Elezea changamoto za mikopo inayotolewa kupitia Application za simu

Elezea changamoto za mikopo inayotolewa kupitia Application za simu

Mr Why

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2019
Posts
2,235
Reaction score
4,252
Wanajamvi zipo changamoto nyingi kuhusiana na mikopo inayotolewa kupitia Application za simu kama Umoja Loan, Premium, Branch na wengineo ikiwemo mteja kubambikiziwa riba kubwa sana zaidi ya asilimia 15% na tishio kwa mteja anayeshindwa kulipa kwa wakati, elezea jinsi ulivyodhalilishwa na mikopo inayotolewa kupitia simu

Je, hawa wakopeshaji serikali inawatambua?

Riba ya mkopo ilishapangwa na serikali sana inawezekanaje mtu akope laki tano alipe laki saba na nusu? Je yeye atakuwa kapata faida ya kiasi gani?

Sio hivyo tu pia rejesho hilo lirejeshwe mwisho wa wiki haya ni masharti ya aina gani? Labda tumulize MO na Bakhresa huwa wao katika biashara zao wanapata laki mbili na nusu kwa kila laki tano wanayowekeza?
 
Back
Top Bottom