Eid Al Adh haa ( Eid An Nahri pia Eid Al hajj )1446 Hijriyyah / 2025 Miylaadiyyah

Chifu mkuu

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2025
Posts
857
Reaction score
926
Nakusalimuni nyote.

Kulingana na tarehe itokanayo na mwandamo wa mwezi wa kimataifa Eid Al Adh haa kwa mwaka huu wa 1446 Hijriyyah sawa na 2025 Miylaadiyyah itakuwa siku ya ijumaa ya tarehe 10 Dhul hijja ( mfungo tatu ) mwaka 1446 sawa na tarehe 6 June mwaka 2025 Miylaadiyyah.

Tukio la sikukuu ya Eid ya kuchinja ( Eid Al Adh haa au Eid An Nahri au pia Eid Al Hajj) litatanguliwa na tukio la waislamu waliopo katika ibada ya hijja kusimama katika viwanja vya Arafat siku ya alkhamisi tarehe 9 Dhul hijja sawa na tarehe 5 June huko Makka nchini Saudi Arabia.

Katika siku hiyo ambayo mahujjaaji watasimama Arafat nchini Saudi Arabia waislamu wote duniani watawaunga mkono mahujaji kwa kufunga funga ya Sunna inayojulikana kama swaumu au funga ya arafa.
Katika hadithi iliyopokelewa na imamu Muslim kutoka kwa swahaba Abuu Qatada Al Answaary ni kwamba mtume صلى الله عليه وآله وسلم aliulizwa kuhusu funga ya siku ya arafa akasema:
" Inafuta madhambi ya mwaka uliopita na mwaka ujao".

Ni jambo jema na muhimu sana waislamu kukithirisha matendo mema katika siku kumi zote za mwanzo wa mwezi wa Dhul hijja ikiwa pamoja na kuswali swala za Sunna, kutoa swadaka, kusoma Quran, kuamrisha mema na kukataza mabaya.

Baadhi ya wanachuoni wanaona kuwa inafaa pia kufunga siku tisa zote za mwanzo zinazoitangulia siku ya Eid ya kuchinja kutokana na hadithi ya mtume
صلى الله عليه وآله وسلم aliposema katika hadithi ya Imamu Bukhari toka kwa swahaba Ibnu Abbaas ya kwamba:
"Hakuna masiku ambayo matendo mema yanapendwa zaidi kwa Allaah kuliko haya masiku kumi. Wakasema , "ewe mjumbe wa Allaah , hata jihadi katika njia ya Allaah?!" Akasema mtume صلى الله عليه وآله وسلم " hata jihadi katika njia ya Allaah, isipokuwa mtu aliyetoka ( kwenda jihadi ) kwa nafasi yake na mali yake na ikawa hakikurudi chochote".

Hadithi hii inatuhimiza kuongeza bidii katika ibada za faradhi na sunna katika haya masiku kumi ya mwanzo ya mwezi wa Dhul hijja ( mfungo tatu ).

Pia katika mambo ya kuzingatia ni kwamba kwa mtu mwenye nia ya kuchinja siku ya Eid haitakiwi kukata kucha wala nywele za aina yoyote wala kupunguza chochote katika mwili wake kv kutahiri hadi atakapomaliza kuchinja.

Hili limekatazwa katika hadithi ya mtume صلى الله عليه وآله وسلم Iliyopokewa na Imamu Muslim kutoka kwa mke wa Mtume Ummu Salama anasema kuwa mtume صلى الله عليه وسلم amesema:

" Yakiingia masiku kumi ( ya mwanzo wa Dhul hijja) na mmoja wenu akataka kuchinja basi asiondoe chochote katika nywele zake wala mwili wake mpaka atakapochinja"

Katika mambo ya kuzingatia ni kwamba kuchinja kunakozingatiwa siku ya Eid ni kwamba.
1️⃣ Yatakiwa mtu achinje baada ya kuwa ameishaswali swala ya Eid.
Akichinja kabla ya swala ya Eid haizingatiwi kuwa kafanya ibada ya kuchinja siku ya Eid.

2️⃣ Mnyama anayechinjwa ya takiwa awe ni mmoja wa wanyama aina nne wafugwao:
Ngamia, Ng'ombe, Kondoo na mbuzi.
Farasi na ndege kama bata na kuku hawazingatiwi katika ibada ya kuchinja siku ya Eid.

3️⃣ Mnyama anayechinjwa yatakiwa awe na afya kamili na asiwe ugonjwa wala ulemavu wa aina yoyote kama upofu, ulemavu katika miguu yake nk.

