Mdau, uniformity ya programs ambazo zinahisiwa kuwa sawa ni kitu muhimu katika kufanya wahitimu wa programs hizo toka vyuo tofauti tofauti kuwa angalau na maarifa na ujuzi unaofanana au kukaribiana. Kuna components muhimu za programs hizo ambazo zinahitaji kufanana lakini sio lazima idadi ya masomo yawe sawa. Kuna masomo ambayo ndio moyo wa fani husika (specialized subjects), haya ndio ambayo yalipaswa kuwa harmonized. Hili ndio lilipaswa kuwa jukumu kuu la Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (na naamini ndivyo ilivyo). Nadhani, wamelegea tu katika hili kwani katika taratibu zao na document zao bila shaka zipo.