SoC04 Elimu ni tunu na zawadi kwa vizazi vyetu mitaala ya elimu ibadilishwe

SoC04 Elimu ni tunu na zawadi kwa vizazi vyetu mitaala ya elimu ibadilishwe

Tanzania Tuitakayo competition threads

LOZANDO

New Member
Joined
May 10, 2024
Posts
3
Reaction score
2
Kwa maono yangu Tanzania tuitakayo kuna baadhi ya vitu vinahitajika kuongezwa na vingine kuondolewa kwenye sekta ya Elimu. Mfano mitaala ya Elimu ya sasa haimuandai mwanafunzi muhitimu, kupata ujuzi ambao anaweza akauhamisha kutoka kwenye maandishi kwenda kwenye vitendo ili kutatua matatizo ya jamii kwa manufaa ya binafsi na taifa kwa ujumla, pia mitaala ya Sasa inamuandaa mwanafunzi kuwa na fikra za kuajiriwa na serikali kuliko kujiajiri, hivyo basi natamani Tanzania tuitakayo na ijayo iandae mitaala ya Masomo kuanzia ngazi ya shule msingi mpaka sekondari Masomo ya vitendo yawe zaidi kuliko nadharia, mfano wanafunzi wawe na Masomo ya kujifunza kuandaa bustani za mboga mboga, ususi, upishi, unyooshaji wa nguo, uandaaji wa bustani, ufundi nguo,nk.

Kuliko wanafunzi wa sasa mwanafunzi muhitimu wa kidato Cha nne hawezi hata kupika chai, wazee wetu walikuwa wakimaliza darasa la Saba au la nne anakuwa na uwezo wa kushona, kupika, ususi, na ufugaji na kujipatia kipato kupitia ujuzi huo kuliko wanafunzi wa sasa anamaliza anakuwa tapeli na omba omba huku akilalamika hakuna ajira, masomo ya vitendo na ujasiria mali yatasaidia kuzalisha wanafunzi wenye weledi wa kusaidia matatizo ya jamii kwa kujiajiri na kuacha kulalamika kuhusu ajira, mfano mwanafunzi anaweza SoMa sayansi baadaye anaweza akihitimu akikosa ajira huku anafikiria suluhisho Akawa na fani nyingine pia mbali na udaktari anaweza fanya kazi ya kutengeneza bustani na ushonaji au upishi, kuliko kulalamika kukosa ajira.

Pia, Ili kuondoa adha ya wanafunzi wanaotoka mbali kufika shuleni na wakati wa kutoka shuleni kwenda nyumbani kwao njiani wanapata dhoruba anuwai mfano kubakwa, kuibiwa, kuuwawa kulaghalaiwa na watu wenye mali wakiwa njiani, nashauri serikali iwe na mabasi ya wanafunzi yatakayoitwa Tanzania School Bus (TASBU), mabasi haya ya wanafunzi yatakuwa maalumu kwa ajili ya wanafunzi, mfano Wakazi wa Dar Es Salaam ukienda sa kumi na mbili kituo kikuu Cha mwendokasi Gerezani- kariakoo unakuta wanafunzi zaidi ya Mia wanasubiria mwendokasi huku wakigombania nafasi ya kuingia kwenye usafiri na raia wengine, wanafunzi wakidondoka na kuumizwa kupigwa viwiko kupoteza hata mabegi yao ya kujifunzia ukiwaona unajiuliza hawa wanapata muda sangapi wa kujisomea usiku, naamini wanafika wamechoka na kulala tu hivyo basi ushauri wangu Tanzania tuitakayo ianzishe mabasi ya wanafunzi kuepusha adha inayokuta wanafunzi sababu ya changamoto za usafiri.

