carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Mkurugenzi wa Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF), Dkt. Khamis Masoud, amependekeza kuundwa kwa kitengo maalum ndani ya Jeshi la Polisi kitakachoshughulikia taarifa na uchunguzi wa watu wanaopotea, kikifanana na vitengo maalum vilivyopo vya kuchunguza uhalifu wa kifedha.
Dkt. Masoud amesema ujasusi na uchunguzi vinapaswa kuzingatia ushahidi, weledi, nidhamu na dhamiri ya kutafuta haki, badala ya kutumika kunyamazisha watu kinyume cha sheria. Ameeleza kuwa kitengo hicho kinapaswa kuwa na wataalamu waliobobea katika haki za binadamu, uchunguzi wa kidigitali na taaluma nyingine za kiuchunguzi ili kuhakikisha taarifa za watu wanaopotea zinachakatwa na kufanyiwa kazi kwa haraka na weledi.
Chanzo: Habari Digital