Chorter
Member
- Jul 8, 2017
- 41
- 68
Habari wanaJF, Mimi ni kijana niliyehitimu shahada ya bsc in math and ICT kutoka chuo kikuu Cha Mzumbe Morogoro mwaka 2018.
Kipindi nipo chuo mtazamo wangu nilikuwa nawaza nisome nimalize chuo then niajiriwe, kwakweli nilijitahd sana kusoma kwa bidii na namshukuru sana Mungu nilifanikiwa kumaliza chuo na kupata shahada yangu ya kwanza.
Baada ya kumaliza chuo nikaanza shughuli za kupambana na maisha ya mtaani kwakutumia msingi wa elimu niliyonayo, nikatafuta tempo na kwa bahati nzuri nilipata sehemu ya kujiegesha kwenye shule moja ya private mbeya mjin, ambapo kimcngi nlikuwa natumia nguvu nyingi sana kufundisha tena mda mwingine nlikuwa najitoa mpaka mda wa ziada kufundisha lakini malipo yalikuwa hafifu mno, miezi mingine ilikuwa inapita bila kulipwa alafu nikijaribu kufatilia majibu ninayopewa n shule haina pesa.
Kwakweli ikafika muda nikaamua kuacha iyo kazi, nkaumiza sana kichwa juu ya kazi gani niifanye ili atleast nijikeep bize nikashindwa kupata, mwaka 2019 mwezi wa sita nkaona Bora niende kijijini kwetu Rungwe- Tukuyu ili nikaangalie kama naweza kupata shughuli yoyote ya kufanya kwabahati nzuri nilivyofika nikakuta ni kipindi ambacho watu walikuwa wanavuna sana tangawizi,
Nikajikuta nimetamani sana kujua kiundani kuhusu ili zao, ikabidi nianze kufuatilia mambo mbalimbali kuhusu tangawizi kuanzia namna inavyolimwa mpaka mavuno na Bei yake sokoni, kwakipindi kile gunia moja la tangawizi lilikuwa linanunuliw sh laki 2 na 50 shambani, nilivutiwa sana kujihusiha na kilimo hicho, na nikaapa kwamba lazima Mimi pia nilime tangawizi mwaka ule.
Bahati nzuri Tukuyu ni nyumbani kwahiyo ilikuwa rahisi sana kupata shamba la kulima, nikaongea na wazee wakanipa shamba nusu hekta, na kwenye ishu ya kuandaa nilikuwa na uzoefu wa kulima ko haikuwa shida, kwahiyo shida kubwa ikawa ni mbegu na mbolea.
Nikapambana sana kudunduliza mbegu nikapata kama gunia moja na nusu ( niliomba kwa ndugu na jamaa pia kiasi kidogo nilinunua) mbolea pia nilinunua.
Mwaka 2019 nilifanikiwa kupanda nusu hekta na baadae mwaka 2020 nilivuna gunia 9, nikauza gunia 5 kwabei ya laki 1 na 80 nikapata sh laki 9 nikaamua kununua ng'ombe mmoja mtamba laki 5, nikabakiwa na laki 4 kwaajili ya maandalizi ya shamba kwa msimu mwingine, gunia 4 niliacha kwaajili ya mbegu.
Baada ya mavuno mwaka 2020 nikaamua kutanua shamba nikalima hekta moja, nikapanda izo gunia zangu 4 uku ile laki 4 ikinisaidia kununua samadi ya kupandia na mbolea za chumvi kwaajili ya kurutubishia, n.b kulima na kupalilia nlikuwa nafanya mimi mwenyewe. Mwaka huu 2021 nimevuna gunia 25 nimeuza gunia 18 mwezi wa 8 mwishoni kwa Bei ya tsh laki1 na 40 kwagunia moja nimepata jumla sh 2,520,000 nimenunua kuku 30 wa kienjeji na pikipiki mpa nimempa kijana malengo kwasiku huwa naingiza tsh 7000 kupitia pikipiki na gunia 7 nimeacha kwaajili ya mbegu.
Mwaka huu 2021 nimeamua kutanua ukubwa wa shamba nimekodi hekta 2 na nusu lile la mwanzo sitalitumia, nimeshaliaandaa shamba na tarehe 25 mwezi huu naanza kupanda.
MAMBO YA KUJIFUNZA VIJANA WENZANGU
1. Wasomi tumekuwa wengi sana kuliko rasilimali zinazozalisha ajira, kwahiyo elimu isitufanye tubweteke na kusubili ajira rasmi kutoka serikalini au kwenye taasisi binafsi, fursa ni nyingi mtaani, tuangalie fursa zilizopo katika mazingira yanayotuzunguka. NB: Ikiwezekana turudi ata vijijini katika machimbuko yetu tukaangalie shughuli za kufanya kuliko kurundikana mjini na kuendelea kulalamika kuwa ajira hamna
2. Mimi nimejikuta tayari nimepata system ambayo inanisaidia kuendesha maisha kupitia kilimo na ufugaji saizi nimefika wakati sitamani ata kuajiriwa kwenda kufundisha.
KWAWOTE WATAKAIPENDA KUPATA USHAURI, MASHAMBA YA KULIMA TANGAWIZI (KUKODI) ELIMU JUU YA KILIMO CHA TANGAWIZI NA JAMBO LOLOTE LINALOHUSU UZI HUU KARIBUNI SANA Whatsap 0782284770 na call ya kawaida 0748433159
Ahsante!!!

Upvote
7