mnakumbuka "God Father"... hata wanaodhani wajanja wanaweza kupwa offer they can not refuse.. ni offer ambayo ukikataa utalipa! So, Bi. Senti over the weekend kanitumia ujumbe kutoka mkubwa fulani na wakasema wanipe ofa ambayo siwezi kuikataa.. now baada ya kuisikiliza ofa yenyewe nimeshindwa kuikataa jambo nimeikubali kwa machozi na kulia chonde chonde..
Ila wheelchair yangu ni ile kama ya Stephen Hawkings.. miye nimeketi tu huku mkono mmoja unafanya kazi zake..
Wandugu.
Katu siwezi kumlaumu mtu kwa kufanya maamuzi yenye lengo la kuboresha maisha yake bila kudhuru maisha ya wengine.
Siwezi kumlaumu Mtu kwa kujihami na kulinda uhai wake pasi yeye kuwa chanzo cha kuhatarisha maisha ya wengine.
Kwa hakika nitamheshimu mtu wa namna hiyo na pia kumuunga mkono kwa juhudi zake ama step zake hizo.
Lakini Mtu aliye tayari kuuza Principle za utu/haki/ uhuru/upendo/ukweli uliodhahiri na wa dhati kwa thamani chache ya vipande 30 vya fedha mtu huyo ni mtu asiyefaa kabisa kabisa.
Duniani zipo ofa, Nabii Muhammad aliahidiwa Ufalme na waarabu iwapo atakoma kuendelea na mafundisho yake, lakini akakataa akasema yupo tayari kufa na umasikini wake kuliko kuacha kufanya kazi hii ya kutangaza haki.
Lakini ukiwachunguza watu makini kwa nini hukataa Ofa za namna hiyo?. ni kwa sababu hutambua kwa dhati kwamba wakati mwingine mtu inabidi ukatae ofa inayopelekea kutokutimiza wajibu wako.
Nelson Mandela alisema yuko radhi kufa ikibidi ili kutetea misingi ya haki kwa ajili ya watu wake.
Iwapo Mtu yuko tayari kutoikataa Ofa nono, na kwa gharama ya ofa hiyo akauza utu wake, akauza watu wake, mtu wa namna hiyo ni mtu msaliti.
Ni mtu ambaye akipewa dhamana kubwa na watu yuko tayari kuwauza watu wake kwa visingizio vya ofa nono na kwa namna hii mafisadi wote wanaozungumziwa nchini wamepitia Hatua hii.
Well Mapambano ya kifikra siyo lelemama wandugu wana JF.siyo kila askari aliyependezwa na gwanda basi ni askari mahiri.
Kuna watu walisema tutaona vioja vingi Mwaka huu.
Kwamba Unaposhindwa kuwashawishi kwa hoja ambao unadhani wanakosea basi njia muafaka ni kuwakubalia mawazo yao. kweli haya ni maajabu.
Waache wawanunue wasanii kina (ze-comedy?) and the likes, waache wawanunue waandishi kina (nani?). lakini kwa kufanya hivyo wasidhani watakomesha mirindimo ya kilio cha wasaka haki.
Ama kweli Muona usiku kwenye giza nene totoro yampasa awe makini sana mchana kwenye mwanga mkali, la sivyo siku akijatahamaki atagundua kwamba kumbe alikwisha pofuka kitambo sana.