PostGE2025 ELAF: Walioua raia, waliochoma vituo vya mafuta wachukuliwe hatua

PostGE2025 ELAF: Walioua raia, waliochoma vituo vya mafuta wachukuliwe hatua

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Baada ya vurugu zilizojitokeza kufuatia uchaguzi nchini na kupelekea baadhi ya vijana kupoteza maisha, uharibifu wa mali za umma na biashara, taasisi ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imetoa wito kwa viongozi wa dini na wadau mbalimbali kuhubiri amani, maridhiano na busara.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Dkt. Hamisi Masoud, amesema kuwa katika kipindi hiki viongozi hawatakiwi kutoa kauli za kuchochea au kuleta taharuki miongoni mwa wananchi ambao tayari wana hofu, hasira na simanzi. Amesisitiza kuwa haikubaliki kuzungumza mambo ya taharuki, na kama ni jambo la kikao cha ndani, basi libaki ndani.

Dkt. Masoud amesema kuwa inapozungumzwa kuhusu amani ya nchi, ni jukumu la kila Mtanzania kuhakikisha inalindwa. Ameongeza kuwa endapo kutatokea mtumishi wa umma anayetoa kauli au kuchukua hatua zinazoashiria kutaka kuipeleka nchi pabaya, wananchi hawapaswi kunyamaza bali wamshauri Rais kuangalia upya kikosi chake.

Aidha, Dkt. Masoud amegusia kauli za baadhi ya Wakuu wa Mikoa ambazo zimeonekana kuleta taharuki na utengano badala ya kuhimiza subira katika kipindi hiki. Amesema ni wakati wa viongozi wote wa umma kujitafakari, hasa baada ya matukio ya kuvunjwa kwa haki za watu katika maandamano ya Oktoba 29 yaliyosababisha vifo vya raia.

Ameongeza kuwa Ofisi ya Taifa ya Mashitaka (NPS) iliyo chini ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ni ofisi ya umma, hivyo haipaswi kumlinda mtu yeyote anayehusika na matukio hayo, hata kama ana mamlaka.

Dkt. Masoud amehitimisha kwa kutoa wito kwa viongozi wa dini, watumishi wa umma na wadau wote wa kijamii kuhubiri amani, mshikamano na busara ili taifa liweze kurejea katika hali ya utulivu na umoja.
 
Watu wanadai haki, ni rahisi kuipata Amani kwenye Haki lakini kuanza na Amani na Haki hamna ni muujiza mwingine.

Alafu mbona viongozi wa dini wanakuwa mbuzi wa kafara. Ni wapi hawa viongozi walikaa kimya wasihubiri amani? Kabla ya uchaguzi viongozi na taasisi zilihubiri na kutoa ushauri kwa wahusika lakini waliziba masikio.. sasa leo maji yashamwagika eti ndo mnaona umuhimu wao, huu ni unafiki na dharau kwao.

Waacheni wawe huru maana kwanza mlishawaambia wasijihusishe na siasa sasa leo mmewakumbuka mmesahau nini kwao?
 
Back
Top Bottom