EFM yamburuza Paul James mahakamani kwa kuvunja mkataba, yadai fidia ya shilingi milioni 200

EFM yamburuza Paul James mahakamani kwa kuvunja mkataba, yadai fidia ya shilingi milioni 200

xPicha-ya-PJ.jpg.pagespeed.ic.i_hS0nz1KE.jpg
xEFM-Radio-page-001.jpg.pagespeed.ic.eWxUeiF9FO.jpg


Mtangazaji wa Clouds FM, Paul James aka PJ ameshtakiwa mahakamani na kituo cha redio cha EFM kwa kuvunja mkataba kinyemela
Mtangazaji huyo aliondoka EFM mwanzoni mwa mwezi huu na kurejea kwenye kituo chake cha zamani, Clouds FM, alichoondoka pamoja na mwenzake Gerald Hando. EFM imefungua mashtaka katika mahakama ya kazi jijini Dar es Salaam kwa madai ya kukiuka mkataba wa kazi wa kituo hicho.

Kufuatia mashtaka hayo, EFM inadai fidia ya shilingi milioni 200 kutoka kwa mtangazaji huyo.
Inadai PJ alikatisha mkataba kiholela na kurudi tena Clouds FM bila kufuata makubaliano pamoja na sheria alizokubaliana nazo katika mkataba wake pale alipojiunga nacho.

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa November 23, 2016 katika mahakama ya kazi jijini Dar es Salaam.

Chanzo: Bongo5

Kabla tu ya kuanza kudaiwa hiyo Hela Jamaa ' kakondeana ' hivyo na sasa hivi ndiyo anatakiwa alipe hiyo Tsh 200,000,000/ je Jamaa ( PJ ) hawezi ' kukondeana ' zaidi na kuwa kama fido dido kwa kuwa na ' mawazo ' ya jinsi ya kuilipa hiyo Hela ya Efm?
 
Kiukweli PJ amejipotezea uweledi kama BWANA YULE Le Propesa,Heshima yake imeshuka kabisa,Efm wekeni kwanza court injuction asitangaze kwanza hapo Clouds FM mpaka kesi ya msingi iishe,na iwe fundisho kusoma terms and condition mnapoajiriwa,Sehemu nyingine wana declare kwamba ukiacha kazi sehemu moja hautakiwi kwenda kwa competitor(Doing Same Bizness) wao mpaka mwaka mmoja upite na si direct.
 
Sijui nini kinawapata watangazaji wetu? hivi kweli Pj alikuwa hafahamu kuwa kuvunja mkataba kuna taratibu zake kweli? nimesikitika sana kama kweli mtangazaji ana kurupuka tuu bila kuangalia au kusoma vipengele vya mikataba yake na mwajiri wake.

Pengine aliona kuna kipengele kinacho mruhusu kuvunja mkataba nakufanya hivyo...pengine.
Ni kweli Clouds hawakujua hilo?
Hata hivyo madai yamepelekwa kwa baraza la usuluhishi na si mahakamani.
wanachukulia ushikaji kwenye kila kitu hawa watangazaji wa hapa DAR...!!

ngoja kwanza efm waoneshe mfano...
 
Msanii wetu yule hajashiriki fiesta kwakuwa inadhaminiwa na tigo wakati ye ni balozi wakudumu wa Voda watu wakamnanga na kumuona hajielewi,
Kama ni kweli basi PJ kafanya mambo ya hali ya chini sana, okay sheria ifuate mkondo wake.
 
Afu nyie wanasheria wa sikuhizi mkoje??kwanini amtunzi siri za clients kwenu.!?

Hiyo ni summons , una uhakika gani ni wanasheria ? labda mwenyewe aliipiga picha baada kuipokea
 
Sijui nini kinawapata watangazaji wetu? hivi kweli Pj alikuwa hafahamu kuwa kuvunja mkataba kuna taratibu zake kweli? nimesikitika sana kama kweli mtangazaji ana kurupuka tuu bila kuangalia au kusoma vipengele vya mikataba yake na mwajiri wake.

Pengine aliona kuna kipengele kinacho mruhusu kuvunja mkataba nakufanya hivyo...pengine.
Ni kweli Clouds hawakujua hilo?
Hata hivyo madai yamepelekwa kwa baraza la usuluhishi na si mahakamani.
Sijui PJ hafahamu taratibu za kuvunja mkataba au ni jeuri ya mwajiri mpya ya kwamba anaweza kufanya atavyo kwa kuwa yuko juu ya sheria, au walifikiri E FM wataiogopa Clouds kwa wako karibu na mamlaka kuu. Ni kitu cha ajabu na wala hakiingii akilini mbona mwenzake Mzee wa Jahazi alizingatia taratibu zote za kuacha kazi na kuhamia Clouds
 
Alitakiwa atoe notification ya mwezi au alipe mshahara wa mwezi nadhani mikataba mingi ipo hivi..
 
Mmmh hapo ndo mahala pake huju jamaa alizimgua sana tena sana

Awalipe tu maana hakuna namna
 
Back
Top Bottom