Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu, kulijenga Taifa la Tanzania kunahitaji ushirikiano baina ya Taasisi mbalimbali na ni jambo lisilokwepeka hivyo ni vyema kukaa kwa pamoja ili kujua majukumu ya kila mmoja katika kutafuta mustakabali wa kuzuia biashara hiyo. Maswi amesema wapo baadhi ya watu wasiowaadilifu ambao wanaweza kushiriki kwa namna moja au nyingine katika utakatishaji fedha jambo ambalo halikubaliki Kisheria.
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Boniface Mwabukusi amesema TLS ni chombo cha Kisheria na Viongozi wake wameapa kuisimamia Katiba na Sheria na hawapo tayari kusimama kama kizingiti cha kuzuia utekelezaji wa jambo ambalo linaleta maslahi mema katika Taifa.