Elimu bila chakula haiwezekani

Elimu bila chakula haiwezekani

Trebla84

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2011
Posts
510
Reaction score
637
Habari ndugu wanajamii forum,

Imekuwa ni kawaida kwa wanafunzi wa maskini wenzangu kukaa shuleni masaa kumi na mbili bila kula, yaani akienda shuleni saa kumi na mbili hapati chakula chochote mpaka saa moja usiku arudipo nyumbani.

Katika pitapita katika mikoa mbalimbali nikagundua kuwa wote wanaoshinda na njaa ni watoto wa maskini wenzangu.
Mtoto hasome kuanzia asubuh mpaka jioni vipindi mfululizo bila kupata chakula chochote zaidi ya maji ya kunywa hapo kama taifa tunakuwa tunajidanganya wenyewe Mana sisi tusiosoma tu mtaani ni lazima nipate chakula Mara tatu au Mara mbili au Mara moja.
Njaa sio kitu kizuri katika masomo hasa kwa wanafunzi.

Wazazi wengi bado wanaamini kwamba Elimu bure basi mwanafunzi anapewa chakula shule na wengine wanaamini kuwa wao wazazi walisomaga bila kula miaka iyo ya 90 na kurudi nyuma.

Tunalitesa taifa la baadae na mwishowe hawapati Elimu yeyote.

Nachoamini ni kwamba Elimu bila chakula haiwezekani na njaa ni adui kwa mwanafunzi.
 
Wazazi ni jukumu lao kuwapa watoto wao chakula au hata uji wa chumvi tuu kwenda nao shule,hizi serikali zetu nyeusi sio za kuzitegemea asilima zote, watoto wetu watafubaa akili.
 
Hivi kumbe mambo yako ivi!!!?// basi km ni vio!! Mashangazi yangu yalinitesa sana basi!!! yaaani ratiba yangu nikiwa na miaka saba kuelekea nane nikiamka kila asubhi najipaka povu la sabuni ndo mafuta yangu hayo!!

naenda shule! kinder garten mpka shule ya msingi....napiga dash kila siku........ mpaka saa kumi na mbili jioni ndo nakula ugali mgumuuu km kiporo! sometimes viazi vya kuchemsha tu, au mihogo ya chukuchuku!

au ugali na mboga za majani tena za kuchemsha tu, maji na chumvi.....baada ya mlo huo, naenda kuoga na kuteka maji kisimani, km siyo zamu yangu kuchunga..... baada ya hapo ninakula msosi,

Na NiNaosha vyombo vilivyo tumika kula chakula cha usiku huo then nasali nalala, hapo sasa ujue shangazi hajaja na li jamaa lake!! tena hilo jamaa lilikuwa tumishi la Mungu aminifu mnoo!!SDA Church ...

Sasa siku shangazi akija nalo hee!! wanakula mapochopocho fresh, ikiwa ni pamoja na viazi vitamu vya kuoka vile! halafu nilikuwaga navitamani sana lkn holaaa!! eti jamaa likija linakula tu. siku moja nikaviiba, nikala vitamuuu heee!

ok! tuendelee .......wakisha kuja sasa sie tunapigwa slogan tu kuwa ''tumetembelewa na Mgeni mtu wa Mungu leo, ni baraka sana hii'' ....so wana tutegea tulale kwanza fofoffooo,

tukisha lala sasa, wanakuja kula mambo live! na kucheza kila aina ya sarakasi!! mbele yetu!...mkubwa wangu yeye mara nyingi alikuwaga hajui hii picha mie ndo nilikwa namfungua akili zake! alikuwa nalala fofofooo!

kimbembe sasa sie kina kajamba nani kulala ni kwenye Mashuka yenye chawa, utitiri, uchafu, baridi, ukweli ni kwamba iilikuwa ikifika jioni tu! roho inaniuma saaana, kwa yale mateso nayoenda kukutana nayo kitandani...

yaani chawa utitiri vilikuwa vyangu, ngozi ilikuwa haitamaniki, kwa kujikuna. ngumuuuu! suguuuuu! halafu ilikuwa inawasha eb fikiria hayo matesooo!

ngozi yangu ilikuwa ngumuu km ya kenge sababu ya kujikuna kuna mara kwa mara!! nakutokuoga mara kwa mara nilikuwa gumzo shuleni! hasa wkt wa kucheza michezo km mpira! kupokezana vijiti.nk,

kutokana na uniforms zangu kuchakaa kabisaa, kuchanika matakoni na chupi sikuwa nayo, ilisababisha kuchekwa na watoto wenzangu, mmoja wao aliyenicheka ni Josephine, ni Mwalimu wa shule ya msingi, leo hii!! ...

