EFD..A failure VAT collection Strategy

Inkoskaz

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Posts
6,361
Reaction score
2,378
Ili jambo lolote lifanikiwe baina ya pande mbili ni lazima liwe na ufahamu waq kutosha kwa pande zote mbili zinazohusika,Electronic Fiscal device(EFD) ni mradi wenye nia nia nzuri lakini haukukuwa na maandalizi mazuri hasa kumshirikisha mdau wa pili ambaye ni mlipa kodi.hakukuwa na elimu ya ufahamu na utumiaji wa kifaa hicho bali ni mradi ulioingia kiujumla bila kuangalia mapungufu hasa kwa mlipa kodi kwa baadhi ya maaeneo kama yafuatayo
1.Vifaa vile vinatumia umeme,havina option ya battery.hivyo kunapokosekana umeme ni tatizo na pia maeneo mengine hakuna umeme kabisa lakini biashara zinaendelea

2.Sehemu nyingi za biashara zinafikiua kilele siku za wikiendi hususani sehemu za starehe,sasa inapotokea malfunctioning kipindi hicho inakuwa vigumu kupata backup service kutoka kwa dealers ambao hawako available 24/7 na hivyo kusababisha usumbufu kwa wadau na hata wao TRA wakihitaji ukaguzi

3.Risiti za EFD hazionyeshi ni item gani imeuzwa bali huonyesha value tu...TATIZO!

4.Upatikanaji wa karatasi zake pia bado haujawa mzuri

5.Kuna watu wanasajili kampun na kusajili VRN then wananaunua machine wanaproduce risit kwa makampuni mengine yanafanya VAT input/Output returns hewa na hivyo serikali kupoteza mapato mengi

6.Mauzo mengine yanafanyika kwa credit terms hivyo hayawezi kuambatana na E-receipt kwa kuwa muuzaji hajapokea pesa ya mauzo lakini sheria inakinzana na hilo kwa kutaka every delivery iendane na e-receipt jambo ambalo ni gumu kwa wafanyabiashara wengi kwani sometimes inabidi delivery ikamilike ndio upate malipo lakini maafisa wa TRA hutaka ukitoa service iambatane na e-receipt wakati wewe hujapokea malipo..kwa maana ukitoa e-receipt unaconfirm kuwa umeshapokea malipo na rekodi zinawafikia TRA wakati si kweli
Nadhani kadhia ni nyingi lakini kama wadau mmeshaziexperience sio vibaya tukizishare hapa kwa faida zetu na hata maboresho kwa idara hii ya Kaizar
Matokeo yake kumekuwa na mkanganyiko na umejengeka uadui kati ya wafanyabiashara na idara hii kwani wao badala ya kuelimisha hukimbilia offence penalties ambazo mara nyingi huwa ni kubwa kuliko hata thamani ya biashara...nijuavyo mimi ili ng'ombe uweze kumkamua maziwa vizuri ni lazima umlishe majani mazuri,umpe maji na pia umpatie tiba kumuepusha na kupe nk
Nawakilisha!
 
Ni kweli mkuu hasa swala la credit note EFD haitambui negative tax so it's off system na ukiwauliza how to deal with credit note hamna majibu ya msingi
 
Lemgo kubwa ilikuwa kuuza machine ambalo hakikia limefanikiwa kwa 90%...... utasikia ''hilo tatizo tupo katika mchakato wa kulishighulikia ili kuondoa usumbufu uliojitokeza na kikosi kazi kimeshaundwa tayari''
 
Uko sahihi kabisa.

On top of that is this, unaongea na muuzaji akupunguzie bei anakubali bidhaa ya laki anakuuzia kwa
Tsh 90,000 au chini kidogo, kwa exchange ya risiti ya tsh.30,000/= tu! UNAKUBALI. Raha hiyo.
Si bidhaa haina jina. Yaani hakijulikani ni kitu gani kimenunuliwa kwa sababu hakuna tume ya bei
inayofuatilia, maadamu KODI ipo.
 
Tungelikuwa na tume ya bei, bidhaa zote zingekuwa na code ya aina moja na bei ya kufanana
na hivyo risiti zote zingeleta kodi ya ajna moja.

Ukiziangalia risiti hizo hata saa zinachekesha.

TRA ilitakiwa iufundishe umma juu ya UMUHIMU WA KODI, si kwa kupitia ktk redio tu bali
kwa matangazo ya kuzagaa kila mahali kama yafanyavyo makampuni ya simu.
 
Habari za jioni?

EFD imefanikiwa kwa kiwango kikubwa
Yaani sasahv kama hauna fischal receipt hauwezi lipwa pesa tofauti NA zamani
 
Ni kweli mkuu hasa swala la credit note EFD haitambui negative tax so it's off system na ukiwauliza how to deal with credit note hamna majibu ya msingi
hiyo factor ni very effective ukizingatia biashara za kibongo za kudeliver na kulipwa baada ya muda fulani
 
Lemgo kubwa ilikuwa kuuza machine ambalo hakikia limefanikiwa kwa 90%...... utasikia ''hilo tatizo tupo katika mchakato wa kulishighulikia ili kuondoa usumbufu uliojitokeza na kikosi kazi kimeshaundwa tayari''
Wao wana EXCUSE kibao lakini kama tatizo limemkuta mfanyabiashara kwa kweli ni vitisho,faini na rushwa ya waziwazi na bado watamuacha bila kumuelimisha asikosee tena siku za usoni
 
hapo ndio tunaita wamebugi step
 
Elimu kwa mlipa kodi kwa mapana ni ya muhimu,imagine wafanyabiashara wasomi au wanaoishi mijini wana uelewa lakini bado wanakumbana na matatizo kwa kutokufahamu baadhi ya vipengele vya sheria hii sasa je kwa mkulima wa pamba Bariadi ama mfugaji wa Longido inakuwa vp hapo
 
Habari za jioni?

