Mwanamaji
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 2,905
- 4,518
Zifuatazo ni hatua 9 za kufuata ili kupata cheti cha tathmini ya athari za mazingira kwenye mradi wako;-
1. Usajili (Registration)
Sajili mradi wako kwa kujaza fomu maalum ya maombi ya usajili kwenda baraza la taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira (NEMC). Gharama yake ni 70,000/=.Kwa siku za karibuni kuna mfumo wa kimtandao (online system) wa kufanya usajili.
2. Upembuzi (Screening)
Fomu ya maombi iliyojazwa pamoja na muhtasari wa mradi (project brief) vilivyowasilishwa NEMC, vitafanyiwa upembuzi ili kujua kama kuna haja ya kufanyiwa tathmini ya athari kwa mazingira ama la. Inachukua siku 45.
3. Tathmini awali (Scoping)
Lengo la hatua hii ni kutambua masuala muhimu (important issues and concerns) yatakayofanyiwa kazi wakati wa tathmini ya athari mazingira. Masuala haya yanawasilishwa NEMC kabla ya kupewa ruhusa ya kufanya tathmini kwenye mradi.
4. Tathmini ya mazingira (Environmental assessment)
Hii ni tathmini ya athari za kimazingira za mradi husika. Inaangazia athari za muda mfupi na mrefu pamoja na kupendekeza njia mbadala za kupunguza athari hizo kwa mazingira na jamii kwa ujumla.
5. Mapitio (Review)
Ripoti ya tathmini ya athari za mazingira, iliyowasilishwa NEMC, itafanyiwa mapitio na kamati ya wataalamu washauri katika muda usiozidi siku 60.
6. Marekebisho (Improvement as recommended)
Endapo kutakua na maoni au marekebisho toka kwa kamati ya wataalam washauri, ripoti ya tathmini ya mazingira itafanyiwa maboresho kwa mujibu wa mapendekezo hayo.
7. Kuwasilishwa kwa waziri (Submission)
Ripoti iliyofanyiwa marekebisho itawasilishwa kwa Waziri mwenye dhamana na mazingira kwa kupitia NEMC.
8. Kukubaliwa (Approval)
Waziri akikubaliana na ripoti iliyowasilishwa kwake, atasaini cheti cha mazingira kwa ajili ya mradi husika. Waziri anayo mamlaka ya kukubali au kukataa, na vyovyote iwavyo, anatakiwa kufanya hivyo ndani ya siku 30.
9. Kupewa cheti cha mazingira (Issuance of certificate)
Baraza (NEMC) litampa muombaji cheti cha mazingira na pia litaambatanisha na masharti anayotakiwa kuyafuata katika uendeshaji wa mradi wake.
NB;
Mleta uzi huu ni mdau wa mazingira, unaweza kuwasiliana nae kwa namba 0767493835 kwa jambo lolote linalohusu tathmini za athari za mazingira au mambo mengine ya kimazingira kwa ujumla wake.
Courtesy of NEMC.

- Tumia wataalam wa mazingira waliosajiliwa (environmental experts) katika kuyatimiza hayo yote yaliyotanabaishwa hapo juu.
- Tembelea tovuti rasmi ya baraza la taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira (NEMC) www.nemc.or.tz kupata orodha ya wataalam waliosajiliwa na masuala mengine mengi ya kimazingira.