Elimu juu ya dawa za kuondoa magugu shambani

Elimu juu ya dawa za kuondoa magugu shambani

Joined
Jul 12, 2017
Posts
27
Reaction score
31
PALIZI YA MAHINDI KWA KUTUMIA DAWA.

Dawa zinazotumika kabla ya mahindi na magugu kuota.

· Katika hatua hii, dawa inayotumika ni aina ya metelaclor+Atrazine.
· Tumia kabla mahindi au magugu hayajaota.
· Tumia wakati hali ya udongo ina unyevu wa kutosha.

· Piga dawa siku ya 1 hadi ya 3 tokea siku ulipopanda mahindi, usipige dawa baada ya siku ya 3. Ni HATARI kwa mahindi yako.

· Tumia maji safi yasio na tope
· Hali ya udongo shambani uwe umelainishwa vizuri wakati wa kulima/kuandaa shamba. Kusiwe na Mabonge
· Usiingie shambani baada ya kupiga dawa.
· Dawa hii ituzuia magugu yasiote na kuruhusu mahindi peke yake yaote.

· Epuka kupiga dawa karibu na vyanzo vya maji
· Epuka kulisha mifugo yako karibu na eneo lililopigwa dawa.

Dawa ya kutumia kama magugu yameota shambani.

Katika mazingira ambayo mkulima aliandaa shamba mapema na muda wa kupanda ukawa umefika.

Lakini unakuta shamba limeota nyasi, huna haja ya kuvuruga tena shamba lako ili kuua nyasi, tumia dawa mbili kwa kuchanganya. Moja iwe ni aina ya Paraquat changanya na Dawa yenye Metalaclor+Atrazine Au Dawa aina ya GSlyphosate changanya na ile yenye Metalaclor+Atrazine,

Uchaguzi wa dawa utategemea aina ya magugu na hatua yaliyofikia katika kukua kwake. Tunashauri Mkulima atumie njia hii zaidi kwa uhakika, mvua zikinyesha usikimbilie kupanda. Subiri kama wiki 2 au 3 ili majani yaote kwa asilimia kubwa, hasa kwa wale wanaoandaa mashamba kipindi cha kiangazi au mara baada ya kumaliza kuvuna.

· Hakikisha kipindi cha kuandaa shamba liwe limeandaliwa virizuri kwa kulainisha udongo na kuondoa takataka zote shambani.

· Ingia shambani, panda mahindi yako kukiwa na nyasi hivyohivyo.
· Piga dawa kwa kuchanganya kama maelezo hapoya juu.
· Tumia maji safi yasiyona tope
· Piga dawa siku ya 1 hadi ya 3 tokea siku umepanda mahindi

· Hakika siku ya kupiga dawa kuwepo unyevu wa kutosha shambani, udongo uwe na unyevu wa kutosha.

· Usiingie shambani baada ya kupiga dawa

· Mchanganyiko huu, dawa moja itaua nyasi zilizohai na nyingine itazuia zingine zisiote bali itaruhusu mahindi peke yake yaote.

· Tumia Nozeli inayoshaouriwa kwa kupiga dawa za magugu
· Epuka kupiga dawa karibu na vyanzo vya maji
· Epuka kulisha mifugo yako karibu na eneo lililopigwa dawa.

Kupanda pasipo kulima-Jembe la Dawa (Zero Tillage)
Mfumo huu ni mzuri kwa wale wenye mashamba ambayo udongo wake ni laini, tifutifu. Huna haja ya kulima shamba lako (labda kama kuna vichaka na visiki ambayo kwa hakika utatakiwa kufyeka na kung’oa), kazi yako ni kusubiri mvua zinyeshe kwa wingi ili udongo ulowane kwa kiasi cha kutosha.

Dawa ya kutumia katika mazingira haya ni aina ya Glyphosate changanya na ile yenye Metalaclor+ Atrazine.

· Baada ya mvua kudondoka/kunyesha subiri kama wiki 2 au 3 ili kuruhusu nyasi ziote kwa wingi

· Piga dawa mahindi yako kukiwa na nyasi
· Piga dawa kwa kuchanganya kama tulivyoeleza hapo juu.
· Hakikisha siku ya kupiga dawa kuwepo unyevu wa kutosha kwenye udongo.

· Mchanganyiko huu, dawa moja itaua nyasi zilizo hai na nyingine itazuia zingine zisiote bali mahindi peke yake ndiyo yataota.

· Tumia Nozeli inayoshauriwa kwa kupiga dawa za magugu.
· Epuka kupiga dawa karibu na vyanzo vya maji.
· Epuka kulisha mifugo yako karibu na eneo lililopigwa dawa.