Ili kukuza taifa la wanafunzi wenye weledi wa kimataifa kwa manufaa ya nchi yetu, kila mwaka serikali itoe fursa kwa wahitimu wa kidato sita watakaofanya vizuri zaidi ya 200 kwenda kusoma vyuo vikuu vikubwa Duniani kama Harvard, kwa Kozi zenye uhitaji Kama udaktari uuguzi Engineering uchumi na taaluma nyingine Zaidi zenye uhitaji zaidi kwa jamii, nchini kuna vyuo ndio lakini kupata ladha ya wasomi kutoka vyuo vilivyoendelea kimataifa Ni Bora zaidi. Kila shule za serikali ziwe na Televisheni na kompyuta ili kurahisha zaidi wanafunzi kujifunzia Elimu kwa kuona kwenye luninga baadhi ya Masomo ya vitendo.

Pia ili kukuza taifa la wanafunzi wenye khofu ya mungu na nidhamu iliyoyajuu, walimu wa Masomo ya dini mashuleni waajiriwe na serikali kuliko kujitolea, ili kila shule ipate fursa ya kupata mafunzo ya kiroho na kukuza imani zilizothabiti.

Serikali inabidi kuwasapoti na kuwasaidia wanafunzi na wananchi wenye weledi na vipaji mbalimbali kwa manufaa ya nchi yetu, wapo watanzania wenye ubunifu wa hali ya juu, mfano wapo wanaoweza kutengeneza pikipiki za umeme na maji kutengeneza gari na vingine vingine vingi wabunifu hawa serikali inaweza kuandaa siku ya vipaji nchini tutakayo iita "VIPAJI DAY" siku hii wanatangaziwa ofa nono wananchi mwenye kipaji chochote ajitokeze unaandaliwa uwanja watu wanakuja kuona vipaji na ubunifu serikali inachagua ubunifu utakaonyeshwa na kuwa tumia vijana hawa kwa manufaa ya nchi.

Elimu bure ni muhimu Sana inawasaidia hata wananchi wa kipato Cha chini kupata Elimu bure, lakini Elimu hii ya bure inachangamoto nyingi Sana ikiwemo idadi ya wanafunzi kuwa kubwa kuliko walimu mfano shule moja inakuwa na mwalimu mmoja wa hisabati biolojia kwa kidato Cha kwanza Hadi Cha nne, kila darasa Lina wanafunzi zaidi ya Mia mbili, apo inakuwa ngumu kupata Elimu stahiki inayoendana na ushindani wa uhitaji ya wanafunzi wenye weledi yakinifu, hivyo basi ushauri wangu Elimu bure ifutwe zile hela za Elimu bure, badala yake kuwa fursa kwa wahitimu wa kidato Cha nne na Cha sita watakaofanya vizuri zaidi kuajiriwa na serikalli, ili hata baadaye atasoma chuo kikuu awe tayari ameajiriwa, Elimu ikiwa ni gharama mwanafunzi atasoma kwa uchungu na nidhamu iliyoyajuu.

Pia Kama Elimu ya vitendo itaidhinishwa mitihani ya mwisho ya kitaifa kwa darasa la nne, Saba, kidato Cha nne na Cha sita, iwe ya vitendo na sio ya nadharia mfano Kama mtihani Ni somo la kushona mwanafunzi ashone, Kama Ni upishi mwanafunzi apike, hii itasaidia kupata wanafunzi Bora na wenye weledi yakinifu kuliko wanaopimwa kwa mitihani ya nadharia na kufaulu vizuri huku hawana msaada kwa jamii.

Mwisho, lli kuweza kudhibiti nidhamu na mmomonyoko wa maadili ya wanafunzi na watoto wa kitanzania wenye, ukoroji, utukutu, ubakaji, wizi, unyang'anyi, utoro mashuleni, serikali tuitakayo ijayo ijenge kila Mkoa iwe na jela kwa ajili ya wanafunzi watukutu, ili mwanafunzi mwizi, mbakaji, mporaji, Jambazi, ambaye hataki shule, awe anapelekwa jela hata miezi sita akapate fundisho, kwa kufanya hivyo tutazalisha taifa lenye nidhamu na weledi.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom