Salamu Wanajukwa,
Huwa najiuliza mara nyingi sana hili swali na ningetamani sana kujua kwa Wajuvi wa mambo.
Kufariki kwa kiongozi mkubwa wa kitaifa ni swala la nchi lakini pia linagusa maslahi mapama ya kiusalama.
Viongozi ni binadamu kama sisi na wanawasiliana na viongozi wengine kwa protocols flani either kwa simu, komputer au barua.
Mawasiliano haya yanaweza kuwa ya kibinafsi, ya siri au ya kimkakati. Ulishawahi kujiuliza kiongozi akifariki handling ya simu yake, PC na documents za mawasiliano yake huwa zikoje.
Je, wanaachiwa familia wachukue tu vitu hivyo au vinafanyiwa security clearance kwanza ndo wapewe au vinataifishwa jumla?
Great thinkers, watafiti na wataalam wa mambo mje mtueleze.
Nawasilisha