SoC02 Elimu bila ajira

SoC02 Elimu bila ajira

Stories of Change - 2022 Competition

Jacksonmyula

New Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
3
Reaction score
2
ELIMU BILA AJIRA
Tanzania yetu ni nchi ambayo inawafanya wanafunzi kuwa na fikra ya ajira hivyo unakuta asilimia kubwa ya wanafunzi wa tanzania wanategemea ajira kitu ambacho kwa upande mwingine ni kazi sana kuajiri wasomi wote na mwisho wa siku wanaopata ajira ni wasomi wachache sana na wengine huishia mtaani bila ajira.

Je serikali ilaumiwe?
Hatuwezi ilaumu serikali kwasababu wanafunzi wanaomaliza vyuo ni wengi kuliko ajira ko wengi wao huishia bila ajira ila serikali haiwezi ajiri wasomi wote hivyo inapaswa kujulikana kuwa wanaosoma wasiwekee ajira kipaumbele kwan haiwezekan wote wapate ajira sasa wanao kosa ajira waende wapi na vyeti vyao kwa upande wangu mim naweza shauri serikali kuhusu elimu ya kujitegemea kwa wanafunzi wa vyuo vikuu ambao wanategemea ajira na hawajui baada ya chuo wakikosa ajira watafanya shughuli gani inahitajika kwenye Elimu yao ya miaka mitatu wafundishwe kuhusu jinsi ya kujiajiri endapo mtu atakosa ajira.


Maisha bila Ajira inawezekana?
Ndio inawezekana lakin siyo rahisi kwan kujiajiri pia kuna hitaji elimu ambayo itamfanya mtu aweze kujiajiri bila ya kutegemea ajira serikalini japo kuwa fikra za wengi wetu tunajua haiwezekeni kujiajiri bila ya kuwa na mtaji jambo hili limekuwa na changamoto hasa kwa watu ambao wamesoma ila wamekosa ajira wengi hukata tamaa maana alichosoma chuoni huwezi pata pesa bila ya kuajiriwa mfano mtu kasomea udactari, uingineer, uanasheria, ualimu na kozi zingine hizo ni baadhi ya kozi ambazo mtu anahitaji ajira kwani ni vigumu sana kujiajiri mwenyewe kwa hiyo unakuta mtu ni msomi ila hana pakuanzia.

Kama serikali ingeweza kuwaandaa wasomi kuwa na uwezo wa ziada ambao unaweza kumsaidia mtu kuishi pasipo ajira mfano serikali ingeweza kuongeza kozi chache ambazo zinahusiana na kujiajiri kama mtu atapenda kuisoma ziwe ni kozi zisizo za lazima yaani ni kwaajiri tu ya kumuandaa mwanachuo kiakili kuhusiana na maisha yake iwapo atakosa ajira mfano wa kozi hizo ni Udereva, Ufundi chereani wa kisasa, Ufugaji, Kilimo, kutengeneza matangazo kupitia kompyuta (graphics design) kozi zipo nyingi ambazo kam mwanachuo akifundishwa anaweza kujitegemea kwa muda ambao hata kuwa na ajira.

Lakini kikubwa hizi kozi zinatakiwa ziwe enje ya mtaala wa elimu yaani mtu asilazimishwe kuzisoma kwa ambao watataka kujifunza wafundishwe kwangu mimi najua kwa mtu ambae atafundishwa namna ya kujiajiri katika ngazi ya vyuo vikuu ni rahisi mtu huyo kujua baada ya chuo iwapo akikosa ajira anakua na ile elimu ambayo itamuwezesha kuishi maisha yake bila ya kutegemea ajira.

KWA UPANDE WA AJIRA
Asilimia kubwa ya ajira zinahitaji uzoefu usio pungua miakia kuanzia mitatu na unakuta ndo kwanza wanafunzi wamemaliza chuo na wanahitaji ajira hii inapelekea wengi wanaotafuta ajira kukaa mda mrefu bila ya ajira kwasababu tu hawana uzoefu na kazi wanazo ziomba hii ni wazi kuwa ni ngumu sana kupata ajira kirahisi hivyo kama msomi akiwa na elimu ambayo itamwezesha yeye kujiajiri ni rahisi kwake kuweza kuishi maisha bila ya kutegemea ajira serikalini lakini iwapo atapata ajira pia ni faida kwake kwani atakua na elimu ya ziada.
 
Upvote 3
Back
Top Bottom