Elimu inayumba : Na haya yafutwe?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,137
Reaction score
17,908
Leo yametangazwa matokeo ya Kidato cha Sita waliohitimu mapema mwaka huu. Ingawa imesemwa kuwa ufaulu umepanda,matokeo husika si mazuri hata kidogo.

Mfano,mwanafunzi aliyeongoza kitaifa amepata Daraja la Kwanza la Alama 5 akipata C,A na A kwa mchepuo wa PCM. Ni kutoka Shule ya Sekondari ya Ilboru ya Jijini Arusha.Kimsingi, elimu yetu imefika pabaya. Yaani anayeongoza kitaifa apate 1.5? Mwaka huu hakuna 1.3 wala 1.4. Shule zote za kumi bora zikiwemo Marian Girls,Mzumbe,Feza Boys,Kisimiri na Ilboru hazina taswira nzuri.Vipi ‘shule zetu'?

Ni aibu kwa wadau wote wa elimu. Aibu kubwa.Elimu yetu sasa inapigwa na tufani.Inayumba.Inapoteza mwelekeo. Inaangamia. Inafikia mwisho. Hatari. Matokeo haya ya Kidato cha sita yamesifiwa. Lakini si vutizi.

Nayo yafutwe?
Mzee Tupatupa waLumumba, Dar es Salaam.
 
Dk Ndalichako katoa matokeo, tumsubiri Kawambwa atayakubali au atayakataa.
 
[h=3][h=1] ACSEE 2012 EXAMINATION RESULTS
[/h] S0248 MARIAN GIRLS SECONDARY SCHOOL

Marian mwaka jana ilikuwa ya kwanza
DIV-I = 93 DIV-II = 43 DIV-III = 4 DIV-IV = 0 FLD = 0[/h]
mwaka huu cheki hapo hiyo marian
[h=1] ACSEE 2013 EXAMINATION RESULTS
[/h] [h=3]S0248 MARIAN GIRLS SECONDARY SCHOOL
[/h]
[h=3]DIV-I = 37 DIV-II = 92 DIV-III = 29 DIV-IV = 0 FLD = 0[/h]
 
Mpango ni kuwafelisha zaidi ili wawatawale kirahisi. Umeona wapi watoto wa vigogo wakisoma shule za serikali siku hizi? Imefika hatua hata shule zinazoitwa za vipaji watu wamezisusa kupeleka watoto wao. Wanafunzi wanalalamika, walimu wanalalamika.

Majengo yamechoka, mazingira hayavutii. Ni bora liende tu. Wanashindwa kutwambia tu kwamba sasa kila mtu kivyake abebe mzigo wake.
 
pinda is a disgrace to this country..hajui lolote anaenda enda tu..yuko bize na mambo ya katavi rangers
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…