Ejaculation Problems: Too Fast, Too Slow or Not at All? [Kuwahi au kuchelewa kumwaga]


Pole sana Chief Engineer,

Tatizo lako kitaalam linajulikana kama “premature ejaculation” au kufika kileleni mapema au kwa lugha ya mtaani ‘kukojoa upesi’. Ni hali ambayo inampata mwanamme ambapo hutoa shahawa kabla ya kuanza tendo la ndoa au muda mfupi tu baada ya kuanza tendo bila yeye mwenyewe kukusudia. Kwa kawaida mtu mwenye tatizo hili hutoa mbegu zake za kiume hata baada ya maandalizi kidogo sana. #Unaweza kugoogle na ukapata taarifa zaidi.

Tatizo hili hujidhihirisha zaidi kwa vijana wenye umri mdogo na hupungua kadri umri wa mtu unavyoongezeka. Karibu kila mwanamme kwa wakati fulani hupata tatizo hili lakini baadhi ya wanaume wenye umri wa kati huwa na tatizo la kudumu.

Chanzo kamili cha tatizo hili bado hakijafahamika. Lakini imethibika kwamba wasiwasi au mishipa ya fahamu inahusika sana na tatizo hili. Hali hii inaweza kutokea unapompata mpenzi mpya au unapofanya tendo hili baada ya muda mrefu kupita toka ulipotoa shahawa mara ya mwisho. Hii ndiyo sababu iliyofanya baadhi ya wanaume kugundua kuwa wakinywa pombe kidogo, huwapunguzia wasiwasi na huwasaidia wachelewe kufika kileleni. Mara nyingine tatizo hili linatokana na matatizo katika mfumo wa homoni za mtu au likiwa ni matokeo ya matumizi baadhi ya madawa.

Kwa kawaida tatizo la kuwahi kufika kileleni mapema ni tatizo ambalo huondoka lenyewe kadri umri unavyokuwa unasogea mbele. Kama tatizo sio kubwa sana, kwa mfano, kama unamudu kuendelea na tendo la ndoa kwa dakika tano na ungependa kufikisha dakika kumi, wewe sio mtu wa kumwona daktari bali mtu ambaye unaweza kufanya mazoezi fulani ya kuongeza muda wako. Vitu rahisi vya kufanya ni kutokuwa na papara, kutulia na kondoa mawazo yako kutoka kwenye tendo na kuyapeleka mbali kwenye jambo jingine tofauti kabisa unapokaribia kufika kileleni. Unaweza kufanya utafiti na mpenzi wako mkapata mtindo (sexual position) ambao utakusaidia usifike kileleni mapema. Kama hali yako ni mbaya zaidi, unaweza kutumia njia zifuatazo:

1. Kufanya mazoezi yanayosaidia kuondoa tatizo la kuwahi kufika kileleni. Hapa chini ni orodha ya baadhi ya mazoezi unayoweza kufanya;

-Kuvuta Na Kutoa Pumzi (Deep Breathing)
-Kuanza Na Kukatisha (The Stop-and-Start Method)
-Kuminya (The Squeeze Method)
-Mazoezi Ya Kegel (Kegel Exercises)
-Mazoezi Ya Tantra (Tantric Techniques)

Mazoezi ya Kegel yana umuhimu wa kipekee kutokana na ubora wake katika kuondoa tatizo la kukojoa upesi (siyajui sawasawa, ngoja waje kina Mzizi Mkavu wanaweza kukusaidia zaidi).

2. Kutumia kondomu maalumu (Condoms With Benzocaine). Kondomu hizi hukusaidia uendelee na tendo la ndoa na kuongeza muda wako wa kufika kileleni kwa kiwango cha hadi dakika tano. Kondomu hizi huwekwa benzocaine ambayo hutia ganzi kwa kiwango kidogo sehemu ya kichwa ya uume ili kupunguza usikivu wa nyege (sexual sensation) na kumfanya mwanamme aweze kutawala muda wake wa kufika kileleni.

