Elimu haina mwisho; Mikutano ya bunge inahesabiwa vipi?

Mikutano ya bunge inahesabiwa vipi? Huu unaitwa mkutano wa 11 , kuanzia lini? Mwaka huu?
Najaribu kutengeneza dhana.... kuhusu bunge

1960 - 65 Mkutano wa Bunge la 1 hapa tulikuwa na bunge la Tanganyika

Ila baada ya muungano 1964 kati ya Tanganyika na Zanzibar
Awamu ya JKN
1965 - 70 Mkutano wa bunge la 1
1970 - 75 Mkutano wa bunge la 2
1975 - 80 Mkutano wa bunge la 3
1980 - 85 Mkutano wa bunge la 4

Awamu ya AHM
1985 – 90 Mkutano wa bunge la 5
1990 – 95 Mkutano wa bunge la 6

Awamu ya BWM
1995 – 2000 Mkutano wa bunge la 7
2000 – 05 Mkutano wa bunge la 8

Awamu ya JK
2005 – 10 Mkutano wa bunge la 9
2010 – 15 Mkutano wa bunge la 10

Awau ya JPM
2015 – 20 Mkutano wa bunge la 11

Sina mahali nimedesa, ila najaribu kufikiri kwa mtiririko hasa kwa kuwa linaitwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Exactly, dhana yako iko sahihi...

Kwa kuongezea tu ni kuwa "Bunge" na "Mkutano wa Bunge", ni vitu viwili tofauti....

"Bunge" huzaa kitu kinaitwa "mkutano wa Bunge". Mfano katika Bunge la 11 kulikuwa na " mikutano" kadhaa...

Kwa kawaida kila mwaka, bunge huwa na mikutano 4 (kama sijakosea na hii ni bila dharura) ikiwemo "mkutano" mkuu wa kupokea, kujadili na kupitisha bajeti kuu ya serikali....

Huu "mkutano wa Bunge la bajeti" mara zote ndiyo mkutano mrefu zaidi wenye vikao vingi zaidi kuliko mikutano mingine yote......

Ndani ya "mkutano wa Bunge" kunazaliwa kitu kinaitwa "KIKAO CHA BUNGE". Hizi ni idadi ya siku wanazokutana wabunge kujadili jambo fulani. Kila siku inazaa " kikao" kimoja cha mkutano husika wa Bunge husika...

Kila mbunge hulipwa ile inayoitwa "sitting allowance" kwa kila kikao anachohudhuria....

Ndiyo maana wakati Bunge linaendelea "LIVE" utaona kwenye TV yako chini kabisa maandishi haya;

Kikao cha....... Mkutano wa....... Bunge la......... Tarehe.......

Tafsiri yake ndiyo hiyo!

å Mfano leo tarehe 16/6/2020 ndiyo ilikuwa kikao cha mwisho (sijui kilikuwa cha ngapi) kwa mkutano wa ...... katika Bunge la 11 la Ndugai....!

å Na tumesikia mara nyingi mbunge fulani akipewa adhabu ya kutohudhuria vikao kadhaa, mfano vikao 20 maana yake ni siku za vikao vya bunge......

å Na ikitokea mbunge akapewa adhabu ya kutohudhuria mikutano kadhaa, maana yake ni katika ile mikutano minne (4) ya kila mwaka....

å Kumbukumbu zangu katika Bunge hili la Ndugai zinaonesha kuwa wabunge wawili (Godbless Lema na Halima Mdee) walishapata adhabu ya kutohudhuria mikutano yote ya Bunge ya mwaka mzima kwa amri ya Job Ndugai - Spika....
 
Wanaposema adhabu ya Mbunge ni kutohudhuria Mikutano 20, wanamaanisha nini?
 
Exactly, dhana yako iko sahihi...

Kwa kuongezea tu ni kuwa "Bunge" na "Mkutano wa.......wa Bunge la......." ni vitu viwili tofauti....

"Bunge" huzaa kitu kinaitwa "mkutano". Mfano katika Bunge la 11 kulikuwa na " mikutano" kadhaa...

Kwa kawaida kila mwaka, bunge huwa na mikutano 4 (kama sijakosea na hii ni bila dharura) ikiwemo "mkutano" mkuu wa kupokea, kujadili na kupitisha bajeti kuu ya serikali....

Ndani ya "mkutano wa Bunge" kunazaliwa kitu kinaitwa "KIKAO CHA BUNGE". Hizi ni idadi ya siku wanazokutana wabunge kujadili jambo fulani. Kila siku inazaa " kikao" kimoja cha mkutano husika wa Bunge husika...

Ndiyo maana ukiona kwenye TV yako chini kabisa, utaona maandishi haya Bunge la.....Mkutano wa.....kikao cha.......tarehe.......

