Elimu gani inamfaa mke huyu

specialist88

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2014
Posts
1,140
Reaction score
618
Rafiki yangu anamke mwenye miaka 25, Mke wake ameishia darasa la 7 kutokana nakukosa mtu wakumsomesha elimu ya sekondari+kumuendeleza kiujumla.
Jamaa amejitoa anataka kumwendeleza mke wake awe wakisasa(kujua ulimwengu unavyoenda),aweze kujua computer+matumizi yake katika maisha yake, aweze kuongea nakuandika lugha ya kingereza kwa ufasaha(ukizingatia ndio lugha inayo'run' ulimwengu') na awe na uelewa wakuendeleza biashara atakayomfungulia kwa mtazamo wa mbele zaidi(biashara kama mgahawa wa chakula,kupamba,kupamba+kupika keki)!

Sasa anahitaji ushauri wa wapi aanzie,na kipi kifuatie na sehemu zipi zinatoa ujuzi huo kwa ufasaha +mbinu nzuri ili asije akapoteza fedha.
NB:-Ushauri ndio unahitajika sio majungu+utani utani.

KARIBUNI TUMSAIDIE NDUGU YETU KIMAWAZO.
 
Kwanini usiseme ni mke wako tukushauri? Kama anataka kujua kiingereza na computer basi asome hivyo tuu ila kama anataka asome ili aje aajiriwe hana budi kusoma form 4 ili aendelee vizuri
 
Kwanini usiseme ni mke wako tukushauri? Kama anataka kujua kiingereza na computer basi asome hivyo tuu ila kama anataka asome ili aje aajiriwe hana budi kusoma form 4 ili aendelee vizuri
Ndugu sijaoa...nadhani habari inajieleza kuwa ni rafik yangu ndo anahtaji ushauri.
 
Amuulize yeye mwenyewe anapendelea nn kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…