Shadida Salum
Journalist at JamiiForums
- Sep 11, 2020
- 69
- 105
Spurs amefanikiwa kutinga fainali baada ya kuiadhibu Brentford kichapo cha bao 2-0 katika mchezo uliochezwa katika Dimba la Tottenham Hotspurs siku ya tarehe 5 Januari 2021.
Huku City akiingia kwenye fainali hiyo baada ya kuitandika Manchester United goli 2-0 kwenye mchezo wa nusu fainali uliopigwa tarehe 6 Januari 2021 ambapo Man United alikua nyumbani katika Dimba la Old Trafford.
Man City anaingia kwenye fainali za michuano hiyo kwa mara ya nne mfululizo huku akiwa amechukua ubingwa katika awamu zote tatu nyuma yani kuanzia 2018 mpaka 2020.
Awali fainali hizo zilipangwa kufanyika Februari 28, 2021 na baadaye kusogezwa mbele mpaka Aprili 25, 2021.
Maamuzi ya kupeleka mbele mchezo huo yamekuja kwa matarajio ya kuwa huwenda mpaka kufika Aprili mashabiki wanaweza kuruhusiwa kuingia uwanjani.