SoC03 Elimu janja ni kuona mbali
Stories of Change - 2023 Competition

Little_me

New Member
Joined
Jun 19, 2023
Posts
1
Reaction score
0
Je, Elimu ni ufunguo wa kufungua milango? Na ni milango ipi haswa, ya maisha?

Kuna mwimbo maarufu uliimbwa ukisema Elimu ni mwanga, kana kwamba unatuangazia kwenye giza, na sio kwenye mwanga kutufunulia vitu vile ambavo tusingeweza ona kwa sababu ya giza.

Siongelei kujumuisha watu wote ila natoa mawazo yangu, elimu imekua gumzo, tatizo, kiwango, biashara, siasa, labda ni pande zake mbili au nyingi.

Je, ushawahi waza elimu bora ni nini? Labda kwa leo tuongelee tu ile elimu wapatayo wanafunzi shuleni.

Kwa wanafunzi walengwa je ni kuhakikisha umemaliza kazi alizokupa mwalimu tu na kuweza kurudia vile alivyofundisha mwalimu darasani na mwisho kufaulu mtihani? Utaskia wanafunzi wakiongelea elimu yao kana kwamba haisaidii, haiwajengi, haiwapi nafasi za ajira, inawapotezea muda, lakini babu na baba zetu walitamani kupata nafasi hii ili waendelee mbele napo ndipo wakasema watahakikisha wamepeleka vizazi vijavyo mashuleni.

Elimu ni mwanga, ni ngazi ukitaka kuona ukitaka kufika itabidi upande. Kuna mapungufu yake lakini kuna mazuri yake kwa nafasi uliyo nayo wewe ni kuajaribu kujipanua katika elimu hio na usiwaze kama awazavyo kila mtu, kumbuka taa imewashwa unaeza kwenda kokote sasa ila usirudi gizani.

Namaanisha badala ya kulalamika, tumia nafasi ya elimu zaidi ya kusema “wanatufundisha vitu ambavyo sivyo”, kuna mwengine aniangalia nafasi hio kwamba kitu hichi naeza nikakitumia.

Kukazia nondo katika nafasi yako, kumbuka unaweza usibadili mfumo wa elimu lakini ukabadili mtazamo na jinsi ya kuwaza.

Kwa wadhamini, Elimu kwenu ni nini? Ni muhimu kujua kwamba mtoto anajua vitu vya msingi kwa kukazia.

Bali akuavyo je, mnathamini nini katika elimu, “We soma tu hata kama ukija kufanya mambo mengine angalau una stashahada” nakubaliana na msemo huo lakini je, ni kweli tunataka kuenda na Elimu kwa mtazamo huo?

Chunguza kwanini mtoto amechagua kitu kisha msaidie kujiendeleza humo pia ukimfundisha yaliyo ya msingi.

Elimu kuwa mwanga sio lazima uwepo darasani lakini ni kokote pale, ila kwa leo tunaongelea hii elimu yetu ya sare na uniform.

popote mtoto aendapo inabidi elimu itukomboe, na sisi kama wadhamini na wazazi tunaeza weka mchango mkubwa kwa kuonyesha nini maana ya elimu na sio tu mtoto kufaulu bila maarifa. Kuna msemo unasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa, vijana wetu wengi sasa wanawaza kuanza biashara, siwalaumu lakini ni vema kama tangu mwanzo tungewasaidia kuona upande mwengine wa Mwanga huu.

Kwa wapanga mikakati, Elimu sio mashindano wala biashara tu ina mambo mengi. Haya ni mawazo yangu tu, tutengeneze njia ya kuwakuza watu kwa kutaka wenyewe kama ilivyo mtu anavyotaka kuangalia simu yake kila baada ya muda, walimu walezi wafundishe kwa kufanya mtu atamani kuwa kama yeye au kuwa na uelewa kama yeye.

Ya nini kuwa na buyu tupu la asali, baada ya kupata shida zote kulipata?

Kwa mfano kufundisha kwa kuwasaidia wanafunzi wasijione kukosea ni shida, kufundisha wanafunzi kuwa na ujasiri na kuweza kujielezea vema.

Kuuliza maswali yatakayo fikirisha na sio kukaririsha.

Kuwa na vipindi vya kujielezea hii itasadia, hasa kwenye afya ya akili. Hasa katika level ndogo za Elimu.

Kwa wazazi watarajiwa panga kujihusisha vema na elimu umpatiayo mwanao, ili hata akija kulalamika ujue ulijaribu kila kitu.

Kwa Viongozi, Kwanza tunawashukuru kwa kazi nzito wanayofanya kuhakikisha elimu inasambaa, hicho ni kiasi, tungependa pia kuongezewa ubora, ubora upo haswa. Ila naongelea Ubora wa Elimu itakayotubeba, itakayotufikirisha, itakayotufanya tusikae chini kusema mfumo haukutusaidia.

Moja ya njia ni kuskiliza mapendekezo ya wanafunzi, labda kwa kukusanya mapendekezo kila mwaka kutoka shule mmoja kwa kila mkoa.

Wanafunzi na wazazi wenyewe hasa wanafunzi wapewe nafasi yao kujieleza. Naam wanafunzi hasa wa vyuo vikuu kwani wao wamepitia yote hayo katika levo za chini,

Tuipe nafasi tena Elimu hii, tuone Mwanga mkubwa ukiwaka.

Mimi pia nlipata nafasi ya kusoma hapa na pale, Nlipenda sana elimu na vyote nlivyojifunza lakini ikafika wakati nikaanza kusahau thamani yake, unakutana na watu wanakuambia jinsi elimu yako inaweza iaikusaidie, lakini si kweli.

Tukijenga uaminifu na kuboresha thamani ya elimu yetu hatutoyumbishwa bali tutafungua milango zaidi tu, na vyote viwili au zaidi vitakaa pamoja.

Kumbuka Elimu sio ajira, elimu si kwa ajili ya kukutambulisha, Elimu si kwa ajili ya maonesho, Elimu yaweza onekana hivo kwa nje lakini wewe kwa ndani beba maana yake, itakayokua na maana kwako.

Kaa na rafiki, mwenzako wa kazi, mwanafunzi mwenzako na mjadiliane picha ya Elimu ambayo mngependekeza. Kisha utoe maoni yako pia.

B19E9229-8B9F-45EF-98D5-AF4462C3E843.jpeg
 
Upvote 0
Back
Top Bottom