Mwisho kabisa ni Sunna kupiga takbira kwa sauti kila baada ya swala ya faradhi kuanzia alfajiri ya siku ya arafa ( tarehe 9 ) na siku ya Eid hadi alasiri ya mwisho wa masiku ya kubanika nyama. ( Tarehe 13 )

Nakutakieni maandalizi mema ya funga ya arafa siku ya alkhamisi na sherehe za Eid Al Adh haa siku ya ijumaa.

Tamati.
 
Katika uislam hakuna mwezi wa kimataifa.
Kuna mwezi gani Maallim.
Mimi ninavyojua Allaah aliumba jua Moja na mwezi mmoja.
Halafu akatuchagulia mtume mmoja ( Muhammad bin Abdillaah ) na kutuelekeza tuelekee kibla kimoja
( Makka kwenye Kaaba tukufu ) Na Mimi ninaposema mwezi wa kimataifa namaanisha mwezi wa dunia nzima kwakuwa mwezi ni mmoja na ndio unaotoa Nuru Dunia nzima.
 
Hakika

Swali langu

Katika fungu twa ruhusiwa kufungua swaumu baada ya 🇨🇳 china kuingia magharib mwezi si mmoja.?
 
Kama
Hakika

Swali langu

Katika fungu twa ruhusiwa kufungua swaumu baada ya 🇨🇳 china kuingia magharib mwezi si mmoja.?
Kama una elimu ya sekondari kasome jiographia kidato cha kwanza na pili, hapo utaelewa kila kitu wameeleza vizuri sana kuhusiana na mzunguko wa dunia , mwezi na utofauti wa kimasaa
 
Kama

Kama una elimu ya sekondari kasome jiographia kidato cha kwanza na pili, hapo utaelewa kila kitu wameeleza vizuri sana kuhusiana na mzunguko wa dunia , mwezi na utofauti wa kimasaa
Wewe ni muislam mwenzangu si wezi kukujib kwa kejeli wala dharau

Umesema mwezi ni mmoja ulikuwa na maana gani
 
Bakwata wametoa taarifa kuwa wanaswali tarehe 7 wewe unatwambia tarehe 5 aacha uongo wako bhana
Umejitahidi Kusoma,, Kuelewa,,Kufahamu Na Kutambua Aliyo Andika Mleta Mada Katika Andiko Lake??Kwa Nia Njema Embu Kasome Tena Kwa Utulivu,,Uelewa,,Utambuzi Na Ufahamu,,Naamini Unaweza Ukaja Na Maoni,,Ufahamu Na Mtazamo Tofauti Na Huo Uliojaaliwa Andika......
 
Hakika

Swali langu

Katika fungu twa ruhusiwa kufungua swaumu baada ya 🇨🇳 china kuingia magharib mwezi si mmoja.?
Mbona umeenda china mbali?!
Dar es salaam na Kigoma wanafungua nyakati tafauti!.
Wakati watu wa Dar, Tanga na Zanzibar wanafuturu Kagera na Kigoma bado jua linawaka je Kigoma na Dar miezi pia ni tafauti?!
Yawezekana hata hii Tanzania huijui.
Kama una ndugu , jamaa au rafiki huko Kigoma ukisikia adhana ya Magharibi ukiwa Dar mpigie simu muulize vipi huko Kigoma au Kagera jua limeishazama.
Huu ni utafiti ambao nimefanya mwenyewe .
Nikiwa wilayani Ngara mkoani Kagera kama saa 12 na nusu hivi jua bado linawaka nikampigia simu mke wangu ambaye alikuwa Tanga akaniambia wao wanamalizia futari na magharibi wameishaswali muda mrefu.
 
Wewe ni muislam mwenzangu si wezi kukujib kwa kejeli wala dharau

Umesema mwezi ni mmoja ulikuwa na maana gani
Kaka usipaniki kasome uelewe mzunguko wa mwezi kuizunguka dunia ukoje , tunaposema mfano afrika ya mashariki wanachukulia majira kwenye nyuzi 45,! je saudia wanachukulia nyuzi ngap? Je pasingekuwepo na tekinoljia kama simu, radio, TV na vyombo vingine vya kupashana habar mwezi ukiandama Zanzibar muumini wa kigoma angepataje habari kama kigoma hajaonekana ! Kwann ukiambiwa umeandama saudia kupitia hizi media unakataa !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…