Egypt imepinga vikali makubaliano ya usimamizi wa Mto Nile

Hiyo jeuri anayo Ethiopia tu. Nchi nyingine zilizobakia (ikiwemo hii ya kwako) ni 🚮 tu kwa Misri.
 
Tupigane tu Mto ni mali ya Tanzania, hata hivyo kumepoa sana.
Comrade! Nchi yako haina uwezo wa kupigana na Misri! Na huu ndiyo ukweli mchungu. Achilia mbali kuipinga/kuidindishia! Na ndiyo maana mpaka leo eneo la nchi yetu (ikiwemo Kandavya Ziwa) hakuna maji ya uhakika kwa ajili matumizi ya nyumbani na kilimo! Na wakati huo tuna Ziwa kubwa kama Victoria!

Huku Misri wakiyachezea tu hayo maji yatokanayo na hilo Ziwa, vile wapendavyo! Tena wakifanya hivyo kwa kutumia sheria zilizosainiwa wakati wa Mkoloni.
 
Kwa taarifa yako Ziwa Victoria ni moja ya chanzo cha Mto Nile kwa hiyo Egypt haitaki matumizi yo yote ya maji bila wao kutaarifiwa na kukubali vinginevyo wako tayari kutumia nguvu za kijeshi.
 
Kwa taarifa yako Ziwa Victoria ni moja ya chanzo cha Mto Nile kwa hiyo Egypt haitaki matumizi yo yote ya maji bila wao kutaarifiwa na kukubali vinginevyo wako tayari kutumia nguvu za kijeshi.
Niliona makala moja ikionesha chanzo cha Nile pale Uganda, kuna ushahidi wowote usio na shaka kuwa Ziwa ndio chanzo cha mto?

Ziwa lipo Misri? Mkataba wa Muingereza sio msahafu kuwa eti watu wasinufaike na maji kisa kuna watu watakufa kiu! Si waarabu wale, Dubai wanapata wapi maji?
 
Kukuelimisha wewe kunahitaji nguvu ya ziada! Mto wo wote ule mkubwa ni mkusanyiko wa vijito vingi vidogo, kwa hiyo Mto Nile vilevile ni mkusanyiko wa mito mingi. Hivyo mito inayofanya Mto Nile kuwepo inaanzia Burundi, Rwanda, Kenya na Tanzania mfano mito ya Rusumo, Kagera, Mara, Simiyu nk ambayo huingia Ziwa Victoria. Kutoka Ziwa Victoria Mto Nile huanzia eneo la Jinja na kuendelea kwenda Kaskazini ambako mito mingine huingia kutoka Uganda, Sudan Kusini, DRC, Ethiopia, Elitrea na Sudan hadi Egypt.

Kwa hiyo nchi zote hizo nilizozitaja ni wadau wa Mto Nile na zinapaswa kukubaliana namna bora ya matumizi ya maji yake.

Umeelewa?
 
Egypt alipewa kichwa na Britain, lakini kimsingi kila mtu anapaswa kuutumia mto kwa nafasi yake. Kabla ya ukoloni kulikuwa hakuna makubaliano yoyote ya matumizi, kila mtu kwa nafasi yake. Yani sisi tuteseke na maji kisa jitu lipo mbali huko tena mwarabu?
 
Ndiyo sababu watu wa Mbarali wanateseka ili bwawa la Mtera lijae maji ya Mto Ruaha kuzalisha umeme na wewe ufaidi kuutumia!

Watu wa Mbarali wakitumia maji kwa nafasi yao wewe utapiga kelele ya kukosa umeme!
 
Ndiyo sababu watu wa Mbarali wanateseka ili bwawa la Mtera lijae maji ya Mto Ruaha kuzalisha umeme na wewe ufaidi kuutumia!

Watu wa Mbarali wakitumia maji kwa nafasi yao wewe utapiga kelele ya kukosa umeme!
Hao wa mbarali ni wananchi wenzangu na sisi wote tunafaidika. Inaeleweka, hao waarabu wa Misri ni nchi nyingine na hawana msaada kwangu.
 
Hao wa mbarali ni wananchi wenzangu na sisi wote tunafaidika. Inaeleweka, hao waarabu wa Misri ni nchi nyingine na hawana msaada kwangu.
Mungu alivyoumba Dunia hakuangalia mipaka ya nchi! Mipaka imewekwa na binadamu, na binadamu wameanzisha Jumuiya mbalimbali kwa ajili ya kuondoa mitafaruku. Ni kwa sababu hiyo hiyo Tanzania imejiunga katika Jumuiya ya watumiaji wa Mto Nile ili ishirikiane na nchi zingine katika kunufaika na matumizi ya maji ya mto huo!

Kwa hiyo kwa kuwa Tanzania ni member wa Jumuiya ya Mto Nile inawajibika kuheshimu makubaliano yo yote.
 
Jumuiya za kikoloni. Kabla kila mtu alikuwa anatumia kwa muda wake na nafasi yake. Ukoloni wa mwingereza ndio ulisababisha yote haya. Alafu wewe kama ni mtanzania, unatete Misri.
 
For years Egypt wamekua wakitupangia Nini tufanye na Nini tusifanye kwenye ziwa Victoria ambacho ndio chanzo Cha Nile river.

Nukuu ya baba wa taifa.
""UTII UKIZIDI SANAA HUZAA UOGA, UOGA UKIZIDI SANA HUZAA UNAFIKI NA KUJIPENDEKEZA NA MWISHO WAKE NI MAUTI""
 
True! Hali ya tabia ya hali ya hewa lazima izingatiwe ili athari iwe kwa wote na siyo Misri wajione ni tofauti!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…