Election Expenses Bill 2009


Hapa rais anazungumzia mbunge mtarajiwa kumuahid kasheshe cheo, etc. kosa wapi wandugu... mbona mnaturudisha nyumba?

tatizo lako ni kuwa unafikiri siasa ni kushawishi wengi; siasa ni kushawishi mmoja mmoja. Kura inayopiganiwa siyo kura ya wengi ni kura ya mtu mmoja. Na hivyo mgombea yoyote anafanya kazi kubwa ya kupigania kura moja. Na hivyo, hawezi (kwa mujibu wa sheria hii) kutoa ahadi kwa mpiga kura mmoja ambayo itamfanya mpiga kura huyo amchague..
 
Rais akafafanua hivi vile vile:


Je hii ina maana gani? na itakuwa na matokeo gani?
 

Nadahni mambo mengi yanaongeza utatata unless Muheshimiwa angefafanua zaidi labda tungepata mwanga.
 
Mkuu emesema kweli, hawa jamaa hawajaweza kutimiza ahadi walizotoa 2005 kwa hiyo hawana cha kuahidi kipindi hiki ndio maana wanataka kukataza wenzao wasiahidi. Wanataka mje tu na bla bla za umoja na amani, chama kikongwe n.k n.k
 
Labda nitumie mfano hai:

Kule Kyela, wakati wa kura za maoni ni formula gani itatumika kugawa fedha kwa Mwakalinga, Mwakyembe, Mwakipesile, na Mwanjala? kwa sababu hawaruhusiwi kukusanya fedha zao wenyewe na matumizi ya fedha kwa kila jimbo yataamuliwa na Waziri?

a. Je wote watapewa kiasi sawa?
b. Kwa vile kampeni zote zitaendeshwa na chama, je kutakuwa na msisimko wa uchaguzi tena?
c. Kama mgombea ana fedha yake ya ziada na anajua kuwa kiasi alichotengewa na chama chake hakitoshi kufikisha ujumbe kwanini azuiwe kutumia fedha zake au kutafuta fedha zaidi?
 
Rais akafafanua hivi vile vile:



Je hii ina maana gani? na itakuwa na matokeo gani?

kuna Mfanyabiashara anaitwa kishimba wa Mwanza alimfhadili mzee mapesa( John cheyo) kwenye urais na kampeni za ubunge kanda ya ziwa.

Kilichofuata baada ya uchaguzi kuisha TRA walipiga mehasabu ya kodi zake miaka minne nyuma akaonekana anadaiwa na alikuwa anakwepa kodi.(kama ni kweli au uongo hilo ni suala lingine) alitakiwa alipe hela kibao na ndipo alianza kutetereka kidogo.

Watu wengi wenye nia njema wataogopa. Na ukizingatia kuwa sucessful kibiashara sio uwongo lazima kuna kodi kodi uzikwepe au kuzifanyia usanii. kazi ipo
 
Kwa vile michango yote sasa itakuwa inaenda kwa vyama vya siasa.. unafikiri ni chama gani kiko katika mazingira mazuri ya kuchangiwa zaidi?
 
Kwa vile michango yote sasa itakuwa inaenda kwa vyama vya siasa.. unafikiri ni chama gani kiko katika mazingira mazuri ya kuchangiwa zaidi?

Ni wazi ni CCM kitafaidika zaidi

kuwa na uwanja sawa na wa haki wa ushindani sheria inabidi itambue vyama hivi vyote havijazaliwa 1990. kuna mabadiiko mengi inabidi yaangaliwe

Kuna chama kilifaidika na kupata michango ya kukatwa kodi watanzania wote . kinahodhi rasilimali na mali nyingi za watanzaia na hata baada ya mfumo wa vyama vingi bado mali na rasilimali hizi ni za chama.

Kwa upande 1ja sheria inaweza kufanikisha kupunguza matumizi ya hela chafu ndani ya CCM lakini upande mwingine inapunguza na kudumaza demokrasioa ya kweli hasa kwa vyama vya upinzani amabavyo ni vichanga.
 

Mind you, sheria ina kiwango cha juu cha matumizi ya uchaguzi kwenye jimbo... so it doesn't matter chama chako ni tajiri kiasi gani, hautaruhusiwa kutumia zaidi ya hapo.
 
