Infinite_Kiumeni
JF-Expert Member
- Jan 23, 2023
- 382
- 687
Kila mtu anamkatisha mwengine tamaa kwa namna moja au nyingine. Lakini ni juu yetu kupunguza hizo tabia, na kuruhusu wengine wawe bora zaidi. Unapoona mtu anajitahidi, usimshushe chini. Angalia maneno yako unayoongea. Maneno yako ni kioo cha akili yako. Inaonesha akilini mwako umejaza nini. Yatoe kwa umakini.
Kumkatisha mwenzio tamaa inatokana na ujinga.
Haijalishi una kitu gani/ umri gani, kila mtu ni mjinga sehemu fulani. Ujinga hujionesha unapokutana na usichokijua. Kuna wengine watatafsiri kwa kutaka kujifunza wengine wataona wanadharauliwa. Ukiona umedharauliwa katika usichokijua, hapo ndo utaanza kumkatisha tamaa mwenzio. Sababu utakua na wivu na chuki kwa usichokijua.
Na kwa vile umejiona umedharauliwa, watu wengine itakua rahisi kukudharau zaidi. Sababu umeongoza watu wengine kukuona wa kudharauliwa. Maneno yako yatachangia zaidi kudharauliwa.
Kuna ka hisia kwamba utapitwa au utaonekana mdhaifu zaidi ya mwenzio. Lakini usiiruhusu hiyo hisia ikakufanyia maamuzi. Bali ichukulie inamaanisha ni muda wa kujifunza. Punguza jazba na acha kung’ang’ania unachokijua. Usijilinde kwenye kile ukijuacho na kulazimisha icho tu. Bali utambue fursa mpya uliyoletewa ya kujifunza. Tambua kuna vitu vingi vya kujifunza, yote ni elimu-elimu ni bahari.
Hata kama ni mzazi, tambua una kitu cha kujifunza kwa mwanao. Ukiona rafiki yako anajitahidi kusoma usimkatishe tamaa. Ukiona mtu anahangaika kuacha punyeto usimkatishe tamaa. Ukiona rafiki yako anataka kuanza biashara usimkatishe tamaa. Ukiona mwenzio anatafuta mwanamke mzuri usimkatishe tamaa. Ukiona bonge anajitahidi kujiweka fit na kupungua usimkatishe tamaa.
Pia, Ukiona mtu anakukatisha tamaa usifadhaike/ usiumie. Sababu chochote anachosema/ anakifanya mtu ni kioo kuhusu yeye. Kama anakuita mpumbavu, ujue ye ndo anajiona mpumbavu ila anaogopa kuwa peke yake.
Anachosema/ anachofanya ni hisia tu kutokana na kile ulichosema/ ulichofanya. Mtu hawezi fanya/ sema chochote ambacho hakijui. Wala usirudi nyuma, we tambua tu hiyo ni shida yake na sio shida yako.
Na uzuri ni kwamba hata unapokatishwa tamaa kuna cha kujifunza.
Usichukulie vibaya ukikatishwa tamaa. Bali iangalie kama mrejesho wa kuzidi kuboresha njia yako. Muda mwingine sio lazima mrejesho uwe mzuri. Ukichukulia mambo hivyo, ni ngumu kukatishwa tamaa, na utazidi kusonga mbele. Nikutakie Siku Njema Bila Kukata Tamaa Kwa Kile Ukifanyacho.