Ndugu wanabodi Sisi kama WATANZANIA akili yetu imehamia kusomesha watoto wetu shule za private wengine wanaziita international. Mimi juzi nilikuwa benki kila mmoja niliona akiwa bize kujaza fomu za kulipia ada na michango ya watoto wao kwenda kusoma shule za binafsi. Nilichoona ni kubabaika tu kwa watz maana hizi za binafsi zinazid kuuua elimu yetu tanzania kutokana na walimu wanaotumika kwenye shule binafsi si walimi by professional ni watu walioamua kwenda kufundisha kisa wanajua kuongea kiingereza vizuri. Tujitafakari ada tunazolipa...kishule tu cha ajabu ada 1300000...zingine mpaka 2000000.
Mimi kuna mdogo wangu amesoma hizi shule tu za kawaida..tulichokuwa tunakifanya ni kumpa hela ya tuition na kumkazania. Mwisho wa siku amemaliza shule hizo hizo na leo hii yuko chuo kama hao hao wa hizi shule za kufuatwa na magari. Bila sisi watz kukubaliana na kuzikubali shule zetu hatutafika. Tutazalisha mafisadi tu.