Ndugu Wananchi;
Sheria imeainisha vizuri mambo yanavyokatazwa kwa upande wa matumizi ya fedha za uchaguzi. Sheria inakataza, kwa mfano, vitendo vifuatavyo visifanyike pamoja na matumizi ya fedha kwa ajili hiyo kuzuiliwa:
1. Kufanya malipo kwa wapiga kura ili wamchague mgombea fulani;
sawa nakubali kwa 100%
2. Kuahidi kazi au cheo au wadhifa kwa mpiga kura ili amchague mgombea;
Sikubali kabisa. Nitakubali kama zaidi ya cheo na wadhifa akiweka neno kuhahidi miradi kama ya barabara , umeme kwa wapiga kura
3. Kutoa zawadi, ahadi, mkopo, au makubaliano yoyote kwa mpiga kura ili amchague mgombea;
Nakubali kwa 70% lakini ufafanuzi wa neno MAKUBALIANO unahitajika
4. Kukubali kurubuniwa kwa mambo yoyote yaliyotajwa hapo juu ili ampigie kura mgombea yeyote;
Neno KURUBUNIWA linahitaji ufafanuzi. je mwanafunzi wa miaka 18 na mtu wa miaka 45 wanawekwa kwenye fungu moja
5. Kufanya vitendo vyovyote kati ya hivyo wakati wowote kabla au hata baada ya uteuzi wa mgombea;
Hapa sijaelewa na sikubali
Mhh hapa kuna utata mfano waziri anaweza kwenda jimboni kwake akatoa ahadi kwa mgongo wa serikali na hata kabla kampeni hazijaruhusiwa. Hii inawabana zaidi wapinzani. wafafanue.KABLA NA BAADA ya uteuzi wana maana gani.
6. Kutoa malipo kwa ajili ya takrima ya chakula, vinywaji au starehe yoyote kwa ajili ya kuwashawishi wapiga kura wamchague mgombea;
Sawa Nakubali kwa 80 %
7. Kuwasafirisha wapiga kura ili wamchague mgombea. Hata hivyo Sheria inaruhusu wapiga kura wenyewe kujilipia nauli kwenda kupiga kura au Serikali kuwasafirisha wapiga kura pale ambapo kuna shida ya usafiri;
-- Sijaelewa nakataa hii inahitaji ufafanuzi sabbu serikali ni ya chama fulani labda angesema Tume ya uchaguzi lakini mhhh