å Mfano leo tarehe 16/6/2020 ndiyo ilikuwa kikao cha mwisho (sijui kilikuwa cha ngapi) kwa mkutano wa ...... katika Bunge la 11 la Ndugai....!

å Na tumesikia mara nyingi mbunge fulani akipewa adhabu ya kutohudhuria vikao kadhaa, mfano vikao 20 maana yake ni siku za vikao vya bunge......

å Na ikitokea mbunge akapewa adhabu ya kutohudhuria mikutano kadhaa, maana yake ni katika vikao vile vinne (4) kwa mwaka....
Kikao cha 8, mkutano 19, Bunge la 10, maana yake nini? Soma ufafanuzi wake hapa
 
Exactly, dhana yako iko sahihi...

Kwa kuongezea tu ni kuwa "Bunge" na "Mkutano wa.......wa Bunge la......." ni vitu viwili tofauti....

"Bunge" huzaa kitu kinaitwa "mkutano". Mfano katika Bunge la 11 kulikuwa na " mikutano" kadhaa...

Kwa kawaida kila mwaka, bunge huwa na mikutano 4 (kama sijakosea na hii ni bila dharura) ikiwemo "mkutano" mkuu wa kupokea, kujadili na kupitisha bajeti kuu ya serikali....

Ndani ya "mkutano wa Bunge" kunazaliwa kitu kinaitwa "KIKAO CHA BUNGE". Hizi ni idadi ya siku wanazokutana wabunge kujadili jambo fulani. Kila siku inazaa " kikao" kimoja cha mkutano husika wa Bunge husika...

Ndiyo maana ukiona kwenye TV yako chini kabisa, utaona maandishi haya; Kikao cha....... Mkutano wa....... Bunge la......... Tarehe.......

å Mfano leo tarehe 16/6/2020 ndiyo ilikuwa kikao cha mwisho (sijui kilikuwa cha ngapi) kwa mkutano wa ...... katika Bunge la 11 la Ndugai....!

å Na tumesikia mara nyingi mbunge fulani akipewa adhabu ya kutohudhuria vikao kadhaa, mfano vikao 20 maana yake ni siku za vikao vya bunge......

å Na ikitokea mbunge akapewa adhabu ya kutohudhuria mikutano kadhaa, maana yake ni katika vikao vile vinne (4) kwa mwaka....
Mkuu ufafanuzi wako umeongeza kitu.
Asante sana.
 
Mikutano ya bunge inahesabiwa vipi? Huu unaitwa mkutano wa 11 , kuanzia lini? Mwaka huu?

Kuna mambo matatu hapa:
1. Bunge la .....
2. Mkutano wa .....
3. Kikao cha .....

BUNGE LA...
Ni muda wa madaraka ya bunge, kati ya kuapishwa kwa wabunge wake (mara baada ya uchaguzi mkuu) hadi pale linapovunjwa (na Rais).

Mifano...
2005-2010 Bunge la 9
2010-2015 Bunge la 10
2015-2020 Bunge la 11
2020-2025 Bunge la 12
Mpangilio huo haujalishi Spika ni nani.

MKUTANO WA....
Ni kipindi cha wabunge kuwapo Dodoma bungeni kwa shughuli za kibunge, tangu pale linapoitishwa hadi linapoahirishwa kwa hotuba ya waziri mkuu.

Mfano bunge hili la bajeti (wabunge wameitwa toka walikotoka, wakaenda Dodoma kujadili bajeti, bajeti ikiisha wanakua wamemaliza mkutano namba fulani wa bunge la 11).

KIKAO CHA....
Kwenye mkutano mmoja, wabunge wanakaa vikao vingi (siku nyingi) huko Dodoma. Karibia kila siku, asubuhi na jioni ambapo wakimaliza hivyo vikao (kwa siku husika) wanasaini na zile POSHO.
Kwahiyo mkutano mmoja una vikao vingi.

BUNGE LA... MKUTANO WA... KIKAO CHA...

Naamini nimesaidia kuongeza uelewa wa wanajukwaa wenzangu.
 
Exactly, dhana yako iko sahihi...

Kwa kuongezea tu ni kuwa "Bunge" na "Mkutano wa.......wa Bunge la......." ni vitu viwili tofauti....

"Bunge" huzaa kitu kinaitwa "mkutano". Mfano katika Bunge la 11 kulikuwa na " mikutano" kadhaa...

Kwa kawaida kila mwaka, bunge huwa na mikutano 4 (kama sijakosea na hii ni bila dharura) ikiwemo "mkutano" mkuu wa kupokea, kujadili na kupitisha bajeti kuu ya serikali. Huu Mkutano wa bajeti Mara zote ndiyo Mkutano mrefu zaidi wenye vikao vungi zaidi kuliko Mkutano mingine yote......

Ndani ya "mkutano wa Bunge" kunazaliwa kitu kinaitwa "KIKAO CHA BUNGE". Hizi ni idadi ya siku wanazokutana wabunge kujadili jambo fulani. Kila siku inazaa " kikao" kimoja cha mkutano husika wa Bunge husika...

Kila mbunge hulipwa ile inayoitwa "sitting allowance" kwa kila kikao anachohudhuria....

Ndiyo maana wakati Bunge linaendelea "LIVE" utaona kwenye TV yako chini kabisa maandishi haya;

Kikao cha....... Mkutano wa....... Bunge la......... Tarehe.......

Tafsiri yake ndiyo hiyo!

å Mfano leo tarehe 16/6/2020 ndiyo ilikuwa kikao cha mwisho (sijui kilikuwa cha ngapi) kwa mkutano wa ...... katika Bunge la 11 la Ndugai....!

å Na tumesikia mara nyingi mbunge fulani akipewa adhabu ya kutohudhuria vikao kadhaa, mfano vikao 20 maana yake ni siku za vikao vya bunge......

å Na ikitokea mbunge akapewa adhabu ya kutohudhuria mikutano kadhaa, maana yake ni katika ile mikutano minne (4) ya kila mwaka....
Asante
 
Kwa kadri nijuavyo ni kwamba Nyerere alituongoza miaka 24 (ukigawanya katika awamu ya miaka mitano mitano unapata awamu 4, bunge la awamu ya miaka mitano ya kwanza tunasema ni mkutano wa kwanza wa bunge, kwa hiyo kila bunge la awamu ya miaka mitano inahesabika kama mkutano wa bunge, Kwa Nyerere tulikuwa na mikutano minne ya bunge).

Awamu mbili za miaka mitano mitano ya Mwinyi (bunge la awamu ya kwanza ni mkutano wa tano wa bunge, awamu ya pili ni mkutano wa sita wa bunge)

Awamu mbili za miaka mitano mitano ya Mkapa ( mkutano wa 7 na mkutano wa 8)

Awamu mbili za miaka mitano mitano ya Kikwete (mkutano wa 9 na mkutano wa kumi)

Awamu ya kwanza ya Magufuli ( mkutano wa 11)

Nipo tayari kusahihishwa.
Uko sahihi kabisa.
 
Hesabu hivi 1965 -70, 1970-75, 1975-80, 1980-85, 1985-90, 1990-95, 1995-2000, 2000-2005, 2005-2010, 2010-2015, 2015-2020
Jumla utapata Ni 11
 
Kuna mambo matatu hapa:
1. Bunge la .....
2. Mkutano wa .....
3. Kikao cha .....

BUNGE LA...
Ni muda wa madaraka ya bunge, kati ya kuapishwa kwa wabunge wake (mara baada ya uchaguzi mkuu) hadi pale linapovunjwa (na Rais).

Mifano...
2005-2010 Bunge la 9
2010-2015 Bunge la 10
2015-2020 Bunge la 11
2020-2025 Bunge la 12
Mpangilio huo haujalishi Spika ni nani.

MKUTANO WA....
Ni kipindi cha wabunge kuwapo Dodoma bungeni kwa shughuli za kibunge, tangu pale linapoitishwa hadi linapoahirishwa kwa hotuba ya waziri mkuu.

Mfano bunge hili la bajeti (wabunge wameitwa toka walikotoka, wakaenda Dodoma kujadili bajeti, bajeti ikiisha wanakua wamemaliza mkutano namba fulani wa bunge la 11).

KIKAO CHA....
Kwenye mkutano mmoja, wabunge wanakaa vikao vingi (siku nyingi) huko Dodoma. Karibia kila siku, asubuhi na jioni ambapo wakimaliza hivyo vikao (kwa siku husika) wanasaini na zile POSHO.
Kwahiyo mkutano mmoja una vikao vingi.

BUNGE LA... MKUTANO WA... KIKAO CHA...

Naamini nimesaidia kuongeza uelewa wa wanajukwaa wenzangu.
asante sana tena sana
 
Unaposema "Unaposikia bunge la 11, inamaanisha bunge la spika wa 11 tokea tupate uhuru." yani unamaanisha mwakani Spika akiwa mtu yeyote apart from JOB Ndugai unamaanisha litaitwa bunge la 12?.. Hapo tu andiko lako linakosa uhalali wa kuendelea kusoma ulichokiandika
Ni kweli, hata akiwa Job au mwingine, bunge litaitwa la 12... Lakini katikati ya bunge la 12, spika akiachia madaraka, kwa kuondolewa kwa mujibu wa sheria au kwa kifo, akiingia spika mwingine litaendelea kuwa bunge la 12.. HIVYO DHANA YA KUSEMA UNAHESABU MASPIKA ITAKUWA SAHIHI ENDAPO TU KILA SPIKA ATAMALIZA MUDA WAKE
 
Back
Top Bottom