

Ewe mola tunusuru, na mpika biriani,



Mwisho..

Martius Rweyongeza, Nshamba Muleba
 
Mm sijawahi kula biriani ivi ni chakula gani icho?
 
Yako dua ina chongo, kwa Mpishi Biliani
Umejawa na kinyongo,kama jini kisirani
umehukumu kifyongo,pasipo fata kanuni
Waume wenda wenyewe,kwa mpishi Biriani

Lake tako ndio umbo, nawamejaa mitaani
Tena wamejaa tambo,siwapishi biliani
wanafanya majambo,hatarishi maskani
Waume wenda wenyewe,kwa mpishi biliani
 
Kazi nzuri Mkuu mwenye macho Asome! Hakika wewe Malenga!
 
Back
Top Bottom