Kibanga Ampiga Mkoloni
JF-Expert Member
- Aug 9, 2007
- 18,772
- 8,939
Sioni suala la imani hapo; anyway, mwendawazimu huwezi kumzuia kufanya chochote akiamua; hata kuvua nguo hadharani ni kawaida kwa mwendawazimu. Je, si kweli kwamba Tanga imeboronga? Je, si kweli kwamba magaidi wamefurumushwa huko Tanga jana kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Jeshi? Je, si kweli kwamba Tanga ndio mkoa unaoongoza kwa kuichagua CCM kwa mtindo wa kimbunga? Je, si kweli kwamba mganga wa kienyeji kuotoka Tanga ni Mbunge? Tanga ina tatizo na lisiposhughulikiwa litaisumbua sana nchi huko tuendako.
Ishu ya ugaidi ilikuwa ya kutengeneza japo yapo mengi mabaya ...
Sioni suala la imani hapo; anyway, mwendawazimu huwezi kumzuia kufanya chochote akiamua; hata kuvua nguo hadharani ni kawaida kwa mwendawazimu. Je, si kweli kwamba Tanga imeboronga? Je, si kweli kwamba magaidi wamefurumushwa huko Tanga jana kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Jeshi? Je, si kweli kwamba Tanga ndio mkoa unaoongoza kwa kuichagua CCM kwa mtindo wa kimbunga? Je, si kweli kwamba mganga wa kienyeji kuotoka Tanga ni Mbunge? Tanga ina tatizo na lisiposhughulikiwa litaisumbua sana nchi huko tuendako.
Watu hawataki kusoma, shule zipo tena nzuri , wanakimbilia kuweka kambi kwenye mapango ya amboni unatarajiwa watafaulu kwa miujiza?Shule 10 za mwisho ni;
Manolo mkoa wa Tanga
Chokocho mkoa wa Pemba
Kwalugulu mkoa wa Tanga
Relini mkoa wa Dar es salaam
Mashindei mkoa wa Tanga
Njelekela Islamic Seminary mkoa wa Kigoma
Vudee mkoa wa Kilimanjaro
Mnazi mkoa wa Tanga
Ruhembe mkoa wa Morogoro
Magoma mkoa wa Tanga.
Ishu ya ugaidi ilikuwa ya kutengeneza japo yapo mengi mabaya Tanga lakini mazuri pia yapo tena mengi tu! Bahati mbaya umechukulia Tanga mjini/ ukanda wa pwani na viunga vyake lakini mkoa wa Tanga ni mkubwa na una mengi mazuri tu mbona hususani wilayani Lushoto ambako elimu iko juu kuna vyuo na sekondary schools nyingi tu unazifahamu Soni seminary Kifungilo girls Mazinde juu Magamba Boys ambayo sasa ni chuo kikuu cha Secuco? Chuo cha mahakama ambacho ndio kitaaluma kikubwa Africa?
Tanga mjini kuna chuo kikuu pia, kuna trade schools za Rosminian usisahau Tanga school vyuo mbali mbali vya ualimu kilimo na fani nyingine
Jamani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni! Hata mojawapo ya ikulu kubwa za nchi hii iko Tanga Lushoto tafiti nyingi za mime na wadudu adieu zinafanyika Tanga Tanga kuna mengi mazuri kuliko inavyodhaniwa
Sidhani kama Tanga itashughulikiwa na Serikali ya CCM kwa sababu hali iliyoko Tanga ndio inayopendwa na CCM. Ngao kuu ya Ushindi wa CCM ni Ujinga wa Watanzania waliowengi.Uchaguzi wa Serikali ya Mitaa ulipoisha CCM ikiongozwa na Kinana walianza kuupongeza Mkoa wa Tanga.
Kusema kweli pwani kwà ujumla kuna balaa kwani kila mwaka kila ngazi Fulani ni lazima mikoa hii itakuwa ya mwisho na Kigoma ikiwemo
Mkuu it is very abnormal kwamba nusu ya shule 10 mbovu kabisa kitaaluma zinatoka huko Tanga. No wonder, Tanga inaelekea kuwa lango kuu la ugaidi Tanzania; no wonder Tanga ndio mkoa unaoichagua CCM kwa kimbunga; no wonder Tanga ndipo alipotoka Mbunge wa kwanza Tanzanaia ambaye ni mganga wa kienyeji na hafahamu chaki inafananaje.
Kule tanga uchawi mwingi. Watu wapo busy kupiga ramli huo muda wa kushika kitabu hawana