Elimu juu ya dawa za kuondoa magugu shambani

Elimu juu ya dawa za kuondoa magugu shambani

Masalu asante kwa uzi wako. Ingawa namba uliyotoa haipatikani.naomba kuuliza jembe dawa hapo juu umesema tutumie
Glyphosate na Metalaclor+ Atrazine. Umeelezea jinsi ya kutumia dawa. Je ni wakati gani unapanda? Baada ya kupiga dawa au kabla ya kupiga dawa? Au unapanda na majani kisha unapiga dawa kwa case pale hujalima na trekta unataka uue nyasi upande?
kuna dawa zinazopigwa wakati kabla hujapanda Na dawa zinazopigwa wakati umeshapanda mfano round up ni dawa inayopigwa kabla hujapanda Na ukipuliza unakaa siku 10 adi 14 ndio unapanda lakini kuna dawa kama tiller gold kwenye mpunga inapulizwa wakati umeshapanda Na mpunga umeota
 
Je hizo dawa zinaleta athari gani katika udongo? Kama ukizitumia mfululizo, Kuna kipindi itabidi ulipumzishe shamba?
 
dawa hizi ni dawa ambazo zimetengenezwa kwaajili ya kuingilia mfumo wa ukuaji wa magugu na hazina madhara sana kwenye udongo kiasi kwamba ukapumzisha shamba kwa ajili ya dawa hapana ila kwa nini tunapumzisha shamba kwa sababu kazi ya udongo uliopo shambani ni kuupa mmea virutubisho na virutubisho hivyo hupungua kadri vinavyozidi kutumika na mimea mfano unamahindi stoo kila siku unachota kidogo unasaga lazima kunasiku mahindi yataisha ndio ilivyo kwenye udongo kadri mimea inavyozidi kutumia virutubisho ndio jinsi vinavyopungua na kufanya shamba likose rutuba ndio hapo utakutana na habari ya kupumzisha shamba ili kutunza rutuba ya udongo
Je hizo dawa zinaleta athari gani katika udongo? Kama ukizitumia mfululizo, Kuna kipindi itabidi ulipumzishe shamba?
 
Vipi kwenye palizi ya ufuta tunatumiaje mkuu nataka nisitumie vibarua kupaalilia
 
Naomba kusaidiwa dawa nayoweza kutumia kwaajili ya palizi kwenye mihogo
 
Atrazine ni dawa hatar saana kwa hormones za binadamu unapo tumia hakikisha haigusi mwili wako
 
Back
Top Bottom