SoC02 Elimu + Teknolojia = Uchumi

SoC02 Elimu + Teknolojia = Uchumi

Stories of Change - 2022 Competition

Kiyoshu Lang

New Member
Joined
Aug 31, 2022
Posts
1
Reaction score
1
Kwanza, salaam kwako msomaji wa andiko hili, lakini pili sifa nyingi na utukufu kwake Allah mwenye enzi hakika ni kwa neema yake pekee mimi na wewe tu wazima wa afya njema.

Kwa kuanza niseme kidogo ni kwanini nimechagua kichwa cha andiko iwe ni Elimu ongeza Teknolojia ni sawa na Uchumi ama kwa lugha nyingine Elimu ongeza na Teknolojia unapata Uchumi, yaani Elimu nzuri na bora ukiongeza na matumizi sahihi ya Teknolojia unapata Uchumi Imara na kinyume chake ni sahihi( vice versa is true) kwa maana ya Elimu duni ongeza matumizi mabaya ya Teknolojia unapata uchumi mbovu. Nitaeleza;

Mfano mzuri na rahisi sana kuweza kutumia katika mada hii ni Taifa letu la Tanzania na watu wake kwa ujumla sisemi Elimu yetu mbaya lakini niseme haituandai sisi kama vijana kuweza kuendana na wakati uliopo yaani karne ya 21 na mambo yake ya Teknolojia ukitaka kuamini hilo pasipo kufikiri sana embu jaribu kufikiri kipaumbele inayopewa somo la computer mashuleni yaani kuanzia msingi mpaka wakati mwingine vyuo vikuu ukiwaondoa wale wanaosoma computer as their core course vyuoni, priority ya somo hili ni ndogo sana kwa wanafunzi na ata kwa walimu pia, utakuta kwa baadhi ya shule zenye neema ya kuwa na computer rooms vipindi vya somo lenyewe wanafunzi wanatumia kama mapumziko ni kwa sababu ya uzito mdogo unaopewa na walimu katika somo la ICT kwa kiswahili TEHAMA sambamba na masomo ya ujasiriamali na fedha/finance kama ambavyo pia nilisikia kwa mbunge mmoja wa viti maalum akisema bungeni 'among things we lack in our educational system is financial literacy' kwa kiswahili moja ya vitu tunavyokosa katika mitaala yetu ni nidhamu ya fedha ama elimu ya fedha na siyo huyo tu ata Robert Kiyosaki mwandishi na tajiri mkubwa wa Marekani aliandika umuhimu wa kufundisha financial literacy katika kitabu chake cha Rich Dad, Poor Dad kwenye ukurasa wa pili.

Nitazungumza sana kwenye haya mambo matatu Elimu, TEHAMA na Uchumi kwa sababu tupo katika karne ambayo hakika TEHAMA imechukua sehemu kubwa sana. na sasa ili TEHAMA lazima Elimu ndipo Uchumi tunaoutaka sisi, walakini kwa sababu ya Elimu duni isiyoendana na wakati, wengi wetu tumeshindwa na zaidi tunaogopa Teknolojia, nasema hivi kwa sababu leo hii zipo biashara nyingi mno za karne hii ya 21 ambazo zimetokana na TEHAMA ambazo zimepata kuwanufaisha kwa kiasi kikubwa wenzetu wachache ambao kwa namna moja ama nyingine wako tayar kupokea vile ambavyo pengine hawakuwahi kuvisikia ama kufundishwa darasani, wazungu wanasema open minded persons. na hapa utagundua kwamba shida si kutokwenda shule ama ujinga si kutokujua kusoma na kuandika hapana ujinga wakati mwingine ni mtu kuamini tu katika kile alichofundishwa darasani na kutokuwa tayari kujifunza vingine vipya na matokeo yake ni uchumi mbovu kwa mtu mmoja mmoja na kwa taifa kwa upana wake.

Kwa uchache nitataja biashara za ki, TEHAMA za wakati huu katika karne hii ambazo kama Elimu na mitaala yetu ingekuwa time based and environmental friendly basi from individual level to national wise tungekuwa katika hatua ya juu na nzuri zaidi kuliko sasa. nazo ni;-

01. Foreign Exchange(FOREX)
yaani kubadili fedha za kigeni, kwa kiswahili. hii ni biashara ya kimtandao japo inafanyika pia traditionaly lakini wengi wanaofanya traditionaly hawaifanyi katika taswira ya biashara ila ni biashara tena yenye soko kubwa na ni kongwe sana ulimwengun kote na ambayo inawapa vijana wengi na watu wa rika zote wenye elimu na ufahamu nayo vipato vikubwa vya uhakka. lakini kwa sababu ya elimu duni na closed minds za wengi wetu basi utasikia huo utapeli, hiyo haifanyi kazi na aina yote ya maneno ya kuogopesha na kukatisha tamaa.

02. CryptoCurrencies
hii pia ni biashara ya kimtandao ambayo inahusisha pesa za mtandaoni yaani pesa zilizopewa jina la 'coins' ambazo unaweza tumia popote duniani within the authorized and permitted countries and companies pasipo kuzifanyia exchange. na soko lake ni jipya na ambalo linakua kwa kasi sana mpaka sasa soko lake halina zaidi ya miongo mitatu, ni biashara nzuri tena yenye uwanja mpana wa mjasiriamali kufanya kazi kama ambavyo nilisema katika FOREX ni trading, kuuza na kununua currencies. lakini kwenye Cryptos kuna trading, lakini pia coin mining, exchange, holding of coins na namna nyingne za individuals kuweza kujitengenezea pesa mfano mzuri ni taifa la Kenya ni miongoni mwa mataifa yanayoongoza katika umiliki wa cryptos na sote tunashuhudia maendeleo ya Kenya yalivyo mazuri . lakini kwa sababu ya ujuzi wa mikosi na mitaala isiyo sahihi tunawasema vibaya walioamua kutake risks hence opportunities, tunakimbia fursa na kuendelea kuumia chini ya mwamvuli wa ajira. hapa chini ni orodha ya mataifa yanayomiliki pesa za mtandaoni kwa mujibu wa gazeti la forbes
inbound2704548423745042080.jpg


03. Direct Selling Businesses
Uuzaji wa moja kwa moja wa bidhaa na huduma kutoka kiwandani kwenda kwa mteja/wateja. ni biashara kubwa pia ya kimtandao na ni tasnia kongwe yenye miaka zaidi ya 80 tangu kuanzishwa kwake na ni moja ya tasnia zilizowahi kuongoza katika pato la dunia(annual turnovers) kwa miaka miwili iliyopita na hapa namna ya ufanyikaji wa biashara ni individual kununua bidhaa ama huduma from a respective company na kisha kupewa access ya kuuza bidhaa za kampuni mtandaoni by recommending to his aquantencies yaan kwa kuzipendekeza kwa wapendwa wake kisha kujitengenezea kamisheni kwa kadri ambavyo mauzo yatazidi fanyika.

Mwisho nimalize kwa kusema, ni wakati wetu sasa wa kubadilika, wa kukubaliana na mabadiliko, wa kuamua kujifunza tena ata ikiwa tulifunzwa hapo awali, wa kuipa nafasi na kuifurahia TEHAMA(embracing technology) na mwisho kuacha ku, critisize pasipo ku, research.

Ahsanteni Sana na Mungu awabariki!
 
Upvote 1
Back
Top Bottom