Elimu Tanzania tumedharau shule za serikali

Kisendi

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Posts
699
Reaction score
179
Ndugu wanabodi Sisi kama WATANZANIA akili yetu imehamia kusomesha watoto wetu shule za private wengine wanaziita international. Mimi juzi nilikuwa benki kila mmoja niliona akiwa bize kujaza fomu za kulipia ada na michango ya watoto wao kwenda kusoma shule za binafsi. Nilichoona ni kubabaika tu kwa watz maana hizi za binafsi zinazid kuuua elimu yetu tanzania kutokana na walimu wanaotumika kwenye shule binafsi si walimi by professional ni watu walioamua kwenda kufundisha kisa wanajua kuongea kiingereza vizuri. Tujitafakari ada tunazolipa...kishule tu cha ajabu ada 1300000...zingine mpaka 2000000.


Mimi kuna mdogo wangu amesoma hizi shule tu za kawaida..tulichokuwa tunakifanya ni kumpa hela ya tuition na kumkazania. Mwisho wa siku amemaliza shule hizo hizo na leo hii yuko chuo kama hao hao wa hizi shule za kufuatwa na magari. Bila sisi watz kukubaliana na kuzikubali shule zetu hatutafika. Tutazalisha mafisadi tu.
 



Ndugu WATU WOTE WAKIAMUA WAPELEKE WATOTO WAO SHULE ZA SERIKALI HAZITATOSHA NA MATOKEO YAKE WATAKOSA NAFASI ZA KUSOMA SEC.MIMI NAPENDA ZIWEPO ZISAIDIWE KUWAHUDUMIA WATOTO WENYE VIPAJI KWA ZINA FACILITIES NA PIA KUWAHUDUMIA WATOTO WA MATAJIRI.ZA SERIKALI ZIBAKI KWA AJILI YA MASIKINI WARAU.
 
Hivyo ni visingizio tu wewe sema huna hela ya kusomesha private
 
kwanini ulikua unampa hela ya tution?
 
Tunaona hata huko private kuna tuition
 
Si kwamba sina hela ya kumsomesha private hebu tujiulize watoto wangapi waliotoka hizo shule za private ni vichwa.......tunaona hata viongozi walio wengi....thinktanker wazuri ukisoma cv zao wengi wamesoma hiziz shule za kawaida....tuna akina zitto...muhongo...mwakyembe....nchemba
...silinde.....jerry slaa....na wengine wengi hii ni mifano...wanaishia kuongoza form six na form four when it comes to higher level hatuwasikia....dogo langu sasa yupo muhimbili anafanya vzuri zaidi ya vizuri
 
unajua kaka wa TZ wengi tunajua mtoto akijua kuongea kingereza ndo anaakili kumbe mmm!! bonge la kilaza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…