Elfu arobaini (40,000) ilivyobadilisha maisha yangu na changamoto nilizopitia katika biashara

Jitathmini usije ukawa bado unakula bata zile zile matumizi bado ni kama yale ukiwa juu, maana hiyo ndio inafanya wengi wanashindwa kupanda tena , kwa kipato kuishia kwenye matumizi na kukupoteza zaidi jitathmini
😂 😂

Hakuna cha matumizi wala nini, kuna kipindi mambo yakigoma kwenda yamegoma, sisi tunabaki kufanya jitihada sababu ni wajibu wetu, yakiamua kutiki yatatiki, yakigoma hata uzikiri uchi, ni bure tu.
 
Mbeya bar yako iko wapi wkend nije kukuungisha bia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekuwa inspired sana na hii story Hongera sana na pole..[emoji123]
 
vyema maisha lazim upitie phase zote ukiruka lazima uirudie ila pambana utatoboa age mate
 
Nakupongeza sana ila nakushauri acha hizo fikra za umri kwamba ukifika 30 utakuwa umetoboa. Binafsi kabla ya 30 nilikuwa njema sana hadi nafika 32 bado nilikuwa nakimbiza kwenye biashara. Ila nilikuja kupigwa na dhoruba kali sana leo nakaribia 40 nimerudi kule karibia na mwanzo. Kinachonisaidia ni roho ngumu na uzoefu mkubwa niliopata huku mtaani. Jiweke tu kuwa bora kila siku ila achana na habari za umri. Babu wa Samunge alitoboa uzeeni baada ya hustles za miongo kadhaa. Na kuna waliotoboa wakiwa na 23yrs wakaja kuanguka na hawakuweza kusimama tena.
 
Hongera bwaashee, unaendeleaje sasa ivi?
 
Maisha haya kuna kupambana na ngekewa inahusika.
Unaweza ukapambana sana na bado usifike ulipokusudia.
Nadhani maisha yanahusisha vyote. Nina rafiki yangu, he is 35 yani ameanza kukamata pesa nyingi akiwa 25 na anazitumia vibaya, lakini anapata nyingine hadi lwo yuko hivyo yani ni sawa pesa inamfuata na anaitumia vibaya katika uwekezaji mbaya mbaya tu. Lakini kupata 20, 30 mls kwake kawaida.
Kuna mwingine ni naibu waziri kwa sasa, hakuwa na ndoto ya kuwa mbunge wala mwanasiasa kama wenzake, ila alifuatwa akaambiwa achukue fomu agombee kura za maoni na bado akawa wa pili toka mwisho, ila jina likarudi akagombea, na akapewa unaibu waziri. Hiyo ni zali.
Hata mimi kuna kazi huwa zinanifuata si kwamba labda ninajua kuliko wengine huwa naona tu Mungu kanifungulia riziki.
Nadhani maisha ni zali + juhudi. Vikibalance unatoboa.
Ila pia jambo muhimu kuliko vyote ni having the right information. Naamini information ndio mtaji mkubwa kuliko vyote.
 
Hivi nyie watu wa Moshi mnangaika na kuteseke hivyo unafikiri mlitumwa pesa kwenu loh!! mimi niangaike kwenye shamba la nyanya mshahara 100k, life is not all about money, life is beyond money
Pesa inazidiwa na oxygen pambana pambana pambana.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…