Dawa ya kutumia kama mahindi na magugu yameota

Katika hali ambapo mahindi na magugu yameota, na kama shambani kwako asilimia kubwa ya magugu ni ile aina ya majani mapana. Dawa ya kutumia hapa ni 2,4D-Amine. Au Atrazine

· Panda shamba lako kisha subiri mahindi na nyasi viote
· Piga dawa yeyote kati ya hizo hapo juu
· Tumia maji safi yasiyo na tope
· Piga dawa mahindi yakiwa yamekuwa kwa inchi 4 hivi, majani 4 na sio zaidi

· Epuka kupiga dawa mahindi yakiwa zaidi ya majani 4, yatadumaa.
· Usiingie shambani baada ya kupiga dawa

· Dawa hizi huua majani na kubakiza mahindi, lakini zinaua magugu aina ya majani mapana peke yake.

· Tumia nozeli inayoshauriwa kwa kupigia dawa za magugu
· Epuka kupiga dawa karibu na vyanzo vya maji.
· Epuka kulisha mifugo yako karibu na eneo lililopigwa dawa.

Dawa ya kutumia kwa palizi ya pili.
Palizi ya pili mara nyingi hufanyika kabla ya kuweka mbolea ya kukuzia, kabla mahindi hayajatoa mbelewele. Dawa inayotumika wakati huu ni ile aina ya paraquart.

· Piga dawa kabla ya kuweka mbolea ya kuzuia
· Piga dawa mahindi yakiwa tayari yametengeneza pingili/miwa
· Tumia maji safi, yasiwe na tope
· Eleza Nozeli ya pampu chini kwa chini na piga katikati ya mstari
· Epuka kupiga dawa kukiwa na upepo mkali

· Tumia Nozeli inayoshauriwa kwa kupigia dawa za magugu
· Usiingie shambani baada ya kupiga dawa.
· Epuka kupiga dawa karibu na vyanzo vya maji
· Epuka kulisha mifugo yako karibu na eneo lililopigwa dawa.

FAIDA YA MATUMIZI YA DAWA ZA PALIZI

· Haiharibu ardhi kwa mmomonyoko au kwa kulima na kugeuza udongo mara kwa mara

· Huokoa muda
· Hukufanya ufanye shughuri zingine za kiuchumi
· Hukufanya upanue shamba na kulima zaidi
· Rais kusimamamia hata kama shamba liko mbali
· Hufanyika kwa muda mfupi,
· Unahitaji vibarua wachace
· Hukupa mavuno mazuri na mengi.


ONYO:
TUMIA DAWA KAMA ILIVYOANDIKWA KWENYE KIBANDIKO AU FUATA MAELEKEZO YA WATAALAMU WA KILIMO KUEPUKA MADHARA/HASARA.


B: PALIZI YA DAWA KWENYE MPUNGA
Viuagugu vinavyotumika kabla majani hayaota.
Katika hali ambayo majani hayajaota shambani, tumia kiuagugu aina ya pendamethatlin au aina ya Oxidiazon 250g/lt.

· Andaa shamba lako vizuri kwa kuchabanga udongo vizuri
· Hamisha miche yako kutoka kwenye kitalu na kupandikiza shambani

· Puliza dawa yoyote kati ya hizo hapo juu baada ya kupanga Mpunga, kabla magugu hayajaota

· Hakikisha umekausha maji shambani masaa 24 kabla ya kunyunyizia dawa
· Usiingie shambani baada ya kupulizia viuagugu

· Viuagugu hivi huzuia majani kuota kwa kutengeneza kitu kama utandu juu ya udongo/ardhi.

Viuagugu vinavyotumika baada ya magugu kuota.
Iwapo magugu yameanza kuota shambani tumia viuagugu aina ya pretilaclo, Pyribenzole, Tiller Gold, penoxulum (Rainbow), propanil, Garil, 2,4D Amine, Bentazole 480g/It.

· Andaa shamba lako vizuri kwa kuchabanga udongo ili kualainisha.
· Pandikiza miche ya Mpunga
· Subiri hadi majani yaanze kuota
· Pulizia kiuagugu chochote kati ya hivyo hapo juu

· Uchaguzi wa dawa utategemea aina ya magugu yaliyoko shambani mwako, mfano zipo zinazoua ndago na nyingine huua punga punga, nyingine huua majani mapana peke yake mfano ni 2, 4D- Amine.

· Hakikisha wakati unapiga dawa magugu yawe katika hali ya kuota vizuri, yasiwe yamenyauka.

· Hakikisha udongo uwe na unyevu wa kutosha
· Kumbuka kukausha maji shambani masaa24 kabla hajanyunyiza kiugugu
· Pata ushauri kwa muuzaji wa pembejeo aliye karibu, atakuelekeza dawa inayofaa kwa shamba lako .

· Usiingie shambani baada ya kupiga dawa.
· Viuagugu hivi huua majani na kuacha Mpunga.

