Leo nimesafiri kutoka Mwanza kuelekea Dodoma na bus moja. Kwenye hilo bus nilikuwa nasikia mlio maeneo ya dreva nikisikia huo mlio naona kama speed ya bus inapungua. Sasa nimeshindwa kuelewa uhusiano uliopo wa huo mlio na speed ya gari. Speed ya gari ikipungua na mlio unakata. Naomba kuelemishwa kwa anayejua na vp mlio ukiendelea tu kulia nini athari yake.