Mind you, sheria ina kiwango cha juu cha matumizi ya uchaguzi kwenye jimbo... so it doesn't matter chama chako ni tajiri kiasi gani, hautaruhusiwa kutumia zaidi ya hapo.

Mhh this is interesting...I am curious serikali na washauri wake walitumia vigezo gani kuweka hicho kiwango cha juu.
 
Mind you, sheria ina kiwango cha juu cha matumizi ya uchaguzi kwenye jimbo... so it doesn't matter chama chako ni tajiri kiasi gani, hautaruhusiwa kutumia zaidi ya hapo.

Ok aksante kwa ufafanuzi lakini bado naona bila kufafanuliwa zaidi muswada huu una utata mwingi mfano

Chama cha mapinduzi kina magari au kina gari kila wilaya wakati vyama vingine havisa usafiri. Ukisema kila jimbo maximum ni shilingi 1000 hawa wengine watatumia shilingi 500 kwa usafiri na 500 kwa kazi nyingine wakati CCM tayari wana rasilimali wao watatumi 1000 zote kwenye kazi halisi za kampeni . je Kutambua kiasi gani chama kimetumia zimetumika wataingiza kwenye mahesabu mpaka asset za chama zilizotumika. kama bend za TOT na magari ?
 

Heshima yako mkuu,

Hapo kwenye red, hiyo balance kuipata ni ngumu sana. Kwa kuongezea sioni kabisa uwezekano wa CCM kuwepo madarakani halafu watunge sheria ambayo kwa kiwango kikubwa inanufaisha vyama vya upinzani.

Ni realiaty ambayo ni muhimu tuikubali kuwa chama kikiwa kimeshika dola, kinakuwa na added advantage.
 


Kunaweza kuwepo na "loop hole" kwenye sheria, badala ya kutoa fedha kwenye chama Wanachama wanaweza kuchangia nyenzo kama magari, kujitolea kuimba au kufanya kazi bila kulipwa..??
 

MMKJ hajakosea kitu yeye kaleta summary ya bill tuijadili hakuna ubaya wowote hata bungeni misuada hujadiliwa kabla ya kupitishwa wewe ndiye uliye na spinning umechoshwa na hoja zake kwa hiyo kila anacholeta MMKJ lazima litakukera hata hivyo hata yeye kauliza hakuja na conclusion yake
 
Tatizo halipo kwnye sheria,lipo kwenu mnaoisoma kama vile kipeperushi cha udaku! kama mtakuwa mnachukua kipande cha neno na kujengea hoja, hata vitabu vyenu vya dini mtavikosoa tafsiri sahihi. jifunzeni kusoma kabla ya kusoma. wengi wenu mnaanza kusoma sheria kabla ya kujifunza ndo matokeo yake mnajiaibisha. sheria hutungwa kwa kufuata Liberal meaning sasa nyie mkizoea kuifasiri kwa literal meaning mtaona kila sheria imekosewa kumbe wewe ndo unakosea kukosoa.Tumkosoe JK kwa lingine sio hili.
 


hili ndilo tatizo kwa swababu unafikiri wote tunashindwa kuelewa sheria na jinsi inavyotungwa. Tunapozungumzia Law of Unintended Consequences tunataka kuona kila ambacho sheria itafanya bila kukusudia. Sasa wewe ukitunga sheria bila kufikiria matokeo yake yasiyotarajiwa ndiyo unashindwa kuelewa kwanini wawekezaji wa Tanzania katika madini wanatangaza hasara miaka nenda miaka rudi; baadaye mnafikiria kubadilisha sheria ya madini ya 1998 kwa sababu hakumfiria matokeo yake yasiyotarajiwa. Ndiyo hilo la kweli kwenye Sheria ya Fedha na mambo ya Capital gain ya 2001 na ni kweli pia kwenye sheria ya Maadili ya Umma ya 1998 na ni kweli pia kwenye Sheria ya Usalama wa Taifa ya 1996.

Sheria zote hizo mmezitunga vizuri tu na with "liberal meaning" matokeo yake mmetengeneza loopholes za kutishia demokrasia na uhuru wetu kwa sababu mnafikiri watu wote hamnazo!