3. Kutumia dawa zilizotengenezwa mahsusi kwa tatizo hili (Antidepressant medicines). Dawa ambazo zimekuwa zikitumika ni pamoja na Vig Power, Clomipramine (Anafranil) na Dapoxetine (Priligy). Tramadol (Ultram), dawa ambayo hutumika kuondoa maumivu, hutumika pia kuondoa tatizo hili.

Kuna creams, gels na sprays ambazo zimetengenezwa kupambana na tatizo la kukojoa haraka. Hizi hufanya kazi kwa kupunguza usikivu wa nyege kwenye dhakari. Mfano wa dawa hizi ni lidocaine au lidocaine-prilocaine ambayo hupakwa kwenye uume kabla ya kuanza kujamiiana…
 
umekuwa kama kuku tu mkuu,upo dar nini?
 
maelezo mazuri, naomba niulize hizi dawa ulizoelezea point mamba 3 na hyo kondom maalumu WAP znapatikana?
 
maelezo mazuri, naomba niulize hizi dawa ulizoelezea point mamba 3 na hyo kondom maalumu WAP znapatikana?

Kabla hujazitafuta hizo dawa na kuzitumia, kwanza muone mtaalam wa tiba ili ambaye atajua ni aina gani ya dawa inakufaa, na kwa dozi gani...
 


Chief check me through 0715476787, hakila utalisahau tatzo hili Na utafurahia kuwa Na mpenzi wako
 
Habari wadau,

Mimi nikijana mwenye umri kati ya miaka 24, hivi tatizo linalonisumbua ni kwamba kila ninapokutana kimwili na msichana huwa nachelewa sana kupata goli la kwanza au hata inafika kipindi inabidi tughairiahe mchezo kutokana ma kuchelewa kwangu kukojoa, kwakweli linanyima raha sana, ili tatizo sijui nini cha kufanya ili niwe normal kama wenzangu dakika tano wanakojoa.

Msaada wadau.
 
Hilo sio tatizo, wewe ndio tatizo kwanza unapokuwa unafnaya lile jambo hakikisha akili yako iko pale na inawaza lile jambo au mwenza wako, jiandae wewe kwanza kiakili halaf upo uwezekano mwenza wako si mzuri katika kukuuandaa, inawezekana hajui kukuandaa pia.
 
Umeelezea la kwanza linachelewa, itakua la pili linawah ndio maana hujalilalamikia
 
Concentration na tendo kwa muda ule sio unafanya tendo huku unawaza usiku utakula nin mkishamliza Game
 
unajua frictional force ndio inafanya ukojoe fasta sasa kama wewe unaogelea kwenye mabwawa ambayo yana near zero friction shauri yako
 
Works for me as well, really like how i get to control my emotions during sex. Nashukuru anaridhika na kuna siku niliwahi mfanyia kusudi ili ku prove hilo. Alilalamika huyooo sintosahau aisee!
 
Utapigaje stori za msiba katikati ya tendo. Huoni kama utakuwa unamkata stimu mwenzio na pia akijua unachomoa ili usipizi huoni kwamba atakuoa dhaifu.
Mi nadhani muda wa kujizugisha ni bora ufange jambo ambalo halitamfanya awaze kuwa unapumzika labda ujifanye unaongeza sauti ya redio au kufunga pazia vizuri. Ikibidi jifanye kama unambidua then ulifanye kama njonjo lako kwa bed.Au kubadili nyimbo katika redio then urudi kati patamu.
 
Trip ya kwanza dakika 15 halaf ya pili nusu saa hapo vp au bado tu ?
 
Wakuu tatazo hili linanisumbua sana huwa nikianza kusex na girlfriend wangu nawahi kupga bao kabla yeye hajafka kileleni ila nikiendelea kwa round zingne yeye anaweza fika hata mara 3 ila mi bado hadi nikimwachia anaumia ila mi bado mjeredi uko straight unataka mambo swali langu ni kwamba nitafanyeje ili nisiwe nawahi kumwaga bao la kwanza na je kwa hapo ninatatzo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…