Kwa hiyo hali hii ya udhalili!! hii!! ilinifanya nijitenge! na watoto wenzangu, in real fact nilikuwa kivyangu sana tu! kuepuka kuchekwa na kudhalilika, na shule naipenda mnoo! japokuwa sikujua kusoma wala kuandika! nilienda tu!

sikuwa chochote wala yeyote pale shuleni, naweza kusema nilikuwa makapi ya shule tu, kuanzia umri mpaka taaluma duni, isiyo vutia waalimu na wanafunzi wote kwa ujumla wao!!

hata leo ukiwaulizia pale shuleni kwangu nilikopitia walai watanijua mwanafunzi mmoja mmoja sana!! hasaa walee nilio chunga nao ng'ombe! sasa tuendelee......

sweta langu pekee la kijani lililokuwa halina vishikizo!! hili nililipewa na dadangu! kwa sasa ni marehemu ambaye wkt huo alikuwa anaishi mjini!!......kishikizo pekee cha sweta hilo ulikuwa ni mkono wangu! wa kushoto na

Mkono wa kulia nilishikia fimbo ya kuswaga ng'ombe! malishoni, hata wkt wa kilimo shambani halikadhalika machungani vilevile!!...sehemu pekee niliyokuwa nikipumzika vizuri! japo nilikuwa sipati mlo wa mchana ni shuleni tu baaasi!

AU nitapumzika tu! endapo mvua itanyesha mfululizo mpaka usiku utasema kimoyomoyo Mungu umeniona leo mwanao!, lkn ikikatika mapema!! weeee! binafsi ilikuwa ni km majanga rorho inasononekaaa! unatamani ufe!

sababu sasa hapo unaenda chunga tena upyaa kwenye baridi na huna koti wala viatu na sweta lako limechanika , unavidonda vya kujikuna chawa na ardhi imejaa unyevu nyevu!

pia majani yana matone ya mvua sasa kwa hali hii uende uka simame huko kunako unyevu...badala ya kuota moto nyumbani! na kula viazi vya kuchoma, mahindi na ndizi! na kula story..mwee iliuma sana... ukilinganisha na

Ile hali ya kukaa darasani kiusafi, bila bugudha kwenye dawati na kivuri mwanana bila kula, kwangu ilikuwa paradiso ndogo!! ilikuwa ni afadhali mnooo! mara mia ! kuliko kwenda kuchunga mifugo porini bila mlo, tena juani,

Hapo ni hivi baada ya kilimo cha alfajili, kwa kukatiza usingizi! ambao pia ni muhimu kwa mtoto anae kua......suala la Elimu ilikuwa ni lazima kwa kila mzazi dhidi ya watoto husika kwa hiyo lazima tu niende shule! kinyume na hapo utajua unoko serikali ya kijiji! husika.. in real fact

Niliishi mbali Sana na shule, lkn kwa sababu ya kilimo/na kuchunga mifugo isiyokuwa na tija kwangu binafsi. nikadanganya waalimu wangu kuwa naishi hapa karibu na shule,

so kwa sababu hiyo! Mwalimu wangu wa drs akaniandikisha drsa la kwanza B''....kifupi hawakunijua kiundani wala mzazi wangu wala shangazi yangu yeyote, hata kwetu hawakupajua kwa sababu I was nothing to them!!

Ajabu tu ni kwamba kati ya Makazi na makao mazuri, kwa binadamu yeyote anae stahili kuishi sisi tulikuwa na makao mazuri pale kijijini kuliko wooote! hii tu ilitosha kufahamika kwa waalimu na wanafunzi wote pale lkn hola!

Isipokuwa sasa watu tulioishi nao ndani yetu! kuwategemea, ndo ulikuwa mzigo wa karne lkn kwa nje tu tulikuwa njema! ok tuendelee ....

na wale wanaotoka mbali wakaandikishwa Drs la kwanza ''A'' kwa hapa nikawa mshindi, hii yooote ni kukwepa kuchunga mifugo, ambayo binafsi haikunisaidia chochote zaidi ya kumfaidisha shangazi na wanawe kuishi maisha mazuri!

kumbuka haya yooote yanatokea wkt huo nikiwa na umri wa miaka nane 8 tu!! sijakosea narudia nikiwa na miaka minane!
 
Back
Top Bottom