EFD imefanikiwa kwa kiwango kikubwa
Yaani sasahv kama hauna fischal receipt hauwezi lipwa pesa tofauti NA zamani
Mkuu hakuna marefu yasiyo na ncha..mafanikio yapo lakini mapungufu ni mengi yanafunika na hayo unayoona mafanikio.na pia hapo umezungumzia upande mmoja, upande wa mlipwaji haujaujali hata kama kuna matatizo tuliyoyainisha hapo juu itatakiwa asilipwe which is not fair
 
Ila kwa upande mwingine ni kutokujua
Kwajinsi ninavyo fahamu efd za Bmtl zina option kabisa ya ku issue credit na kwenye z report yako itaonyesha kabisa kuwa umeuza elfu kumi by cash na elfu mbili by credit...Sasa hapo ndio mziki kutofautisha hizo credit na cash sales.
Mapungufu mengine ambayo mtu unaweza dhani ni tatizo ni mtumiaji mwenyewe watumiaji hawako serious wengi ni wakwepa kodi. Kwasababa mtu unapewa risiti mpaka uombe ilo ni tatizo
 
Ni kweli mkuu hasa swala la credit note EFD haitambui negative tax so it's off system na ukiwauliza how to deal with credit note hamna majibu ya msingi

hapo ndio tatizo, uki credit, EFD hai-cancel that transaction, wakati wa kufanya vat reconciliation na kuandaa report kwa ajili ya malipo tra inaleta taabu. Kila mwez nagombana na ma-auditor wa TRA wenyewe wanasema tunawaibia. Kwa vile EFD machine haitambui credit note na sisi tusi credit hata kama kunamakosa wakati wa ku issue invoice.
 
Hapo ndio maana kamili ya hizo mashine kosa likifanyika ukaelezee kama kweli ni kosa au la
 
Bei ya hizo machine ambayo hulipwa kwa kodi yetu mbona haiongelewi, bei ya EFD ni kubwa mno ukilinganisha na bei ya vifaa vingine vinavyofanya kazi kama EFD, wakati POS terminal zitumiwazo na mabenk huuzwa kwa USD 100-250, EFD huuzwa kati ya usd 1000 hadi 2500 KUNA NINI HAPO ?
 
Wao wana EXCUSE kibao lakini kama tatizo limemkuta mfanyabiashara kwa kweli ni vitisho,faini na rushwa ya waziwazi na bado watamuacha bila kumuelimisha asikosee tena siku za usoni

ni kweli kabisa hizi mashine zimeongeza wigo wa rushwa kwa watu wa TRA, nimeshuhudia kwa macho yangu mbele ya watu ndani ya ofisi ya TRA wanachukua rushwa "kukusaidia" usilipe faini ya 3mn ! nilionavyo hili zoezi ni kuwa, TRA watahakikisha mambo mengi wananchi hawajui ili waboreshe wigo wa rushwa hali kadhalika wananchi nao watajitahidi kujua mbinu za kuishi nazo hizo mashine kwa "manufaa". Hivyo mwishowe itakuwa ni mradi ulioshindwa, kwani hamna mtu au kikundi ambacho kina haja ya kufanya marekebisho !
 

Ndo maana hii biashara imejaa wahindi !
 
Mimi na kabiashara changu cha consultancy nimeanza kutumia EFD mwezi July. Unampelekea mteja ESD invoice , TRA wao wanaona figure za pesa tuu as if umelipwa, kumbe mteja hajalipa mpaka leo!. Nafanya return mwezi wa 9 Kitaeleweka tuu!.

Hizo fiscal devices zetu ni za obsolate technology hazionyeshi
1. Mteja ni nani?
2. Hazionyeshi ni bidhaa gani?.
3. Hazionyeshi type of curency zaidi ya
TZS !.
4. Hazionyeshi kama umelipwa au la!.
5. Hazionyeshi credit note wala any
discount!.
6. Ni mimashine ya ajabu kabisa yanayota computer system ya windows tuu, sisi
watu wa os tunaotumia mac
tunalazimika kuweka li pc la window kwa vile TRA wao fiscal software
yao wao ni windows only!.

7. Wale wenye kufanya international
regional transactions kwa nchi za EAC
ndio kabisa, systems zetu don't speak the same language, huku kwetu TRA
wakitumia Ayscuda++, wenzetu Kenya
na Uganda wao wanatumia Simba na
ukijumlisha Rwanda na Burundi only
only God knows what!, tutegemee nini
kwenye regional intergration?.
tambua

Ukishatuma tuu invoice, mashine inatuma Z-report TRA kuwa nimelipwa, in actual fact bado sijalipwa mpaka kesho!.
 
Yaani wanajitahifi wadau wawe kizani wawakamue
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…