El Merreikh Vs Azam FC 28/02/2015

El Merreikh Vs Azam FC 28/02/2015

Casuist

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2014
Posts
1,189
Reaction score
2,970
Baada ya furaha ya kufuzu raundi nyingine kwa Yanga, leo tuwe pamoja kwa wawakilishi wengine wa Tanzania, Azam FC. Tukumbuke mechi ya kwanza iliyochezwa Dar es Salaam, Azam ilishinda goli mbili bila.
===========

00' Kipenga kinapulizwa kuashiria mwanzo wa mpira kati ya El Merrikh na Azam FC

16' Goooooool, El Merreikh wanafunga goli la kwanza

29' Himidi yuko chini kutokana na maumivu, magoli bado 1-0

32' Mabadiliko: John Bocco anaingia kuchukua nafasi ya Brian

39' Himidi Mao anapewa kadi ya Njano

42' Shomari Kapombe anapewa kadi ya njano na mpira wa adhabu kuelekea lango la Azam FC

45+' Salum Abubakar anaangushwa chini na unapigwa mpira wa adhabu ndogo kuelekea El Merreikh

45+' Mpira unaenda mapumziko na magoli yanasalia 1 kwa Wasudan na 0 kwa Azam FC

45' Kipindi cha mapumziko kimekwisha, mpira umeanza na El Merreikh wanapata penati kuelekea Azam

46' El Merreikh wanakosa penati kwa kupiga mpira nje

54' Mabadilio El Merreikh: Aimar Said anaingia kuchukua nafasi ya Abdallah

57' Mabadiliko Azam FC: Frank Domayo anaingia, Magoli bado 1-0

70' Manula anajitahidi kuokoa na unakuwa mpira wa kona

72' Muhidin Mao anaugulia maumivu na kusaidiwa na watu wa huduma ya kwanza, matokeo bado 1-0

78' Mabadiliko Azam: Said Morad anaingia kuchukua nafasi ya Kipre Tcheche

84' Gooool: El Merreikh wanapata goli la pili baada ya ahmed Abdallah kupiga mpira wa kichwa

87' Kunatokea vurumai uwanjani hapa na wachezaji wa El Marreikh wanamzonga refa

90+' El Merrikh wanapata goli la tatu

*Mpira umekwisha kwa tamati ya 3-0 hivyo kufanya matokeo ya jumla kuwa El Mereikh 3-2 Azam hivyo Azam wanashindwa kuendelea na mashindano, pole yetu sote
 
Baada ya furaha ya kufuzu raundi nyingine kwa Yanga, leo tuwe pamoja kwa wawakilishi wengine wa Tanzania, Azam FC. Tukumbuke mechi ya kwanza iliyochezwa Dar es Salaam, Azam ilishinda goli mbili bila.
===========

00' Kipenga kinapulizwa kuashiria mwanzo wa mpira kati ya El Merrikh na Azam FC

16' Goooooool, El Merreikh wanafunga goli la kwanza
Tarehe 28/01/2015? haya
 
mwenye kujua kinachoendelea sudan tupeni updates
 
Kuna sehem nilipita nikakuta wale watu wa vijiweni wanabishana kuwa hiyo mechi haitaonyeeshwa kituo chochote... Ni siri hata watu wamekatazwa kuingia na camera hakuna waandishi wa habari.... yaani alikua anawadanganya wenzake live na wenzake wakawa wameamini
 
Mpwa kijiwe gani hicho?
 
Ndio ukweli sio kwamba alidanganya wasudani nao wameanza ushenzi wa misri ingawa zama hizo zimepita
 
Back
Top Bottom