EFM yamburuza Paul James mahakamani kwa kuvunja mkataba, yadai fidia ya shilingi milioni 200

Mzee wa jahazi anajielewa kwa mbali .PJ mzee wa pombe Kali bila kuonja asubuhi atangazi
 
Mimi.naungana na wewe, Mitanzania.sijuhi ikoje, hasa hilo jinga la kuitwa Bikira wa Kisukuma, Mishipa imemsimama utafikiri ana share E-fm. Hii case ndo kwanza imeitwa kwa hearing. Bado haijajulikana nini kilichopo kwenye Mkataba. Sheria za Kazi zipo wazi kabisa. Nini unatakiwa kufanya unapoamua ku resign Kazi. Labda kama mshahara wake ulikua ndo huo Mil. 200 lakini kama ni hii mishahara ya Kibongo unaacha kazi kwa notisi. Tusiwe mbumbumbu wa sheria. Hao E-fm wanatafuta Kiki tu nao, Huyo Bikra kapost Ujinga Juzi kuhusu Coverage ya Radio yao. Halafu watu wakamuumbua.
 
Gadner alikaa pale miaka 2 kulinda mkataba uyo pj akae mwezi tu auvuruge si atakua kichaa
 
Afu nyie wanasheria wa sikuhizi mkoje??kwanini amtunzi siri za clients kwenu.!?
Hili swala linanishangaza sana mkuu. Privacy ya clients is at stake. Na sidhani kama tatizo ni new generation of lawyers, kuna senior counsels wanafanya haya mambo hadi aibu mkuu
 
Hakuna utaratibu wa kumlazimisha mfanyakazi kiivyo.Mkataba wa kazi upo direct
Mkubwa Pitia Pitia mikataba ya kazi utaiona hayo makitu,Kuna training za kazi unapelekwa nje ya nchi kuna hela unalipiwa ila ukikubali inabidi uifanyie kampuni chini ya miaka kadhaa kisha unaweza kuondoka ila ukiacha chini ya miaka miwili inabidi uilipe.
 
Sijahukumu labda kama umeshindwa kunielewa kama sheria hizo amefata na taratibu za kuacha kazi sidhani kama E-fm wange kwenda kulalamika... maana hizo sheria ziko wazi na sidhani kama kuna upande haufahamu hayo labda kama kuna upande umekosea kutafsiri vizuri huo mkataba...
Mimi ambacho ninashangaa ni inawezekanaje pj kufanya hivyo? time tells ..
Lakini kwa swala la million 200 hata kama E-fM Watashinda lakini mahakama haitokubali fidia ya million 200
 
Reactions: bdo
[emoji121]
HIZI MEDIA STATIONS NAZO ZINA UKASUKU MKUBWA SANA WA KUNG'ANG'ANIA WATU AMBAO KIMSINGI UWEZO WAO NI WA KAWAIDA SANA,

KWA NINI WASITUPE PLATFORM SISI-
TUPO TU HUKU MTAANI TUNA VIPAJI NA TAALUMA ILA TUKIENDA KUOMBA CHANCE WANATUBANIA??
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]. Hata wangesema mil. 10 tu sidhani kama anayo
 
Hapo awatamuweza kwa sababu alikuwa kwenye probation period ya miezi 6
 
Nimeshangaa mleta mada na huyo mwandishi wanaposema mahakama ya kazi wakati document waliyoambatanisha ni ya Tume ya usuruhishi.
 
Efm wastaarabu sana wamempeleka kwenye baraza la usuruhishi kwanza na si mahakamani.
 
Na walioandika Taarifa hii wameshindwa kutafsiri kwamba hiyo ni Tume na si mahakama ya kazi?
 
Ni Mara chache sana ukakuta mwajiri anashinda kesi pale CMA! Efm wasahau hizo 200m!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…