SoC03 Elimu rafiki kwa mabadiliko yenye tija

SoC03 Elimu rafiki kwa mabadiliko yenye tija

Stories of Change - 2023 Competition

Athumani malumalu

New Member
Joined
Mar 24, 2022
Posts
4
Reaction score
4
Elimu rafiki, huu ni mfumo wa utoaji maarifa kwa jamii au mwanafunzi yanayo shabihiana na mazingira katika kutenda na kukabiliana na hali halisi katika mazingira hayo. Upatikanaji wa elimu rafiki katika taifa letu imekuwa changamoto kubwa, nahii pengine ni kwasababu ya kile kinacho tajwa kama maendeleo ya sayansi na teknolojia.

Suala hili limekuwa likikwamisha sana jitihada za maendeleo katika vyanzo vya ndani vya mapato na kutegemea Zaidi vyanzo vya nje kama misaada,wataalamu na kadhalika, na kutokana na elimu isiyo rafiki tunajikuta kuwa na idadi kubwa ya wasomi wenye manufaa kidogo sana katika kuchangia na kusaidia maendeleo ya taifa na serikali kuwa na mlundiko wa lawama kutoka kwa jamii juu ya ukosefu wa ajira na kutowazingatia wasomi wa ndani.

Mfumo huu wa elimu katika taifa letu unachangiwa hasa na mamlaka husika kushindwa au kuchelewa kuweka nguvu na kuleta mabadiliko yenye tija katika sehemu zinazo muathiri mwanafunzi moja kwa moja badala yake mamlaka zinajikita hasa katika maeneo yanayo muathiri mwanafunzi kama sehemu ya pili au ya tatu kama vile uongozi,na taasisi na wadau wa elimu. Katika kukabiliana na hili maeneo yafuatayo ni muhimu sana kuwekwa katika uangalizi na ufuatiliaji wa karibu ili kuepusha tatizo hili

Mabadiliko ya kimitaala,mitaala mingi ya shule za shule za serikali imekuwa ikifanyiwa mabadiliko yenye msaada mdogo sana ukilinganisha na uhitaji wa elimu nufaishi katika vizazi. Upunguzaji na uongezaji wa baadhi ya mada katika mitaala hii umekuwa hauzingatii sana katika umuhimu elimu inayotakiwa kutolewa rejea mabadiliko katika mtaala wa Kiswahili shule za msingi inadhihirisha hoja hii.

Usimamizi watunzi binafsi wa vitabu vya kufundishia, ukiachana na watunzi wa serika yani (TIE) Tanzanuia institute of education, kumekuwa na watunzi wengi wa vitabu vinavyo tumiwa sana na wanafunzi mashuleni hasa katika elimu ya kidato cha tano na sita, ambavyo waandishi hawawezi kutajwa kwa sababu za kisheria ila kwa kuipa nguvu hoja hii rejea vitabu vya masomo yafuatayo na matumizi yake katika shule za sekondari jografia,historia,kemia,fizikia,kingereza. Suala hili limekuwa likisababisha wanafunzi kuchukua elimu zinazo kinzana na uhalisia wa mambo kutokana na baadhi ya waandishi kutokuwa mahiri katika masomo wanayo yaandika.

Muda wa ufundishaji wa mtaala mzima na mada elekezi,hili nalo limekuwa tatizo kubwa kwa wanafunzi kushindwa kupata elimu rafiki kutokana na mlundiko wa mada na muda wa elekezi hili linapelekea mwalimu kufundisha mada anazohisi ni zamsingi tu nakupuuza baadhi ya mada anazodhani si za muhimu, shida hii ina athiri hata ratiba binafsi za mwanafunzi kujisomea nje darasa, kwa hesabu za kawaida kabisa mwanafunzi wa kidato cha pili anatakiwa asome masomo yasiyo punguwa 9 na jumla ya mada zisizo pungua 45 hadi 50, hii inapelekea wanafunzi wengi kusoma kwa ajili ya mtihani tu na si kwa ajili yakupata maarifa kwa ajili ya baadae.

Ukumbatiaji wa mada zisizo na umuhimu kabisa katika mitaala ya elimu, rejea somo la bailojia kidato cha nne mada mabadiliko ya kikaboni(organic evolution),historia kidato cha kwanza, Kiswahili darasa la tatu,la nne,la tano na sita kumekuwa na mlundiko wa mada nyingi zenye manufaa hafifu katka maendeleo ya elimu yakujitegemea katika jamii, hvyo basi ni wajibu wa serikali kuliangalia kwa ukaribu suala hili

Mchakato katika uhamisho wa shule, eneo hili ni muhimu sana katika mzingatio miongoni mwa sababu zinazowafanya wanafunzi wengi kushindwa kupata elimu nufaishi kwao nikushindwa kumudu taratibu na sharia za uhamisho, kutokana na baadhi ya shule kutokuwa na walimu au nyenzo za kumfundisha mwanafunzi kulingana na lengo lake katka elimu yake ingekuwa bora kwa mwanafunzi huyu kuhama bila vizuizi katika shule zetu za ndani kwenda katika shule itakayo mhakikishia sio kufaulu tu bali kupata elimu stahiki kulingana na matarajio yake, baadhi nchi jirani zimekuwa na utaratibu huo kuhakikisha wanafunzi wake wanafikia malengo yao bila kuwa na sababu yakukwamishwa na serikali.

Katika taifa letu serikali imekuwa na utaratibu wakumzuia mwanafunzi kuhama kwa muda usiopungua miezi mitatu, baada ya hapo taratibu lukuki zinafuata hasa kwa wanafunzi wanaopatikana katika maeneo ya mbali na shule wanazohitaji kuhamia wanatumia gharama nyingi katika usafiri, chakula na mengineyo jambo ambalo linadhoofisha mapambambano ya mwanafunzi

Mpangilio wa uendeshaji elimu ya juu, katika ngazi za juu yaani elimu ya vyuo vikuu usimamizi wa mamlaka na utaratibu wa uendeshaji mitihani bado ni sehemu yakuzingatiwa sana, je kuna umuhimu wa serikali kushindwa kuweka utaratibu wakusimamia na kuendesha masomo kama ilivyo katika ngazi zingine za elimu?

Chuo kikuu imekuwa miongoni mwa maeneo ya elimu yanayosemwa semwa vibaya na wanafunzi kutokana na dhana zinazozua kauli kama mhazili wako ndio muamumuzi wako wa mwisho jambo linalo athiri saikolojia ya wanafunzi wengi wa ngazi za elimu ya juu inapotokea tatizo lolote la kitaaluma kati ya mwanafunzi huyu na mhazili.

Hivyo basi ni muhimu serikali kuzingatia mambo yanayozungumzwa na wadau wa elimu na kuyafanyia upembuzi yakinifu kwa ajili ya maslahi mapana ya taifa katika kuzalisha wasomi wanoweza kulta tija na mafanikio chanya katika taifa na kupunguza wimbi la utegemezi wa ajira za serikali.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom