Elimu haina mwisho; Mikutano ya bunge inahesabiwa vipi?

Mikutano ya bunge inahesabiwa vipi? Huu unaitwa mkutano wa 11 , kuanzia lini? Mwaka huu?

Exactly, dhana yako iko sahihi...

Kwa kuongezea tu ni kuwa "Bunge" na "Mkutano wa Bunge", ni vitu viwili tofauti....

"Bunge" huzaa kitu kinaitwa "mkutano wa Bunge". Mfano katika Bunge la 11 kulikuwa na " mikutano" kadhaa...

Kwa kawaida kila mwaka, bunge huwa na mikutano 4 (kama sijakosea na hii ni bila dharura) ikiwemo "mkutano" mkuu wa kupokea, kujadili na kupitisha bajeti kuu ya serikali....

Huu "mkutano wa Bunge la bajeti" mara zote ndiyo mkutano mrefu zaidi wenye vikao vingi zaidi kuliko mikutano mingine yote......

Ndani ya "mkutano wa Bunge" kunazaliwa kitu kinaitwa "KIKAO CHA BUNGE". Hizi ni idadi ya siku wanazokutana wabunge kujadili jambo fulani. Kila siku inazaa " kikao" kimoja cha mkutano husika wa Bunge husika...

Kila mbunge hulipwa ile inayoitwa "sitting allowance" kwa kila kikao anachohudhuria....

Ndiyo maana wakati Bunge linaendelea "LIVE" utaona kwenye TV yako chini kabisa maandishi haya;

Kikao cha....... Mkutano wa....... Bunge la......... Tarehe.......

Tafsiri yake ndiyo hiyo!

å Mfano leo tarehe 16/6/2020 ndiyo ilikuwa kikao cha mwisho (sijui kilikuwa cha ngapi) kwa mkutano wa ...... katika Bunge la 11 la Ndugai....!

å Na tumesikia mara nyingi mbunge fulani akipewa adhabu ya kutohudhuria vikao kadhaa, mfano vikao 20 maana yake ni siku za vikao vya bunge......

å Na ikitokea mbunge akapewa adhabu ya kutohudhuria mikutano kadhaa, maana yake ni katika ile mikutano minne (4) ya kila mwaka....

å Kumbukumbu zangu katika Bunge hili la Ndugai zinaonesha kuwa wabunge wawili (Godbless Lema na Halima Mdee) walishapata adhabu ya kutohudhuria mikutano yote ya Bunge ya mwaka mzima kwa amri ya Job Ndugai - Spika....
 
Wanaposema adhabu ya Mbunge ni kutohudhuria Mikutano 20, wanamaanisha nini?
 
Kikao cha 8, mkutano 19, Bunge la 10, maana yake nini? Soma ufafanuzi wake hapa
 
Mkuu ufafanuzi wako umeongeza kitu.
Asante sana.
 
Mikutano ya bunge inahesabiwa vipi? Huu unaitwa mkutano wa 11 , kuanzia lini? Mwaka huu?

Kuna mambo matatu hapa:
1. Bunge la .....
2. Mkutano wa .....
3. Kikao cha .....

BUNGE LA...
Ni muda wa madaraka ya bunge, kati ya kuapishwa kwa wabunge wake (mara baada ya uchaguzi mkuu) hadi pale linapovunjwa (na Rais).

Mifano...
2005-2010 Bunge la 9
2010-2015 Bunge la 10
2015-2020 Bunge la 11
2020-2025 Bunge la 12
Mpangilio huo haujalishi Spika ni nani.

MKUTANO WA....
Ni kipindi cha wabunge kuwapo Dodoma bungeni kwa shughuli za kibunge, tangu pale linapoitishwa hadi linapoahirishwa kwa hotuba ya waziri mkuu.

Mfano bunge hili la bajeti (wabunge wameitwa toka walikotoka, wakaenda Dodoma kujadili bajeti, bajeti ikiisha wanakua wamemaliza mkutano namba fulani wa bunge la 11).

KIKAO CHA....
Kwenye mkutano mmoja, wabunge wanakaa vikao vingi (siku nyingi) huko Dodoma. Karibia kila siku, asubuhi na jioni ambapo wakimaliza hivyo vikao (kwa siku husika) wanasaini na zile POSHO.
Kwahiyo mkutano mmoja una vikao vingi.

BUNGE LA... MKUTANO WA... KIKAO CHA...

Naamini nimesaidia kuongeza uelewa wa wanajukwaa wenzangu.
 
Asante
 
Uko sahihi kabisa.
 
Hesabu hivi 1965 -70, 1970-75, 1975-80, 1980-85, 1985-90, 1990-95, 1995-2000, 2000-2005, 2005-2010, 2010-2015, 2015-2020
Jumla utapata Ni 11
 
asante sana tena sana
 
Ni kweli, hata akiwa Job au mwingine, bunge litaitwa la 12... Lakini katikati ya bunge la 12, spika akiachia madaraka, kwa kuondolewa kwa mujibu wa sheria au kwa kifo, akiingia spika mwingine litaendelea kuwa bunge la 12.. HIVYO DHANA YA KUSEMA UNAHESABU MASPIKA ITAKUWA SAHIHI ENDAPO TU KILA SPIKA ATAMALIZA MUDA WAKE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…