kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,677
Licha ya kuwa mataifa mengi yamesaini mikataba mbalimbali ya kimataifa ya kuhimiza elimu kwa wote wanaostahili, mamilioni ya watoto, vijana na watu wazima wamekosa haki hiyo kutokana sababu mbalimbali.
Licha ya kuwa umaskini unaweza kuwa sababu kubwa ya hali hii, zipo baadhi ya nchi ambazo watu wanakosa haki ya elimu kutokana na na ubaguzi wa kijinsia, rangi na dini.
Kwa Tanzania mamia ya watoto wanabaguliwa na kunyimwa haki ya kupata elimu kwa sababu mbalimbali.
Kundi la watoto wenye ulemavu wa aina mbalimbali wanakosa fursa ya elimu kutokana na sababu mbalimbali.
Kundi hili pia linapata shida hata kupata huduma za afya na usafiri.
Katika kukabiliana na hali hii kwa upande wa elimu, imeanzishwa Sera ya Elimu Jumuishi.
Mwanzoni, Elimu Jumuishi ilifahamika kama ni kuwajumuisha watoto wenye mahitaji maalumu katika darasa lenye watoto wasio na ulemavu.
Kwa sasa maana hiyo imebadilka na kuwa kuwashirikisha pia watoto wanaoishi katika mazigira magumu. Mfumo huu wa elimu unawaweka pamoja watoto wenye mahitaji maalumu, wenye uwezo wa juu kiakili, wenye ulemavu na wale wasio na ulemavu.
Lengo la mkakati huu ni kuwawezesha watoto wote wapate fursa sawa ya kupata elimu bora.
Kwa upande wa Elimu Ya Msingi, Elimu Jumuishi inamaanisha maadili yanayotokana na haki za binadamu kwa kutambua kuwa kila binadamu ana upekee wake. Hata hivyo, viko vikwazo vinavyotokana na sababu zinazomkabili mwanafunzi moja kwa moja.
Sababu hizo ni pamoja na ulemavu wa macho, masikio na sehemu nyingine za mwili. Umbali kutoka nyumbani hadi shuleni, miundombinu isiyo rafiki kwa watu wenye ulemavu wa wa viungo, ukosefu wa vifaa vya kufundishia na walimu wasio na ujuzi na uzoefu wa kutosha.
Wizara zinazoshughulikia masuala ya watoto wenye ulemavu ni Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).
Kwa bahati mbaya uratibu wa suala hili hauridhishi kama inavyototakiwa kwa sababu shule zinaendelea kujengwa na mahitaji ya walemavu hayazingatiwi. Miundombinu ya darasani haiwawezeshi wenye baiskeli maalumu kuitumia na vyoo shuleni siyo rafiki kwa walemavu.
Vitabu vya nukta nundu na vielelezo vingine vya kufundishia na kujifunzia havitoshelezi mahitaji.
Mitalaa na walimu wenye ujuzi na uzoefu wa kufundisha walemavu wa aina mbalimbali kama wasioona, viziwi, wenye mtindio wa ubongo hawapo wa kutosha. Hali hii inasababishwa nakukosekana kwa mpango wa kuwa na vyuo vya kutosha vya kuwasomesha walimu wa taaluma hizi.
Inatarajiwa kuwa suluhisho la tatizo hili ni kukubaliwa kwa Rasimu ya Katiba Mpya ambayo imependekeza uwepo wa maelezo kuhusu walemavu. Rasimu hii imependekeza kuwa watu wenye ulemavu ni lazima watambulike, waheshimiwe na wapewe huduma zote muhimu katika jamii.
Huduma hizo ni za afya, elimu, usafiri na pia kupata fursa ya kushiriki katika masuala ya maendeleo ya kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni na kijamii.
Hii ni hatua muhimu sana kwa kuzingatia kuwa watu wote ni sawa. Tunatarajia kuwa maelezo haya yatatekelezwa kivitendo na wala siyo kubaki katika majalada bila kufanyiwa kazi
Chanzo: Mwananchi