EFM yamburuza Paul James mahakamani kwa kuvunja mkataba, yadai fidia ya shilingi milioni 200

chinchilla coat

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2016
Posts
5,107
Reaction score
10,969


Mtangazaji wa Clouds FM, Paul James aka PJ ameshtakiwa mahakamani na kituo cha redio cha EFM kwa kuvunja mkataba kinyemela
Mtangazaji huyo aliondoka EFM mwanzoni mwa mwezi huu na kurejea kwenye kituo chake cha zamani, Clouds FM, alichoondoka pamoja na mwenzake Gerald Hando. EFM imefungua mashtaka katika mahakama ya kazi jijini Dar es Salaam kwa madai ya kukiuka mkataba wa kazi wa kituo hicho.

Kufuatia mashtaka hayo, EFM inadai fidia ya shilingi milioni 200 kutoka kwa mtangazaji huyo.
Inadai PJ alikatisha mkataba kiholela na kurudi tena Clouds FM bila kufuata makubaliano pamoja na sheria alizokubaliana nazo katika mkataba wake pale alipojiunga nacho.

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa November 23, 2016 katika mahakama ya kazi jijini Dar es Salaam.

Chanzo: Bongo5
 
Nachojua PJ ni msomi .....ilikuwaje akashindwa kutambua masharti ya mkataba wake wa awali akiwa E-FM.....!? Hili ni funzo kwa waajiliwa wengine.....maana 200M kwa wakati huu si mchezo......
 
Sijui nini kinawapata watangazaji wetu? hivi kweli Pj alikuwa hafahamu kuwa kuvunja mkataba kuna taratibu zake kweli? nimesikitika sana kama kweli mtangazaji ana kurupuka tuu bila kuangalia au kusoma vipengele vya mikataba yake na mwajiri wake.

Pengine aliona kuna kipengele kinacho mruhusu kuvunja mkataba nakufanya hivyo...pengine.
Ni kweli Clouds hawakujua hilo?
Hata hivyo madai yamepelekwa kwa baraza la usuluhishi na si mahakamani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…