Matumizi ya Glyphosate katika kuandaa shamba la Mpunga.
Katika hali ambayo shambani kuna majani sugu kama vile pungapunga, ndago, sangari nk. Tunashauri mkulima atumie kwanza kiagugu aina ya Glyphosate wakati wa kuandaa shamba.

· Fungulia maji shambani ili kuruhusu majani yote yaote kwa wale wa kilimo cha umwagiliaji, lakini kwa wale wanaotegemea mvua basi subiri mvua zinyeshe na majani yaote kwa wingi.

· Piga dawa inayopendekezwa hapo juu.
· Subiri siku kati ya wiki 2 hadi 4 ili majani yote yaungue

· Baada ya hapo unaweza kuingia shambani na kupanda Mpunga , au unaweza kuvuruga shamba lako kwanza halafu panda Mpunga.

· Fuata Masharti mengine yote kama iliyoainishwa hapo juu.

Viuagugu vinazotumika kwa kilimo cha Nchi kavu/ kisicho umwagiliaji

Matumizi ya Dawa aina ya Glyphosate.

· Katua shamba lako mapema kipindi cha kiangazi.
· Mvua za mwanzo zikinyesha, subiri majani yaote yote

· Subiri wiki 3 hadi 4 ndipo umwage mbegu shambani, hii ni kuruhusu magugu yote yafe /yaoze

· Siku ya kumwaga mbegu,vuruga shamba lako viruri.
· Dawa hii huua nyasi sugu aina ya ndago na mpunga punga na aina nyingine mbalimbali

· Epuka kupiga dawa hii kwenye mpunga uliota, itachoma na kuua

Matumizi ya 2,4D-Amine
Dawa hii inaweza kutumika kwa palizi baada, mpunga na majani vikiwa vimeota. Huua majani mapana peke yake.
 
Kwa hiyo hakuna kupalilia?
Vipi bei inayotosha kwa ekari moja?
 
Asante kwa elimu mkuu.

Unaposema "piga dawa siku ya 1 hadi ya 3.." unamaanisha dawa ipigwe kwa siku zote 3 mfululizo, au siku mojawapo kati ya hizo 3?
 
Mkuu Masalu, asante sana kwa elimu ya kilimo. Kweli kuna changamoto nyingi sana kwenye kilimo na ulichokionyesha hapo juu ni suluhu ya sehemu ya hizo changamoto. Ombi langu ni vema utupatie mawasiliano yako (simu au unapatikana wapi) ili tuweze kuwasiliana na wewe kwa ushauri zaidi.

Mfano; mimi nitahitaji sana dawa hizo na ningependa nipate mwongozo wako, maana kwa soko huria hili dawa ziko aina nyingi sana, na kila moja utaambiwa inafaa kwa matumizi hayo. Asante kwa kunielewa
 
Mkuu Masalu, asante sana kwa elimu ya kilimo. Kweli kuna changamoto nyingi sana kwenye kilimo na ulichokionyesha hapo juu ni suluhu ya sehemu ya hizo changamoto. Ombi langu ni vema utupatie mawasiliano yako (simu au unapatikana wapi) ili tuweze kuwasiliana na wewe kwa ushauri zaidi. Mfano; mimi nitahitaji sana dawa hizo na ningependa nipate mwongozo wako, maana kwa soko huria hili dawa ziko aina nyingi sana, na kila moja utaambiwa inafaa kwa matumizi hayo. Asante kwa kunielewa
namba zangu ni 0758583098
nipo mkoa wa njombe
 
Asante kwa elimu mkuu.

Unaposema "piga dawa siku ya 1 hadi ya 3.." unamaanisha dawa ipigwe kwa siku zote 3 mfululizo, au siku mojawapo kati ya hizo 3?
inategemea na Maelezo ya dawa kwani dawa zinatofautiana na Kila dawa ina Maelezo yake
 
Kuna sumu ya kupulizia miti na kuikausha?

au sumu ya kupulizia shamba pori?
 
Hivi ukitumia Multi glysophate pekee haiwezi kufanya kazi mkuu? maana hiyo paraquat haipatikani.
Kuna dawa tofauti tofauti hata nyingine Mimi sijaziolodhesha lakini nazo ni nzuri na zinafanya kazi vizuri ata hiyo multi glysophate ni nzuri
 
Masalu asante kwa uzi wako. Ingawa namba uliyotoa haipatikani.naomba kuuliza jembe dawa hapo juu umesema tutumie
Glyphosate na Metalaclor+ Atrazine. Umeelezea jinsi ya kutumia dawa. Je ni wakati gani unapanda? Baada ya kupiga dawa au kabla ya kupiga dawa? Au unapanda na majani kisha unapiga dawa kwa case pale hujalima na trekta unataka uue nyasi upande?
 
Back
Top Bottom