SoC04 Elimu ijikite kuibua vipaji na kukabiliana na mabadiliko ya teknolojia

SoC04 Elimu ijikite kuibua vipaji na kukabiliana na mabadiliko ya teknolojia

Tanzania Tuitakayo competition threads

ELPHAZ CHARLES

New Member
Joined
Apr 20, 2024
Posts
3
Reaction score
1
Kama ijulikanayo kuwa jamii isiyo na elimu bado iko gizani, tena giza haswa ikizingatiwa sasa dunia imeshapiga hatua kubwa kwenye matumizi ya teknolojia. Hivyo hata kila Taifa liko haile haile kuendana na kasi hiyo.

Mosi, Tanzania inaweza kuungana na nchi nyingine katika hatua hiyo kwa kuboresha mfumo wa elimu ambao utalenga kuchochea na kuwajengea wanafunzi uwezo wa kuwa wabunifu na wajuzi katika masuala ya teknolojia.

Kwanza ifahamike kuwa tayari nchi yetu iko nyuma sana katika mfumo huo, Emu fikiria mwanafunzi wa shule ya msingi hadi sekondari (primary level to advanced level) akikamatwa na simu anafukuzwa shule, lakini huyo huyo aliyekatazwa kutumia simu anatakiwa akifika chuo atumie kompyuta. Je, kujifunzia wapi wakati hata simu haijui? Tubadili hii dhana.

Wanafunzi wafundishe matumizi ya vifaa vya kiteknolojia tangu wakiwa wadogo la sivyo tutaendelea kuwa nyuma nyuma. Tuweke mazingira ya kimashindano kama ilivyo katika umiseta na umitashumita, yaani kila shule na chuo kishiriki kila mwaka katika mashindano ya wazo fulani lenye ubunifu wa kiteknolojia walioufanya kwa walioufanya. Hii itainua Ari ya uvumbuzi na utafiti.

Pili, elimu ijikite kuibua vipaji vya wanafunzi tangu elimu ya msingi hadi vyuoni.
Kwanza tuachane na kasumba kuwa vipaji ni mpira na kuimba pekee kwa sababu saivi kuna michezo ya stand up comedy, sakarakasi, riadha, ngumi na mengineyo ambayo yote imekuwa ajira kubwa duniani.

Hivyo tunaweza kulifanikisha hilo kwa kuanza na majaribio kwa shule kadhaa kwa kila halmashauri (angalau shule 5 kwa kila halmashauri) ambapo katika shule hizo waajiriwe waalimu wenye ujuzi katika uvumbuzi wa vipaji.
Mathalani mwalimu wa michezo awe na elimu ya masuala ya michezo, mwalimu wa kilimo awe na ujuzi wa kilimo vivyo hivyo na katika idara nyingine.

Kwa sababu elimu yetu imekuwa ikiwaandaa wanafunzi kuwa waajiriwa kuliko waajiri, wakulima, wafanyabishara na wanavipaji wakubwa duniani.
 
Upvote 1
Hivyo hata kila Taifa liko haile haile kuendana na kasi hiyo.
Yooh bro, lipo hailehaile ama nn 😁

Wanafunzi wafundishe matumizi ya vifaa vya kiteknolojia tangu wakiwa wadogo la sivyo tutaendelea kuwa nyuma nyuma. Tuweke mazingira ya kimashindano kama ilivyo katika umiseta na umitashumita, yaani kila shule na chuo kishiriki kila mwaka katika mashindano ya wazo fulani lenye ubunifu wa kiteknolojia walioufanya kwa walioufanya. Hii itainua Ari ya uvumbuzi na utafiti.
Mmmh hatutakuwa tumeenda kasi sana kwenye hili maana tujiulize je? Wanafunzi hao wanatumiaje simu zaidi: wanaandika app au wanatumia apps?. Maana simu kama somo na simu kama chombo tu ni vitu viwili tofautii.
Unaonaje wakisoma kwanza nadharia ili waje kuitawala teknolojia kwa vitendo?
 
Back
Top Bottom