VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Leo yametangazwa matokeo ya Kidato cha Sita waliohitimu mapema mwaka huu. Ingawa imesemwa kuwa ufaulu umepanda,matokeo husika si mazuri hata kidogo.
Mfano,mwanafunzi aliyeongoza kitaifa amepata Daraja la Kwanza la Alama 5 akipata C,A na A kwa mchepuo wa PCM. Ni kutoka Shule ya Sekondari ya Ilboru ya Jijini Arusha.Kimsingi, elimu yetu imefika pabaya. Yaani anayeongoza kitaifa apate 1.5? Mwaka huu hakuna 1.3 wala 1.4. Shule zote za kumi bora zikiwemo Marian Girls,Mzumbe,Feza Boys,Kisimiri na Ilboru hazina taswira nzuri.Vipi ‘shule zetu'?
Ni aibu kwa wadau wote wa elimu. Aibu kubwa.Elimu yetu sasa inapigwa na tufani.Inayumba.Inapoteza mwelekeo. Inaangamia. Inafikia mwisho. Hatari. Matokeo haya ya Kidato cha sita yamesifiwa. Lakini si vutizi.
Nayo yafutwe?
Mzee Tupatupa waLumumba, Dar es Salaam.