Elimu kuhusu kisukari

NZURI PESA

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2011
Posts
5,958
Reaction score
2,954
Watu wengi huanzishiwa dawa mara tu akipimwa na kukutwa na sukari ipo kuanzia 10 -12 haswaa wale wa aina ya pili ya.kisukari, kimsingi ni makosa.angalia iwapo kiwango cha sukari yako katika damu ni 4-11 ukiwa hujala chochote hiyo ni normal range.

Na inapo kuwa 4-14 ukiwa umekula ni normal kwahiyo unachopaswa kifanya ni kwamba ukipima kiwango utakacho pata utoe 11 ambayo ni maximum range

kwa mfano umepima ukakuta ipo 15 utoe 11 utapata 4 hivyo kiwango kilichozidi ni hiyo 4 ambayp unaweza kuimudu kuipunguza bila dawa karibuni kuchangia na nipo tayari kurekebishwa.
 
Safi sana mtaalamu kwa kutoa somo,nilisikia Unga wa majani ya mlonge ukiwa unatumia kijiko kimoja cha chai mara mbili kwa siku(asubuhi na jioni-una mix kwenye chai au uji au maji) nayo ina-control kiwango cha sukari mwilini,ni kweli?
 
Safi sana mtaalamu kwa kutoa somo,nilisikia Unga wa majani ya mlonge ukiwa unatumia kijiko kimoja cha chai mara mbili kwa siku(asubuhi na jioni-una mix kwenye chai au uji au maji) nayo ina-control kiwango cha sukari mwilini,ni kweli?
nikweli unga wa mlonge unasaidia kurekebisha kiwango cha sukari mwilini lakini uuandae mwenyewe pia uunywe kwenye uji si chai na kama utatumia chai basi usi ichuje mkuu unywe na makapi.
NB: UKIWEZA TUMIA JUISI YA MLONGE
 
Wastani wa kiwango cha sukari mwilini hupimwa ukitegemea nyanja mbili, endapo mtu amekula kitaalam wanaita "Random blood glucose(RBG)" na pale endapo mtu akiwa hajakula "Fasting blood glucose(FBG)".

Wastani (normal range) ambayo inabidi uipate kabla mtu ajala chochote (FBG) ni 4.4 to 6.1 mmol/L (79.2 to 110 mg/dL) ila kushuka kidogo au kupanda kidogo inaweza isiwe shida inategemea mtu na vyakula anavyokula na shughuli anazofanya. Na akishakula (RBG) inaweza kupanda 4.4 to 7.8 mmol/L au zaidi kidogo.

Na kuhusu kuanzishiwa dawa mkuu inategemea kwanza ni aina gani ya kisukari maana kuna mpaka kisukari kinachowapata kina mama kipindi cha ujauzito na kinaondoka chenyewe baada tu ya mama kujifungua.

Ila tukumbuke sana magonjwa haya tunaweza KUEPUKA kwa kula vizuri (diet) na kufanya mazoezi ya kutosha.



@ joseverest nadhani utakua umepata idea kdg [emoji23]






Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app
 
Aisee nashukuru kidogo nimeelewa
 
Sawa mkuu,inakuwaje kama umepima ukakuta ni chini ya 11...
 
Naomba kujua sababu za mtoto kupatwa na tatizo la kisukari

Sent from my HUAWEI Y360-U61 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…