Game Theory
JF-Expert Member
- Sep 5, 2006
- 8,546
- 855
Eid Mubarak kwa wote. Hapa Tz natumaini itakuwa jumatano.
Nachukua afasi hii kuwapongeza waisilamu kwa kukamilisha mfungo mtukufu wa Ramadhani na pia kuwatakia heri ya sikukuu wana-JF wote.
Kule Nigeria wamesali leo, Saudia na UAE wametangaza idi ni kesho na nchi nyingine zilizobaki duniani itakuwa Jumatano.
Nawatakia sikukuu njema ndugu zetu wa Ansar Sunna!
........nilitamini kweli hii sikukuu ianze alhamisi ili tuwe na long weekend tupumzike kwa siku nne zingetosha kabisa kwenda kutembelea ndugu na jamaa sehemu za mbali kidogo ..
all in all sikukuu njema watanzania zangu
GAME THEORY,
..Sheikh Zayed kwanini hawajengei Waislamu wa Tanzania hata hospitali moja ya rufaa?
..EID NJEMA KWA WATANZANIA WOTE.
Masatu,
..Uislamu upo Tanzania toka zama hizooo.
..Sheikh Zayed aliyejenga msikiti mkubwa na wa anasa kiasi hicho, wakati wa uhai wake, kabla hajafariki 2004, amefanya nini kwa Waislamu wenzake wa Tanzania?
..hizi nchi za kiarabu/Kiislamu ni matajiri sana. it is about time tuanze kuwashika mashati wasaidie wenzao wa Tanzania.
..wengesaidia kujenga bonge la hospitali la rufaa bongo, kila m-Tanzania angefaidika.
..EID NJEMA KWA WATANZANIA WOTE.