Ukiisoma hiyo sheria with your liberal mind. Je mtu akichangia shilingi laki 999,999 kwa chama anatakiwa kutangaza?
 
Mind you, sheria ina kiwango cha juu cha matumizi ya uchaguzi kwenye jimbo... so it doesn't matter chama chako ni tajiri kiasi gani, hautaruhusiwa kutumia zaidi ya hapo.

you can't do that!! we are in a democracy not a tyranny of the party! mimi kama nina fedha zangu za kutosha kujitangaza katika kugombea ambazo nimezipata kihalali na natangaza kuzitumia kihalali kwanini serikali iniwekee kikomo kwa sababu mtu mwingine hana kama mimi? Huu ni udikteta wa chama and you don't see any problem with that.
 

aaaaahaaaaa kumbe hujaisoma sheria/muswada....Mimi nadhani tungesoma kwanza kabla ya kupoteza muda hapa, mheshimiwa rais amegusia kwenye 3. hapa chini.

Mheshimwa Rais anaendelea


Najua utasema makosa ya JK... lakini haya yako kwenye sheria sasa sijui alishika akili za wabunge na kalamu zao... I don't know
 

nimeisoma.. ndio maana nimeuliza... siulizi kutoka hewani! Yaani, mtu mmoja tunampa madaraka ya kuamua nini kinafanyika kwenyejimbo? Hivi huoni kuwa unintended consequences zitasababisha baadhi ya majimbo kutengewa fedha zaidi na hilo la "etc" ndio linandokeza discretion kubwa ambayo tunataka kumpa mtu mmoja. Sheria haiweki kanuni hasa ya kugawa hizo fedha kwa wagombea au kwa jimbo. Kuna majimbo yatapata zaidi (maana yake wagombea wake watakuwa na uhuru mkubwa wa kujitangaza, na majimbo mengine yatakuwa na fedha kidogo na matokeo yake yanaweza kutabiriwa)?

Huoni kwamba katika misingi hiyo the incumbent atakuwa na unfair advantage?

Unapokubali kuwa serikali iweke mipaka ya kiasi kinachoweza kutumika kwenye jimbo, je uko tayari kuona serikali ikiweka mipaka idadi ya magari, vipeperushi, matangazo ya radio, tV n.k ambayo chama kinaweza kuyafanya kwenye jimbo ili kuleta uwiano? Je huoni kuwa inatishia uhuru wa kujieleza?
 

You are right Kasheshe, make sheria ikisema mpiga kura inamaanisha mtu mmoja, na hiyo yaweza kuwa illegal, make hapo mgombea atakuwa anafanya signs za rushwa, ilitakiwa sheria itoe ujumla wa wapiga kura na sio mpiga kura, any way bwana, The Mwana Village yupo sawa, make hata ilani ya CCM tayari ikitafsiriwa inaashiria rushwa, make unawaaidi wananchi vitu ambavo havipo katika mazingira ya kawaida------ahadi lukuki, we angalia 2005 ahadi zilikuwa ngapi kutokana na ilani yao, sasa Mr President anasema sheria imekataza wagombea kutoa ahadi, ilani je, si ahadi hizo jamani, bsi waondoe hata ilani za vyama, wagombea waje na policy na strategies zilizokaa kiinchi zaidi badala ya vyama, halafu huu mfumo wa mgombea uraisi kutumia 100% ilani ya chama it is wrong, huu sio wakati wake, wakati wa chama kimoja ilikuwa ok, sasa utakujaje na ilani ya chama wakati nchi sio ya chama kimoja, so what happen hata raisi akichaguliwa kwa kishindo 80% what about 20% ambao hawakumchagua,

mimi naona 2010 wagombea uraisi waje na agenda zao at least 65% and 35% za chama, ili tujue hawa watu wana uwezo gani kufafanua policies and what kind of strategies have put on focus when elected, sio tu mtu anakuja na kuanza kuimba jukwaani kuhusu CCM, tell people the policies you have put forward, in your tenure as a president how the country is gonna move forward----badala ya ngonjera za akina Komba---ccm,ccm---what is that?????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…